YOABU ALIKUJA KWA MADHABAHU AMECHELEWA

I WAFALME 2:28-34

UTANGULIZI

Kuna toba inayochelewa. Mtu huyu alikuja kwa madhabahu ya Bwana lakini alikuwa amechelewa hivyo akafa. Hili ni jambo la huzuni nyingi sana, Yohabu alilala hapo madhabauni mfu. Damu yake ililowa madhabahu lakini alikuja amechelewa. Kushika pembe za hekalu haitoshi kwa kuokoka. Yoabu hakuwa mtu wa ibada na kanisa, alikuwa mtu wa vita, jemedari. Yoabu  hakuwa na Imani timilifu hivyo hakumpa Mungu heshima alipokuwa hai, hakuwa na uhusiano na nyumba ya Mungu na kuhani katika maisha yake. Lakini alipokuwa katika hatari alikimbilia nyumba na watu wa Mungu. Yoabu alifika, lakini amechelewa. Neema ya Mungu haipatikani wakati wowote.

Hebu tuone:-

I.  KUNA TOBA ISIYO YA KWELI.

  1. Toba ya Farao haikuwa ya kweli (Kutoka 10:16-17)
  2. Yuda naye alikuwa na toba isiyo ya kweli (Mathayo 27:4) Yuda alitubu kwa mwanadamu si kwa Mungu.
  3. Simon alitubu na kubatiswa, lakini moyo wake ulikuwa kinyume mbele ya Mungu (Matendo 8:13, 22-23)
  4. Ni hatari sana kutubu dhambi bila kumaanisha (Mathayo 12:43-45)

II.  KUNA TOBA YA KWELI.

  1. Zakayo- (Luka 19:6) Zakayo alikuwa tayari kuweka safi maisha yake.
  2. Legioni wa huko wagerasi (Marko 5:1-15)

III.  KUNA TOBA INAYOKUJA IMECHELEWA.

  1. Wakati wa Nuhu, wengi walikuja kwa safina lakini wamechelewa (Mwanzo 7:16)
  2. Esau hakupata nafasi ya kutubu, ijapokuwa alitafuta sana kwa machaozi (Waebrania 12:16-17)
  3. Sauli- “Mungu ameniacha, hanijibu tena wala kwa manabii, wala kwa ndoto (I Sam.28:15)
  • Yoabu naye alijaribu kushika pembe za madhabahu ya Bwana, lakini Mungu hakumjibu.
  • Aliuliwa papo hapo juu ya madhabahu ya Bwana.
  • Alifika, lakini amechelewa sana.

 

MWISHO

  • Kuna uwezekano wewe umtafute Bwana, usimpate, unapomtafuta kwa sababu ya pressure pasipo Roho Mtakatifu (Yohana 6:44)
  • Hatuwezi kuokolewa wakati tunapoenda (personal convenience).Tunaokoka kwa maana Roho Mtakatifu ametuvuta (Methali 1:25-28)

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago