Swahili Service

VITU VITATU VYA THAMANI

MFULILIZO:  YESU KRISTO NI THAMANI 

SOMO:   I PETRO 1:7-19     

Mtume Petro anataja vitu vitatu vya thamana katika nyaraka zake mbili. Hivi vitu vitatu vya thamani vinahitaji kuwa thamana kwetu pia.

Mwokozi wetu ni wa thamani, Imani yetu ni ya thamani na Neno la Mungu ni la thamani kwetu.

Thamani maana yake ni ghali, bei juu,kitu tukufu, kitu cha uzito, kitu cha maana sana.(valuable, costly, rare, prized, splendid, glorious, weighty and influential).

Hebu tuone jinsi tumepata vitu vya thamani  sana katika Kristo:

I.  YESU KRISTO NI THAMANI (1 PETRO 2:4-7)

  1. JIWE TEULE LA PEMBENI LENYE HESHIMA.
  2. Yesu Kristo ni jiwe la thamani, jiwe la pembeni, Jiwe la kwanza kuwekwa msingi, kuna jiwe moja tu la pemeni, Yesu Kristo wa thamani  .
  3. Katika mbingu yote, kulikuwa na Yesu Kristo mmoja tu.
  • Kondoo mmoja tu, anayeweza kuokoa wanadamu.
  • Hakukuwa na mwanadamu, hau malaika mbinguni kote wa kuokoa isipokuwa Kristo pekee.
  • Kristo ni wa pekee, hakuna mwingine, yeye ni nanga –yaani jiwe la pembeni.

       2. DAMU YA YESU NI YA THAMANI. (1 PETRO 1:18-19).

  1. Kabla ya wokovu tulikuwa watu bure, na watupu.
  2. Tulikombolewa kwa damu ya thamani (precious blood).
  3. Duniani na mbinguni yote hakukuwa na damu nyingine,

Damu ya Yesu pekee ilikuwa na uwezo wa kuokoa mwanadamu.

  1. Tone moja pekee ya damu ya Yesu Kristo ni thamani Zaidi kuliko mali yote ya dunia hii.
  • Damu ya Yesu Kristo yote ilimwangika hili mwanadamu awe safi, tayari kuingia mbinguni.
  • Damu isiyo na dhambi ilipata kuwa dhabihu ya kuokoa.
  • Yesu Kristo na damu yake ni thamani Zaidi

II.  IMANI YETU NI YA THAMANI (I PETRO 1:7)

  1. Imani yetu ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu
  2. Kitu cha pili thamani kulingana na Petro ni Imani yetu. (I Petro 1:7)
  3. Tunajua dhahabu ni thamani, dunia yote na mataifa yote utumia dhahabu kuthamini pesa zao.
  4. Dhahabu safi imesafishwa na moto, Imani yetu inapitia kwa moto ionekane kama ni safi.
  5. Imani yetu ni thamani kwa sababu ya haki ya Yesu Kristo (II Petro 1:1)
  6. Imani hii inayookoa haitokani na sisi
  7. Kuna Imani moja pekee inayookoa mwanadamu – imani dani ya Kristo.
  8. Tumepokea Imani ile ile iliyookoa Petro na wenzake
  9. Kuna Imani za kila haina duniani, lakini ni Imani moja pekee inayookoa, Imani dani ya Kristo. (2 Petro 1:, Mathayo 7:21-23)

III. AHADI ZA MUNGU NIZA THAMANI (II PETRO 1:4)

  1. Ahadi ya kuwa wana wa Mungu. (II Petro 1:4-11)
  • Ahadi ya kubandilishwa tuwe na tabia ya Mungu.
  • Sasa sisi si wangeni tena kwa agano za Mungu
  • Sasa sisi ni wana wa Mungu, warithi wa Mungu, warithi pamoja na Yesu Kristo.
  • Zamani tulikuwa wanadamu, lakini sasa tu wana wa Mungu (from son of Adam to son of God)
  • Ahadi hizi zinatutoa kutoka kwa dunia hii ya dhambi na kutukalisha na Mungu huko mbinguni.
  • Ndivyo ahadi hizi zinaitwa, “ahadi kubwa mno, za thamani” (II Petro 1:4)
  1. Katika ahadi hizi tumeahidiwa;
  2. Kufufuliwa na kupewa miili ya ufufuo.
  • Miili mpya, mwili kama wake Kristo (Wafilipi 2:1)
  1. Miili ya ufufuo haitaharibika, hakuna ugojwa, uzee, dhambi na kuaribika.
  2. Ahadi hizi nizakudumu (I Petro 1:4)
  • Ahadi za Mungu haziaribiki, hazina uchafu, kunyauka, zimetuzwa mbinguni.
  • Zaidi ya yote tumehaidiwa ufalme mwema mbinguni, mbingu mpya, dunia mpya na Jerusalemu mpya.
  • Hivyo tuko na Mwokozi wa thamani, Imani ya thamani na Ahadi za thamani.

MWISHO

  • Je, umempokea Yesu Kristo kama mwokozi wako?
  • Yesu Kristo ni wa thamani zaidi. Ameni.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *