WEDNESDAY SERVICE

NEEMA YA MUNGU HUBADILISHA WATU

NEEMA YA MUNGU NI YA AJABU

TITO 2:11-14

Neema ya Mungu hubadilisha watu. Neema ni kipawa cha Mungu kupitia kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, Neema ni kwa kila mtu atakaye. Neema ya Mungu inapokelewa kwa njia ya Imani. Neema ya Mungu ni Mtu-yaani Yesu Kristo. Neema ni Mungu kutupokea na kutubadilisha ili sisi tufanane na Yesu Kristo.

Siku moja mzee mmoja na mwanawe walitembea Nairobi kwa mara yao ya kwanza kutoka mashambani. Walipofika kwa moja wapo ya manyumba marefu Nairobi walistaajabu kuona “Lift” kwa mara yao ya kwanza wakashangaa sana . Mwana akamuuliza babaye “Baba, na ile ndio nini?” Baba akamwambia mwana “Mimi sijui.” Walishangaa sana mama mzee alipoingia, baadae “lift” ikafunguliwa na pakatoka binti kijana mrembo sana. Baba akamwambia mwanaye “Enda ukamlete mama yako!!’

Neema ya Mungu inatubadilisha kuwa watu wema zaidi. Imesemwa “Ikiwa dini yako haijakubadilisha, basi wewe badili dini yako”. Hebu tuone leo, neema kama chombo cha kubadilisha watu, kuwageuza kuwa watu wapya ndani na pia nje.

Neema ya Mungu inapo pokelewa-Neema ya Mungu inaanza kazi yake mara moja.Kazi ya neema inaendelea katika maisha yetu mpaka mwisho. “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, tupate kuishi kwa kiasi na haki na utauwa. Katika ulimwengu huu wa sasa, tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu, ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema -Tito 2:11-14. Hebu tuone:-

  1. NEEMA INAKARIBISHA (Tito 2:11)
  • Mtume Paulo anasema kwamba (Vs. 11) “Neema ya Mungu imefunuliwa”.
  • Maana yake “Imefunuliwa” ni imedhihirika, imefunguliwa (Epiphany).
  • Yaani Yesu Kristo amekuja duniani Mungu katika mwili.
  • Kufunuliwa maana yake ni kwamba “Mungu amejulishwa kwetu”.
  • Yesu Kristo alimfunua Mungu Baba kwetu sisi.
  • Yesu Kristo alimwambia Filipo “Aliye niona mimi amemwona Baba”-Yohana 14:9
  • Paulo aliandika katika Wakolosai 1:15 “Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote”.
  • Yesu Kristo naye alijijulisha kwetu, alitembea Yudia, Samaria na Galilaya, na nchi za watu wa Mataifa.
  • Sisi hatungefahamu Neema ya Mungu bali na Yesu Kristo kuja duniani.
  • Hivyo Neema ya Mungu ni Yesu Kristo.
  • Pia “Neema imefunuliwa” ina maana kwamba “Nuru imekuja kung’ara gizani”-Yohana 1:4, “Basi Yesu akamwambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe bali atakuwa na Nuru ya uzima” Yohana 8:12.
  • Paulo anatueleza katika Tito 2:11 “Neema imefunuliwa.” Neema hii inatuletea wokovu kwa kila mtu.
  • Hivyo ametualika kwa uhusiano na Mungu.
  • Neema ya Mungu, ni Mtu-Yesu Kristo. Yesu Kristo amefunuliwa sasa yeye si siri tena.
  • Neema anatualika kumjia Mungu. Neema inatukaribisha na kutualika.
  • Katika Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi arusi wasema njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje na yeye atakaye na ayapate maji ya Uzima bure”.
  • Kumbuka neema ni kipawa cha Mungu.
  • Hatuwezi kununua-kipawa ni chako wakati umekipokea
  • Tunapopokea kipawa cha Mungu, Neema ya Mungu mara moja inaingia na kufukuza giza na dhambi ya roho.
  • Kipawa cha Neema ni kipawa cha dhamani sana. Yesu Kristo alilipa gharama kwa njia ya kutoa nafsi yake msalabani. Neema ni bure, lakini gharama kwa Mungu.
  1. NEEMA INAOKOA
  • Mungu anapotukaribisha kwa neema yake pia anatuokoa kwa neema yake.
  • Neema inapotualika, ni lazima neema itufungulie mlango pia.
  • Matendo yetu mema na wema wetu haziwezi kufungua milango ya Mbinguni.
  • Neema ya Mungu kupitia kwa damu ya Yesu Kristo ni ufunguo wa kuingia-Waefeso 2:8-9.
  • Matendo yetu ni kama nguo iliyo chakaa sana. Isaya 64:6 “Kwa maana sisi sote tumekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa kama upepo uondoavyo.”
  • Neema maana yake ni kwamba tusijali wema wetu.
  • Wokovu ni kuhesabiwa haki mbele ya Mungu- Warumi 3:23-26.
  • NEEMA INATAKASA NA KUOSHA SAFI.
  • Tunapompokea Yesu Kristo ndani ya maisha yetu, Roho mtakatifu anaanza kazi ya utakaso na kubadilisha.
  • Tunaishi katika dunia iliyo chafuliwa na dhambi hivyo watu wameumizwa kiasi tofauti tofauti.
  • Kila mtu ana changamoto tofauti, tunapigana na dhambi tofauti, majeraha yetu ni tofauti hau tumejeruhiwa tofauti. Kwa majeraha yetu, hatuna nguvu kuishi maisha atakayo Mungu.
  • Kazi hii ya kuoshwa dhambi ndio utakaso (sanctification).
  • Utakaso ni kazi ya kuendelea ndani ya maisha yetu tangu kuokoka!
  • Katika Tito 2:12 Biblia inasema Neema inatufundisha.
  • Neema ni “Chuo cha Neema” (Grace University).
  • Mwalimu katika chuo hicho ni mmoja tu-Roho Mtakatifu.
  • Kitabu katika chuo hiki ni kimoja tu-Biblia.
  • Neema inatufundisha:
  1. Kukataa ubaya na tamaa za kidunia Tito 2:12
  • Neema si leseni (license) ya kuishi utakavyo.
  • Neema, kwanza inabadili moyo wako, Neema inabadilisha tamaa zako za kale.
  • Neema inabadilisha akili na nia ya mtu.
  • Neema ya Mungu inabadilisha mawazo na tamaa za mwili.
  • Neema inabadilisha tabia ya mtu mbele ya Mungu na watu.
  • Neema inatufundisha kusema ndio kwa yale mema-2 Petro 3:10, Waefeso 4:22-24.
  • Neema ya Mungu inatufundisha kumngojea Bwana Yesu Kristo kurudi duniani.
  • Neema ya Mungu imefunuliwa kwa watu wote hata wewe.
  • Neema ya Mungu inatuweka huru, inatuosha dhambi na kutusaidia kukaa safi kiroho.

MWISHO

  • Neema ya Mungu inaleta wokovu.
  • Neema ya Mungu inatufundisha kusema la kwa dhambi na kuishi maisha ya utakatifu.
  • Neema ya Mungu inatufundisha tumaini ya Baraka ya kumngojea Yesu Kristo kurudi duniani.
  • Je, umefanya nini na Neema ya Mungu?
  • Kama bado hujampokea Yesu Kristo ndani ya maisha yako fanya hivyo sasa.
  • Neema ya Mungu huleta mabadiliko katika maisha.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *