Sermons Swahili Service

USIKU MFALME HAKULALA

Pst Julius Kilonzi

Esther 6:1-14, 7:4,10

Katika kitabu cha Esta jina la Mungu halijatajwa. Lakini tunamuona Mungu kila mahali. Tunaona uwezo wake, miujiza yake na rehema zake katika kisa hiki. Ndivyo ilivyo pia katika maisha yetu, kuna nyakati hatuoni Mungu katika hali zetu; hata hatusikii sauti yake; kunakuwa na kimya kingi, ni kama Mungu ametuacha – lakini Mungu yupo. Wakati Mungu anakosa kuonekana kumbuka kwamba bado yupo na anajishungulisha sana na maisha yako. Hata leo katika hali yako Mungu yupo na anahusika kabisa. Anatengeneza njia kwa ajili yako na yangu. Katika kisa hiki watu wanne wametajwa;

A). Mfalme Ahasuero
Hajui watu wanaoenda kuuliwa.
Hajui mke wake anavyohusiana nao
Hajui Ususiano wa Mordekai na Esta
Hajui mpango wa siri wa Hamani
B). Mordekai,
Hakupandisha cheo kama Hamani, lakini hakujali
Alijua kulinda moyo wake
Alifahamu Mungu sio mdhalimu (Waebra 6:10)
Mungu sio kama mwanadamu – kusahau kazi zetu
C). Hamani
Alijipenda mwenyewe – ubinafsi
Alichukia Mordekai na wayahudi (wana wa Mungu)
Aliwapangia mabaya Wayahudi na Mordekai kuwateketeza (annihilation).
D). Mungu
Lakini yuko wapi Mungu? Mbona mambo yaharibike hivi?
Mungu yupo – kabisa.
Anafanya kazi katika siri, Yuko kimya akitenda kazi
Anasababisha matukio na hali zote
Ndivyo mambo hutendeka baada ya maombi (wamefunga siku tatu)
Ni kama yameharibika… (xxx lakini Mungu)
Lisaa la kumi na moja Mungu….
Anaifanya kuchanganyikiwa adui zetu
Hebu tuone;

I. MUNGU ANADHIBITI MATUKIO YOTE
Mfalme alikosa usingizi – Mungu alimkosesha usingizi.
Susa yote walilala isipokuwa mfalme wao (insomnia)
Anakumbusha mfalme kuhusu Mordekai na kazi nzuri (Waebra 6:10)
Hamani amefika mapema na mpango wa kumaliza Mordekai. Mfalme anamwita na kumwongelesha kwanza.
Mordekai anakuwa na nafasi ya kwanza (suddenly) kwa ratiba za mfalme.
Mfano wa biblia: Yusufu, Musa na binti Farao, Yona na samaki, Yesu kuzaliwa, …..

II. MUNGU HUDHIBITI MATUKIO ILI KUWAOKOA WANAOMPENDA (HATUTAANGAMIA!!)
Kwanini mfalme asilale? – Lazima akumbushwe
Lazima Mordekai atunzwe (atendewe mema)
Lazima mpango mbaya wa Hamani ufike kikomo
Tanzama wakati wa Mungu (God’s timing – exact)
Hamani anapendekeza jinsi ya kufanyiwa (hakujua)
Hamani ni mwenye kupenda kusifiwa
“Fanyia Mordekai yote uliyopendekeza”.!!!
Hamani gafla anafedheheshwa…. Lazima atamsifu adui yake Mordekai (6:11)
Kwa siku nzima Hamani anamsifu adui yake – kinyume!!
Uovu hautashinda kamwe kwa watu wa Mungu
Mipango mibaya ya adui za watu wa Mungu yaonekana kufaulu – lakini gafla itashindwa.
Twajua kuwa sisi hatuna nguvu nyingi. Twategemea neno “lakini Mungu”
Usiongope jinsi mambo yanavyo-onekana Mungu anatenda kazi kwa siri.
Pengine Hauna kazi; huna mtoto, haujanjenga, hauna ploti, haujaolewa, wamesema utakufa masikini, pengine wewe ni mgonjwa, wamekulaani, wamengojea kuanguka kwako …. Lakini Mungu anaenda kukuokoa (but God) Mwanzo 50:20.

III. KUNA WAKATI WA KULIPWA MEMA NA MABAYA PIA.
Kwanini Mordekai hakulipwa kabla ya wakati huu? Kwanini alisahauliwa?
Lazima uovu uonekane kama unashinda
Usiongope kwamba umengojea sana .. Mungu anampango mwema
Hivi ndivyo zilivyo njia za Mungu (Tanzama: Daudi, Mauti na Kufufuka kwa Yesu)
Ngojea kwa subira Mungu hachelewi.

IV. MAGURUDUMU YA MUNGU YANAPOZUNGUKA WALIO JUU WATAKUWA CHINI.
Hamani alikuwa mwenye kiburi lakini akafedheheshwa
Alikuwa tayari ameutayarisha mti wa kumtundika Mordekai (5:14) lakini akatundikwa huko yeye (7:10)
Unabii wa mke wake Zereshi …. “Utaanguka mbele ya Mordekai Myahudi”.(6:13)
Adui zako pia wataanguka mbele yako Mkristo unayeomba na kutenda haki.
Mordekai na Wayahudi walikuwa katika hatari ya kuteketezwa lakini wakapata vyeo na majumba ya watesi wao.

MWISHO
Je kuna Hamani kwa maisha yako? Mwamini Mungu kumshungulikia. Wewe omba…funga….tenda uaminifu.
Je, mambo yanaonekana kuzorota kabisa, usijali Mungu anatenda kazi katika siri
Mpe Mungu yote yanayokusumbua leo.

The following two tabs change content below.

Julius Kilonzi

Pastor Julius Kilonzi has served in the role of Administrative Pastor at First Baptist Church since joining the staff in 2010. Under Rev. Dr. Willy Mutiso and the Elders' Council, Julius’s primary role is to lead the FBC Staff team in the implementation of the church’s vision.

Latest posts by Julius Kilonzi (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *