Swahili Service

ASEMAYO MUNGU JUU YA KESHO

MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO

SOMO: 1 WATHESALONIKE 4:16-17; UFUNUO 7:9-10

 

 

Mungu ametujulisha juu ya kesho, pia ametuonya kuwa tayari atakaporudi.

Ni kwa nini kuhubiri juu ya siku za baadaye ?

  1. Kwa sababu Yesu Kristo mwenyewe alihubiri sana juu ya siku za baadaye.
  • Asili 20% za maneno ya Yesu Kristo zilikua juu ya kurudi kwake
  • Kristo alifundisha saana juu ya kuja kwake mara ya pili, hivyo sisi nasi tunahitaji.
  1. Kwa sababu Mungu yuko na mpango juu ya kesho-(Yeremia 29:11 )
  2. Kwa sababu tunapata tumaini juu ya kesho, dhidi ya wakati huu wa kukata tamaa na kuvunjika moyo.
  • Kurudi kwa Yesu Kristo ndio faraja yetu (l Wathesalonike 4:18) na pia ndio tumaini letu (Tito 2:13).
  1. Kwa sababu ni changamoto ya kukaa tayari kuishi maisha takatifu na kuweka bidii kuhubiri injili duniani kote kote (Mathayo 24:44,14;Luka 12:20 )

Leo tunatazama mpango wa Mungu juu ya  kesho na jambo la kwanza ni unyakuzi/kunyakuliwa kwa watakatifu na ufufuo wa watakatifu wafu pia tujifunze juu ya masharti ya kunyakuliwa:- Hebu tuone,

MPANGO WA MUNGU NA UNYAKUO

SIKU ZA MWISHO WA DUNIA NA MPANGO WA MUNGU.

  1. Jambo la kwanza ni kunyakuliwa kwa kanisa (Rapture).
  • Kunyakuliwa ni kutolewa kwa watu wa Mungu kutoka dunia hii.
  • Itabidi kanisa kunyakuliwa kwa sababu ya dhiki kuu inayokuja duniani (7 years Tribulation)
  • Dhiki kuu itakua siku za hukumu ya Mungu juu ya wote waliokataa Yesu Kristo.
  • Watu wa Mungu hawawezi kuingia katika hukumu (Warumi 8:1-2).
  • Dhiki kuu inapoendelea hapa duniani watu wote wa Mungu watakua hewani (mbinguni) huku, wakihukumiwa kazi zao mbele ya kiti cha enzi cha Kristo (BEMA)-(2 Wakorintho 5:10)
  1. Jambo la pili: ni kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili duniani (2 Advent). Hii ni kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili duniani pamoja na kanisa. Yesu Kristo mwenyewe atarudi duniani, kumshinda mpinga Kristo, kuharibu dhambi na uovu na kuleta ufalme wake duniani.
  • Kutawala dunia yote kutoka mji wa Yerusalemu kwa miaka 1000 (millennium)
  • Utawala wa Yesu Kristo (1000 years) hapa duniani ni kutimiza ahadi ya Mungu kwa lsraeli juu ya Masihi wao.
  1. Jambo la tatu: ni baada ya Miaka 1000 wafu waliokufa bila Yesu Kristo watafufuliwa pamoja na wote waliomkataa Yesu Kristo watahukumiwa.
  • Shetani, mapepo, wenye dhambi wote, mauti mpinga Kristo na nabii wa uongo wote watahukumiwa na kuingia katika ziwa la moto – milele na milele, (kiti kikubwa cheupe).
  • Baada ya hayo yote Mungu ataharibu kwa moto dunia hii ya leo na mbingu, na kuumba mbingu mpya na nchi mpya na Yerusalemu mpya.
  • Hivyo tutakaa na Yesu Kristo milele na milele.

JE NI NINI KUNYAKULIWA?-(RAPTURE)

  • Kunyakuliwa ni kurudi kwa Yesu Kristo ghafla hewani, kunyakua kanisa lake mbele ya siku hatari ya dhiki kuu.
  • Kanisa litakapo nyakuliwa, na pia wafu wote waliokufa katika Kristo, kwa miaka saba mambo mawili yatafanyika hewani (miaka 7).
  • Kazi zetu zitahukumiwa (ll Wakorintho 5:10)
  • Harusi ya mwana kondoo itafanyika.

 

PICHA YA DUNIA JUU YA KUNYAKULIWA- l Wathesalonike 4:16-17).

PICHA YA MBINGUNI JUU YA KUNYAKULIWA-(Ufunuo 7:9-10)

  • Hivyo kunyakuliwa kwa kanisa kutaleta mambo mawili, 1. Hukumu mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo (BEMA) -2. Matendo yetu yatahukumiwa na wengine watapata dhawabu zao na wengine Hasara ( l Wakorintho 3:10-14).

UKWELI JUU YA KUNYAKULIWA .

  • Kutokunyakuliwa maanake ni mtu huyo bado hajaokolewa.
  • Kunyakuliwa ni kutenganishwa na dhambi na Hali na mazingira ya dhambi-(Mathayo 24:40-42)
  • Tunahitaji  kujiweka tayari Kila saa maana hatujui siku wala saa ajapo Kristo.
  • Kanisa linaponyakuliwa, mara moja mpinga Kristo (Antichrist, mtu wa dhambi:- man of sin) atachukua mamlaka duniani.
  • Mpinga Kristo atatoka bara ya Europe hau ufalme wa Roma ya zamani (EU)
  • Mpinga Kristo atatawala kwa nguvu nyingi zaidi.
  • Mpinga Kristo tayari yuko na nambari ya Kila mtu duniani (Huduma Namba)
  • Dhiki kuu ni gadhabu ya Mungu duniani karibu watu wote wa dunia watakufa mauti-(Ufunuo 8-11).

JE, UMETIMIZA MASHARTI YA KUNYAKULIWA?

Kuna masharti ya kunyakuliwa.

Ni lazima umezaliwa mara ya pili.

  • Kuwa mshirika, kubatizwa, meza ya Bwana na fungu la kumi ni masharti ya kunyakuliwa.
  • Yesu Kristo alitufundisha kwamba cha muhimu zaidi ni kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:3-5) l Wakorintho 5:17, Warumi 8:9).       

Lazima kuungama dhambi zote-(lsaya 59:2), Ezekieli 18:24, Zaburi 66:18.

Kesha, omba, tii, kaa katika Roho Mtakatifu, (Luka 21:36) Mathayo 7:21).

Tubu dhambi ya kiburi. Ishi katika msamaha (Yakobo 4:6, l Petro 5:5, Ezekieli 28:17.

MWISHO

  • Je, umeokoka?
  • Je, unatembea na  Kristo  katika Roho Mtakatifu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *