Swahili Service

MAAJABU YA MTOTO YESU KRISTO

SOMO: 1ST TIMOTHEO 3:16

 

Mtoto Yesu Kristo alikuwa mchanga lakini mzee, alikuwa maskini sana, lakini tajiri sana. Alikuwa dhaifu sana na kumbe mwenye nguvu zote. Alikuwa kimya na kumbe alinena yote. Alikuwa wa ulimwengu na kumbe mjumbe wa mbinguni.

“Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.

Mungu alidhihirisha katika mwili.

Akajulikana kuwa na haki katika roho.

Akaonekana na malaika.

Akahubiriwa katika mataifa.

Akaaminiwa katika ulimwengu.

Akachukuliwa juu katika utukufu”- 1st Tim.3:16.

  1. Paulo alieleza kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kutumia neno (AJABU) au siri kubwa kwa maana alizaliwa na bikira. Mungu akawa mtu. Hebu tuone maajabu tano juu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

MCHANGA SANA- KUMBE MZEE WA SIKU

  1. Mwana wa milele alizaliwa kutoka milele na kuingia katika wakati.
  • Malaika walipoimba mbele ya wachunga kondoo mle Bethlehemu, mtoto Yesu Kristo alizaliwa.
  • Yesu alikuwa mtoto wa masaa machache lakini katika mwili.
  • Mika 5:2- “Basi wewe, Bethlehemu Efrathi, uliye mdogo miongoni mwa elfu za Yuda, kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakaye kuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”
  • Yesu Kristo hakufanyika Mwana wa Mungu mle Bethlehemu- lakini milele na hata milele Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu- Zaburi 2:7, 12; Mithali 30:4; Waebrania 1:2; Yohana 3:17.
  • Hatungeweza kuwa na “Baba wa milele”- Isaya 9:6- bila kuwa na “Mwana wa milele.”
  • Mwana wa Mungu ni wa milele na milele. Hana Mwanzo, Hana mwisho- Waebrania 7:3.
  1. Yesu Kristo alikuwa Mungu kamilifu.

Wakolosai 2:9-“Maana katika Yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu jinsi ya kimwili.”

  • Yesu Kristo ni Yeye aliye “Neno la milele” maana hapo Mwanzo palikuwa na Neno, naye Neno alikuwa na Mungu naye Neno alikuwa Mungu- Yohana 1:1; 4.
  • Yesu Kristo ni Muumba- Yohana 1:3.
  • Yesu Kristo alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili.
  1. MASKINI SANA- BALI TAJIRI ZAIDI.
  2. Umaskini wa Kristo.
  • Kama tungechagua wazazi wa Kristo, tungetafuta matajiri, wasomi, waheshimiwa kisiasa na pengine Wafalme. Hivyo mamajusi walimtafuta mtoto Kristo kwa mfalme Herode.
  • Tungependa sana Kristo azaliwe katika hospitali safi, madaktari wa juu zaidi, lakini Kristo alizaliwa katika hori ya ng’ombe.
  • Alizaliwa kwa nyumba ya maskini sana.
  • Kristo aliacha sifa zake zote mbinguni.
  • Kristo aliacha sifa zake zote, hakuwa na nyumba.
  1. Alitufanya kuwa tajiri- 2nd Wakorintho 8:9.
  • Tulipata kuwa matajiri kwa umaskini wake.

KRISTO ALIKUWA DHAIFU- BALI NGUVU ZOTE NI ZAKE MILELE.

  1. Kristo ni Mungu aliyekuwa dhaifu.
  • Hakuna mtu dhaifu kama mtoto wa mwanadamu. Hawezi kujikinga, kuongea na kujilisha.
  • Inachukua miaka miwili mtoto wa mwanadamu kujisaidia.
  • Aliyeumba vyote alijisalimisha mpaka mauti (Kenosis)- Wafilipi 2:6-7.
  • Alikuwa Mungu aliyekuwa tayari kupata majeraha.
  • Kristo katika udhaifu wake alikuwa mwenye nguvu.

KATIKA KIMYA CHAKE KRISTO ALINENA YOTE.

  1. Katika kimya chake katika hori ya kulia ng’ombe, Kristo aliyeumba vyote alikuwa kimya.
  2. Alikuwa neno la uzima.

ALIKUWA KIUMBE DUNIANI, BALI MUNGU WA MBINGUNI.

  1. Kristo ni chanzo cha maisha na uzima wote.
  2. Kristo ni chanzo cha uzima mbinguni- 1st Wakorintho 15:47; Yohana 3:13.

 

MWISHO

  • Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
  • Maanake Krismasi ni amani duniani.
  • Je, Kristo ni Mwokozi wako leo?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *