Swahili Service

BARAKA KUPITIA WASAIDIZI HATIMA

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: 2 WAFALME 5:1-8

 

Mungu amepanga kila mmoja kupata baraka kupitia kwa wasaidizi wa hatima. Naamani alisaidiwa na kijana mwanamke asiyetoka nchi ya Israeli. Huyu kijana mwanamke alikuwa mtumwa.

  • Mungu pekee anawainua watu kupitia watu wengine. Mungu anawabariki watu kupitia watu.
  • Usaidizi wa Mungu unapitia watu wanaoinuliwa na Mungu kukusaidia. Hawa watu wanaoinuliwa na Mungu kukusaidia wanaitwa wasaidizi hatima (destiny helpers).
  • Uwezo wako kugundua, kupokea, kudhamini, kuhifadhi na kusheherekea watu waliotumwa kwako kukusaidia ni jambo la busara kwako mwenyewe.
  • Watu wengi wanatekeleza katika maisha si kwa sababu ya kukosa elimu na maarifa, lakini wanakaa mbali na wasaidizi hatima waliotumwa kwao na Mungu.
  • Safari ya kufikia hatima yetu katika Bwana itakuwa rahisi kupitia ushauri, urafiki, ushirika na ufahamu wasaidizi wanaotumwa na Mungu kwako, katika kila hatua ya safari yako duniani.
  • Mungu hakupangia Naamani kufa kama mwenye ukoma-lakini usaidizi wake utapitia kwa kijana mwanamke-mtumwa katika nyumba yake.
  • Msaidizi hatima si lazima awe tayari, mtu mkuu, msomi, mwenye kujulikana, mashuhuri, lakini awe chombo kilichopangwa na Mungu kutimiza jambo kuu katika hatima na maisha yako. Hebu tuone:-

HAINA ZA WASAIDIZI HATIMA (Kinds of destiny helpers).

  • Ni lazima utambue haina mbali mbali ya wasaidizi hatima na kujiweka katika hali na mahali pa kuwapokea ndiposa uyapokee yote kutoka kwao.
  1. Mwenye kushikanisha (the connectors).
  • Hawa ni watu wanao uwezo wa kukuunganisha na watu walio na uwezo na kuchangia maisha na hatima yako.
  • Huyu kijana mwanamke mtumwa katika nyumba ya Naamani alikuwa connector katika Naamani na Elisha.
  • Kuna uhusianao madhubuti katika tabia yako na nafasi utakayo pata katika maisha yako.
  • Tabia zako na nafasi (opportunity) zako zinaenda pamoja.
  1. Walimu na washauri (role models and mentors).
  • Hawa ni watu walio na uwezo na ujuzi na uzoefu wa kufahamu unachohitaji kufikia hatima yako katika Mungu.
  • Uaminifu wako, unyenyekevu wako katika uhusiani wenu utachangia sana kwa kile utapata kutimiza hatima yako.
  • Kwa mfano, Musa na Yoshua, Elisha na Eliya, Timotheo na Paulo, Yoshua na Kalebu.
  1. Wadhamini (the sponsors) wafadhili.
  • Hawa ni watu ambao Mungu amewatuma kukulipia kutimiza ndoto zako zote hau sehemu.
  • Hawa wanaweza kulipa gharama za maisha yako, miradi yako.
  • Yesu Kristo alikuwa na wafadhili, wanawake wakuu kama jinsi Susana, Mariamu, Yusufu wa Arimathea, Nikodemu.
  1. Mwenye kupendekeza, mashabiki (the recommenders).
  • Hawa ni watu watakao pendekeza kwa wale wasiokufahamu hau mahali sauti yako haiwezi kusikizwa.
  • Yusufu alipendekezwa kwa farao, Daudi alipendekezwa kwa mfalme Sauli.
  • Onesimo alipendekezwa kwa Filemoni na mtume Paulo-Filemoni 1:8-20.
  • Kuna watu hawataweza kukufahamu bila kushabikiwa.
  • Kujua watu wanaoweza kukushabikia ni jambo bora sana.
  1. Waombezi (the intercessor)
  • Hawa ni watu wanaokuombea kwa moyo safi na upendo.
  • Hawa wanakuombea ili mipango ya Mungu juu ya maisha yako ikatimie.
  • Yesu Kristo alimwombea Petro.
  1. Wakuu wa kiroho, maaskofu (the overseers).
  • Hawa ni watu wanaojipa jukumu juu ya maisha yako kwa wema.
  • Hawa wakuu wanakuombea, wanatoa unabii juu ya maisha yako na ndani ya maisha yako.
  • Hawa wanakushauri, wanakutia moyo kwa neno la Bwana.
  • Hawa wanauwezo wa kukukemea na kukuonyesha njia za Mungu.
  1. Washikadao (partners).
  • Hawa wanafanya kazi ya maisha pamoja nawe.
  • Mke au mume wako ni mshiriki pamoja nawe katika safari ya maisha.
  • Kuchagua mume au mke ni jambo na uamuzi wa hatima.
  • Ndoa inabadilisha maisha ya mtu daima!!
  • Pia washiriki katika biashara, huduma.
  • Unapopanga maisha yako usiwausishe watu wasiofaa, watakusumbua katika maisha na hatima yako.
  • Mfano ni Paulo na Sila na Barnabasi katika huduma, Prisilana Akila katika ndoa na biashara.
  1. Wanaokuhudhi (the persecutors).
  • Hawa ni watu wanaokusudia kukufanya mabaya, hawa hawakutakii mema.
  • Lakini hawajui kwamba Mungu atatumia chuki na wivu yao kukubariki.
  • Yusufu na ndugu zake, Hannah na Peninah, Mordecai na Haamani.

SABABU ZA KUOMBEA WASAIDIZI WA HATIMA.

Kila mtu anahitaji kusaidiwa kwenda haraka na mbali katika safari ya maisha.

  • Shetani anaweza zuia wasadizi wako kwa kuwafanya adui au wasionekane.
  • Shetani alileta dhoruba katika bahari ya Galilaya ili mtu mwenye pepo (legion) asikombolewe-Marko 5:1-10.
  • Shetani anaweza kukufanya kudhihaki wasaidizi wako.
  • Naamani alikuwa karibu kukosa uponyaji wake kwa sababu nabii Elisha alikosa kumwona na kumlaki-2 Wafalme 5:11-14.
  • Wakati mwingine wasaidizi wako wanaweza kuwakilishwa na shetani.
  • Tabia ya Mordekai na heshima zake ziliaribiwa na Naamani mbele ya mfalme.
  • Tena wasaidizi wako wanaweza kutumiwa na shetani wasikusaidie.
  • Tambua, kwa watu Mungu ameweka katika maisha yako na katika kila musimu wa maisha kukusaidia ikafikie hatima yako katika Bwana.
  • Omba sana wasaidizi wako wakakufikie.

MWISHO

  • Ombea wasaidizi wako wakafunuliwe kwako.
  • Omba wasaidizi wako wakakufikie.
  • Omba Mungu akufunulie wewe ni msaidizi wa nani.
  • Omba, ukatimize hatima yako katika Bwana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *