Uncategorized

KANISA MAUTUTI.

MAKANISA SABA YA UFUNUO

UFUNUO 3:1-6.

Maisha yamejaa mambo baridi na ukweli mgumu sana! Kwa mfano, kuna wakati lazima kufanya uamuzi kuhusu maisha ya mpenzi wako, awe mtoto, mama, baba, mume, au mke. Kuna wakati miili hii yetu inakuwa gonjwa zaidi, kiasi hakuna tumaini ya mgonjwa kuishi maisha. Wakati huo jamii nyingi zinalazimika kuamua kusimamisha matibabu ya dawa kwa mpenzi wao na kuacha mpenzi wao afe. Kuna wakati ambao kupona hakika hakupo tena, au dhamani ya maisha haimo tena. Wakati kama huu, unalazimika kumwomba daktari kuzima mashine zake na mpenzi afe mara hio hio. Lakini pia kuna jamii itakayoamua kuendelea kutumia mashine na dawa mpaka dakika ya mwisho. Ukweli huu pia unahusu kanisa la Kristo.  Makanisa yanakufa pia. Kuna makanisa yaliosifika sana kuwa na utukufu na nguvu za Mungu. Sasa makanisa hayo, yanaishi katika utukufu wa hapo awali. Makanisa haya yanaishi kwa mashine za kufuliza lakini ni maututi. Makanisa haya yako na sifa za kuishi na kuwa hai, lakini tayari maututi. Hivi ndivyo ilivyokuwa na kanisa la Sardi. Kanisa la Sardi lilionekana kuwa hai, lakini Tabibu Mkuu alipopima aliona maututi. Tabibu mkuu anawaambia wakristo wa pale Sardi kama hataona ishara ya uzima, yeye atazima ile mashine na kufuliza na kanisa la Sardi halitaishi tena daima!

Tunaposoma juu  ya kanisa la Sardi, ni maombi yangu kwamba sisi wa F.B.C A/River tunajitazama na kujipima pumzi ya roho yetu na kujua hakika hali yetu kama kanisa  na kama binafsi, kwa maana tunaweza kujiona sisi kama tuko hai, kumbe tunakufa. Tunaweza kujiona kama sisi ni kitu na kumbe sisi ni bure kabisa.

Basi, tumuulize Kristo atuonyeshe hali yetu jinsi ilivyo hasa na tumuulize dawa gani inaweza kuturudisha kwa afya na uzima. Hebu nihubiri juu ya kanisa maututi. Tuone je, tunaishi au ni wakati wa Bwana Yesu Kristo kuzima mashine ya kutufulizia hewa:-

  1. UKWELI BARIDI WA HALI YA KANISA LA SARDI (Ufu. 3:1).
  2. Tabibu mkuu
  • Kwa kumtambua na kumfahamu anaye nena katika mlango huu wa maandiko , tunahitaji kutazama Ufunuo 1:16 “Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume na upanga mkali wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.”
  • “Naye alikuwa na nyota saba mkonno wake wa kuume”. Maanake, Yesu Kristo ni yeye anayejua zaidi kanisa lake. Yesu Kristo yupo karibu zaidi na anajihusisha na kanisa lake kwa karibu sana.
  • Yesu Kristo anatazama kwa karibu mambo na kazi ya kila kanisa na pia kila mshirika.
  1. Kristo anazo nguvu za Mungu.
  • Kristo anaye Roho wa Mungu hivyo kanisa linahitaji kutumika katika nguvu za Roho Mtakatifu, lakini si kwa nguvu za mwanadamu, ujuzi, uongozi na mpango wa mwanadamu, lakini ya Roho Mtakatifu.
  • Kanisa linapotembea katika nguvu za mwili halitasimama, lakini tunapotembea katika Roho Mtakatifu kuna ushindi.
  • Tunapotembea katika Roho Mtakatifu kutakuwa na utukufu, nguvu na uzima. Mauti na kushindwa kutakuwa mbali.
  1. Kristo anashikilia wahubiri.
  • Kila mtumishi mkweli wa Mungu anashikiliwa na uwezo wa Mungu.
  • Kristo anashikilia mchungaji (Pastor) na pia kila mshirika.
  • Ikiwa mchungaji hatajisalimisha kwa Mungu washirika hawawezi kubarikiwa.
  1. Kristo anashika ufahamu wa Mungu-“Ninayajua matendo yako.”
  • Kristo anawaeleza wakristo wa pale Sardi kuwa anayajua yote. Ushindi wao na kuanguka kwao, nia na mawazo yao, agenda na mipango yao.
  • Kristo anafahamu kile tunachoendelesha hapa FBC-AR.
  • Kristo anafahamu sana pale tumefaulu na pale tulioanguka. 2 Mambo ya Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia kimbia duniani kwote ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake.”
  • Je, Mungu anajua yapi juu yetu kama FBC-AR?
  1. Sifa za kanisa la Sardi.
  • Kila mtu aliyelijua kanisa la Sardi alijua Sardi ni kanisa hai.
  • Wote walijua Sardi ni kanisa lenye moto wa Roho Mtakatifu na kanisa la sifa na jukumu.
  • Wote walijua Sardi ni kanisa la vitendo na injili.
  1. Ukweli wa mambo ya kaisa -Sardi
  • Haijalishi watu waliona nini, Yesu alijua ukweli wa mambo.
  • Yesu aliwaambia wa Sardi hata ingawa wote wanafikiria wao ni wazuri, lakini wamekufa kama kanisa.
  • Kama jinsi ilivyo mauti, Sardi hawakuwa na nguvu-walikuwa wamekufa!!
  • Hata ingawa walikuwa na juhudi, juhudi zao zilikuwa katika mwili.
  • Walihubiri lakini kazi yao haikuwa na matunda ya milele. Wenye dhambi hawakuokoka na maisha ya wengi wao haikubadilika.
  • Ni jambo mbaya, watu wote waone kwamba wewe ni Mkristo wa Roho, lakini Kristo anaona mauti kwako.
  • Unahubiri vizuri, unaomba vizuri, unakesha vizuri, unaongoza vizuri lakini wewe ni mauti.
  1. DAWA YA KWELI, KUPONYA KANISA LA SARDI (Ufu. 3:2-3).
  • Kanisa la Sardi lilikuwa na shida kubwa lakini kuna tumaini ya uponyaji wao!
  • Tabibu mkuu na wa karibu alikuwa na habari njema kwao na kwetu pia.
  • Sardi, wanaweza kupona lakini lazima kupokea dawa ya Mwokozi.
  • Kama Sardi, walikataa dawa ya Tabibu, basi yeye atalizima kanisa la Sardi milele.
  1. Kwanza wanaambiwa wakeshe.
  • “Kukesha” ni kufukuza usingizi wao.
  • Kanisa hili la Sardi lilikuwa na utukufu na sifa pale mbele lakini waliacha kufaulu kwao kwa kwanza kuwaletea usingizi.
  • Yesu Kristo anawahimiza kukesha na kufahamu ushindi wa jana hautasaidia leo na kesho.
  • Kanisa lilianza na maono (vision) na kuanzilishwa na mtu (man).
  • Kisha hayo maono yakawa mvumo wa wengi yaani
  • Kisha walioanza na kuongoza wanakufa.
  • Kisha ile movement inakuwa sanamu-
  • Kasha ile sanamu inakuwa ukumbusho-
  • Hivyo man to movement to monument to memorial.
  1. Pili-Wanaambiwa wafanye kazi.
  • “Ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa.
  • Kuyaimarisha mambo, Kristo anawaambia kufanya mambo manne.
  1. Fufua-Imarisha (Revive). Kuna mambo ambayo tayari yalikuwa yamekufa na mengine karibu kufa.
  • Kazi yao haikupendeza na kukamilika mbele ya Mungu.
  • Je, ni yapi tulikuwa tunafanya lakini yakafa, mengine yamezorota kwa Korona!
  1. Kumbuka-jinsi ulivyopokea
  • Kumbuka jinsi ulivyookoka, ukampenda Kristo kwa kweli, ukajazwa Roho Mtakatifu, ukatambea na Kristo bila dhambi.
  • Kumbuka ya kale ya kanisa la FBC-AR, kumbuka ya kale ya maisha yako.
  1. Amua-Kwamba utayaimarisha yale yako karibu kufa. Maombi, Biblia, ushuhuda, injili, kesha.
  • Imarisha mambo yote, si moja tu.
  1. Tubu dhambi.
  • Dhambi zimezidi sana katika wateule.
  • Dhambi inatutenganisha na Mungu na nguvu zake-Isaya 59:2.
  • Tukatubu udhaifu, uzembe, uovu na kifo.
  1. Tatu-Anawaambia wangoje. Wawe katika hali ya kumngoja Bwana.
  • FARAJA NA DHAWABU KWA KANISA WAKITUBU (Ufu. 3:4-6)
  1. Ahadi kwa mabaki (V. 4)
  • Wale waliomuishia Kristo na kutembea naye anawaambia waendelee. Yeye atawapa dhawabu yao.
  • Dhawabu yao ni kwamba, wataishi naye mbinguni milele, kwa sababu wameokoka.
  • Wewe ambaye ni mabaki (Remnant) zidi kumpenda na kumtumikia Kristo katika utakatifu.
  1. Ahadi kwa watakao tubu (V. 5)
  • Ahadi kwa watakao tubu ni kwamba Kristo ni kuwavika mavazi meupe, hatafuta majina yao kutoka kwa kitabu cha uzima.
  • Nitawakiri majina yao mbele ya Baba yangu na malaika wake. Mathayo 10:32 “Basi, kila mtu atakaye nikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”
  • Rafiki yangu huenda wewe ni mmoja wa wale wameacha moto wa Roho Mtakatifu kuzimika ndani ya maisha yao. Ikiwa ni hivyo, unahitaji kutubu. Mrudie Bwana naye atakurudia.
  • Mkiri Yesu Kristo mbele ya watu naye atakukiri mbele za malaika mbinguni.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *