Uncategorized

THIATIRA-KANISA LA YEZEBELI.

MAKANISA SABA YA UFUNUO

UFUNUO 2:18-29

Kanisa la Thiatira lilikuwa moja ya makanisa saba ya ufunuo. Bwana Yesu Kristo anawapongeza wakristo wa Thiatira kwa kazi yao njema na matendo ya imani. Thiatira walikuwa na upendo, huduma na subira. Matendo yao ya kwanza yalikuwa bora zaidi, yalizidi yale ya kwanza. Kwa kutazama kutoka nje, kanisa la Thiatira lilikuwa kanisa la kupendeza sana, upendo, imani, huduma na subira. Thiatira walishika sana mambo hayo manne na kuzidi sana kila mwaka!!

Lakini pamoja na upendo, imani, huduma na subira yao, kanisa la Thiatira lilikuwa na shida moja kubwa. ‘Lakini nina neno juu yako ya kwamba wamridhia (tolerate) yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu” (2:20). Kanisa la Thiatira lilivumilia na kumridhia “mwanamke” aitwaye Yezabeli. Yaani roho ya Yezebeli ilitawala kanisa la Thiatira.

Kazi ya Yezebeli ilikuwa kufundisha na kutongoza watumishi wa Mungu na kuwapoteza ili wazini na kula chakula kilichotolewa kwa sadaka kwa mapepo. Mungu wa mbinguni tayari alikuwa amemhukumu pamoja na wafuasi wake.

Mungu tayari alikuwa amempa Yezebeli wakati wa kutubu lakini Yezebeli alikataa kutubu dhambi zake na kugairi.

Lakini huyu Yezebeli alikuwa nani? Yezebeli alikuwa tayari amekufa na kufariki dunia katika kitabu cha Wafalme wa pili.

Lakini elewa hivi, Yezebeli mwenyewe alikufa lakini roho ya Yezebeli haikufa. Roho haikufi. Hivyo roho ya Yezebeli ilikuwa katika kanisa la Thiatira. Daimoni ya Yezebeli ilitawala mji wa Thiatira.

Sisi nasi twaishi nyakati mbaya sana. Wakati wetu ni hatari maana roho ya Yezebeli inatawala kizazi hiki chetu kila mahali na kanisani pia.

Yesu Kristo tayari alitupilia mbali upendo, imani, huduma na subira ya Thiatira kwa maana kanisa la Thiatira lilimrithia Yezebeli kanisani na katika umma. Roho ya Yezebeli ni roho moja inayotawala siku hizi za mwisho. Hebu tujifunze:-

  1. YEZEBELI NI NANI? (1 Wafalme 16:29-33).
  • Yezebeli alikuwa binti Ethbaali mfalme wa Sidoni mkanaani.
  • Mfalme Ethbaali pia alikuwa mfalme na pia kuhani mkuu wa Baali mungu wa wakanaani.
  • Baali alikuwa mungu anayehusika sana na uzinzi na uasherati wa kila haina.
  • Yezebeli alilelewa katika jamii na taifa ambayo njia ya kupanda cheo ilikuwa ni kupitia ngono na uasherati.
  • Baadaye Yezebeli alikuwa malkia, mke wa Mfalme Ahabu mle Israeli.
  • Yezebeli alizaliwa katika ufalme na akaolewa katika ufalme mwingine.
  • Hivyo Yezebeli alielewa sana mambo ya ufalme, maisha, vitendo na siasa za kifalme.
  • Mfalme wa Israeli Ahabu alitawaliwa na kukaliwa na Yezebeli.

Baadaye Yezebeli alileta dini ya wakanaani yaani Astheroth (maashela). Alikuwa mungu wa mwezi na kutawala mambo ya mapenzi na ngono. Alikuwa mungu wa kike (goddess of love and sensuality).

Makahaba, Malaya na makuhani wa kike walijaa hekalu za Baali, hivyo wanaume wa Israeli hawangejizuia majaribu ya hawa wanawake wa baali.

  • Waisraeli milioni kumi (10 million) walichagua Baali. Kiasi ni watu elfu saba pekee (7,000) waliendelea kumwabudu Yehova.
  • Yezebeli alikufa kitambo, lakini roho ya Yezebeli inatawala nafsi nyingi, jamii, makanisa na mataifa mengi hivi leo.
  • Roho ya Yezebeli ni roho ya mwisho wa dunia. Roho ya Yezebeli inaongoza Agenda ya Shetani.
  • Roho ya Yezebeli ni roho ya kike, inapenda kuongoza, kutawala na kukalia (“take-charge”).
  • Yesu Kristo anachukia roho ya Yezebeli kanisani, jamii na taifa.

 

  1. JINSI YA KUTAMBUA ROHO YA YEZEBELI.
  2. Roho ya Yezebeli n roho ya mtego (manipulation).
  • 2 Timotheo 2:26 “Wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.”
  • Roho ya Yezebeli anawashika wanaume na wanawake pia (Jezebel is gender neutral).
  • Ahabu pengine angekuwa mfalme mwema kama si Yezebeli.
  • Mama yako akiwa na roho ya Yezebeli atakuongoza toka mbali na kukubebea akili zako.
  • Mwanamke ‘Yezebeli’ ni ‘unayeishi naye’ co-habitation. Yaani kuambatana naye nafsi zikishindana.
  • Roho ya Yezebeli haiwezi kubali makosa..
  • Mtu akiwa na roho ya Yezebeli hawezi kubali makosa yake. Roho ya Yezebeli haiwezi kuchukua jukumu maana ni roho ya unafiki na kiburi.
  • Roho ya Yezebeli ikishika mke hau mume, basi hakuna njia ya kutoka maana Yezebeli hawezi kutubu dhambi zake hata kufa.
  1. Roho ya Yezebeli ni roho ya kupoteza watu alaiki (Ufunuo 2:20)-(misleading spirit).
  • Watu wanamfuata Yezebeli bila kufikiri.
  • Yezebeli alipopitia hapa F.B.C A/River watu walimfuata bila kufikiri mpaka leo.
  • Roho ya Yezebeli ni roho inayowatumia watu kutimiza Agenda ya Shetani.
  • Roho ya Yezebeli inatumia hisia ya watu na kuwafanya watu kukasirika bure na kuchukia.
  • Roho ya Yezebeli ni roho ya mpinga-Kristo.
  • Roho ya Yezebeli inawatumia watu kama watumwa, watu wanapagawa na Shetani.
  • Roho ya Yezebeli ni roho ya kuwatumia watu kutekeleza Agenda za Shetani.
  • Roho ya Yezebeli ni roho ya kuichawi na kiuganga.
  • Roho ya Yezebeli ni roho inayoishi katika uasi na uchafu (1 Wafalme 19:1-2).
  • Yezebeli alituma barua kwa Eliya na kumtisha kwamba kwa masaa 24 atakuwa maiti!!
  1. Roho ya Yezebeli ni roho ya kuzini na tamaa (spirit of lust)-2 Samweli 11:4
  • Mfalme Daudi alipopatikana na roho ya tamaa mbaya alisema “Basi, Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa, naye akaingia kwake, naye akalala naye……………”
  • Mpango wa Yezebeli si mtu Yule pekee, lakini lengo ni kuangusha jamii nzima hau taifa lote.
  • Taifa lote la Israeli lililipa gharama za dhambi ya Mfalme Daudi.
  • Wengine wetu tunamwalika Shetani nyumbani kwetu na nafsi zetu na kujiletea madhara makuu-(1 Wathesolonike 4:3)
  • Ni lazima kutimua dhambi kutoka kwa maisha yetu (Mithali 22:10; 1 Wakorintho 5:7).
  1. Roho ya Yezebeli ni roho ya kutisha mtu (1 Wafalme 19:3)-‘A tormenting spirit’
  • Roho ya Yezebeli itapenda mtu akimbie kutoka huduma, mwito, jukumu, hatima, maono, jamii, ndoa na kanisa.
  • Eliya alikimbia Yezebeli akataka kujinyonga na kufa.
  1. Roho ya Yezebeli ni roho ya kudharau (Mocking spirit.)
  • Mfalme Daudi alikimbia kwenda kwa adui zake (1 Samweli 27:1)
  • Roho ya kudharau watumishi wa Mungu (2 Wafalme 9:32)

MWISHO

  • Je, Roho ya Yezebeli imekupata?
  • Njia ya kushinda Yezebeli ni kujitenga naye.
  • Yezebeli anafahamu kwamba Yehu anakuja kumuua.
  • Je, umeokoka, okoka sasa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “THIATIRA-KANISA LA YEZEBELI.”

  1. Nimepata maarifa mengi , Mungu akubariki) Lakini pia naomba unitumie historia ya kanisa la similina

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *