Swahili Service

NYENYEKEA, UKATII

MFULILIZO:  YESU KRISTO NI  WA THAMANI SANA

SOMO:   I PETRO 2:13-14, I PETRO 3:1-7

Kunyenyekea ni nia na moyo wa kujisalimisha  kuweka watu wengine mbele, kutii amri kujisalimisha chini ya mamlaka ya mtu mwingine.

Siku moja muamerika na muafrika walienda kuvua samaki wote wawili walikuwa na chupa ya minyoo (yaani worms). Muamerika alipochukua minyoo alipata kuifunga chupa yake vikali sana, lakini muafrika hakuifunga chupa yake. Muamerika akamwambia muafrika je, kwanini haufungi chupa yako ya minyoo? Muafrika akasema, wajua kwamba minyoo yako ni ya kiamerika, lakini hawa wangu ni wa kiaafrika – minyoo moja hakiinuka wenzake watamvuruta chini. Sisi si watiivu na wanyenyekevu, tunamwasi aliyejuu yetu. Leo tunajifunza juu ya unyenyekevu na utii wa kibiblia. Je, tumnyenyekee nani katika Bwana?

I.  JE, TUMNYENYEKEE NANI?

  • Biblia inatufundisha wazi tumnyenyekee nani
  1. Mnyenyekee (mtii) Mungu (Yakobo 4:7)
  • “Basi mtiini Mungu, mpingeni shetani naye atawakimbia.”
  1. Wakuu wa kanisa (Waebrania 13:17)
  • Watiini wenye kuwaongoza na kuwanyenyekea”
  1. “Nyenyekeaneni nyinyi kwa ninyi” (Waefeso 5:12)

Wengi tunafahamu unyenyekevu na utii kwa hawa watatu, lakini hebu tuone wengine watatu wa kunyenyekea.

II.  NYENYEKEA SERIKALI (I PETRO 2:13-14)

  • Hata ingawa utaifa wetu ni mbinguni ni lazima pia kuitii serikali za dunia hii kwa ajili ya Bwana wetu Kristo.
  • Yesu Kristo alisema mengi juu ya kutii serikali.
  • Tunahitaji kuiti serikali, mipango yake (policies) tunaitaji kupinga kura, kulipa kodi na kuiombea serikali.
  • Petro aliandika waraka wake, wakati Roma ilikuwa chini ya kaisari Nero, aliyekuwa mkatili zaidi duniani (64AD)
  • Kaisari Nero aliwatesa wakristo na kuwaua hata mtume Petro alikufa chini yake, pia Paulo
  • Nero aliwatumia wakristo kwa kuwakisha moto hili wawe taa kwa barabara
  • Hata ingawa hivyo Petro anasema tukaitii mamlaka ya serikali iliyo wekwa juu yetu
  • Mtume Paulo alikuwa na wazo hiyo hiyo ya mtume Petro (Warumi 13:1-7)
  • Kuasi serikali kumependekezwa tu wakati serikali inapendekeza kutotii Mungu (Daniel 3:16-23) (Matendo ya mitume 4:13-22, Matendo 5:27-29)
  • Tunaitii serikali kwa njia ya kulipa kodi, kulipa forodha, kuwaeshimu viongozi, kutii amri zilizowekwa, kupiga kura na kuiombea.

III. WATUMISHI WAWATII WAAJIRI WAO (I PETRO 2:18-20)

  • Petro hapa haongei juu ya utumwa (slavery) lakini watumishi wa kulipwa mishahara.
  • Waroma hawakufanya kazi yeyote, mbali waliwatumia watumwa kama, dakitari, waalimu, waimbaji etc.
  • Watu walipookoka watumwa na bwana zao walikuja kanisani.
  • Bwana na mtumishi walipoingia kanisa, wote walikuwa sawa mbele ya Mungu.
  • Hivyo watumishi wakaacha kuwatii Bwana zao waajiri. Hivyo Petro anawaandika watumishi kuwatii Bwana zao.
  • Mungu anapenda sisi tuwatii waajiri wetu, wengine tuna waajiri wazuri, wengine waajiri mbaya (I Petro 2:19-20)
  • Katika mateso kazini Kristo alituachia mfano mwema wa utii (I Petro 2:21-25)
  • Kristo aliteseka sana, hata ingawa hakuwa na dhambi
  1. UNYENYEKEVU NA UTII KATIKA JAMII (I PETRO 3:1-2)
  • Mke kwa mme
  • Mme kwa mke
  • Watoto na wazazi
  • Mke na mme
  • Heshima kwa wakuu wetu
  • Mme na mke wanahitaji kujisalimisha wao kwa wao (I Petro 3:1-2, Waefeso 5:12)
  • Katika desturi za Roma, wanawake hawakuwa na haki zozote.
  • Wasichana walikuwa chini ya baba zao, walipoolewa walikuwa chini ya mume zao.
  • Walipookoka waume na wake zao walikuja kanisa mahali pa usawa na uhuru.
  • Wake walipookoka walipata uhuru wao, Yesu akawa Bwana wa kwanza, mme Bwana wa pili.
  • Hawa wanawake walianza kuwahubiria mume zao na kutotii, hivyo Petro anawashauri wanawake wakristo kunyenyekea mume wao.
  • Petro ambaye alikuwa na mke nyumbani anaeleza kwamba ndoa ni kunyenyekea kwa sababu mme na mke ni mwili mmoja.
  • Hivyo kwa upendo, wapendana wao kwa wao.
  • Heshima wao kwa wao, chakula wao kwa wao
  • Pesa wao kwa wao, kulea wao kwa wao
  • Kunyenyekeana ndio mpango wa Biblia (I Petro 3:7)
  • Mme hawezi kupenda mke wake na kumheshimu bila kunyenyekea.
  • Unyenyekevu ni jambo la uchanguzi wa moyoni watu wanapokuwa sawa (Ibrahimu na Sara)
  • Hivyo waume:
  1. Usimtusi mke wako
  2. Usimwone mke wako kuwa bure (don’t belittle her)
  3. Muelewe mke wako kuwa chombo dhaifu, kinguvu
  4. Mpende, nena naye, tumia wakati naye, mheshimu nyenyekea.
  • Hivyo wake
  1. Mheshimu mme wako, mpende na kumsifu
  2. Mtie nguvu na moyo
  3. Mpe sapoti .Tumia lugha tano za mapenzi (wakati pamoja, muguze, maneno ya faraja na pongenzi, zawadi, etc)
  • Hivyo watoto
  1. Wajulishe wazazi kile unachofanya
  2. Waambie marafiki zako ni nani
  3. Wajulishe jinsi ulitumia pesa waliokupa
  4. Wajulishe nani unaongea naye kwa simu
  5. Uliza ushauri kwa uamuzi wako kutoka kwa wazazi wako.
  6. Wajulishe wazazi wako unawapenda sana
  • Hivyo wazazi kwa watoto
  1. Wapende watoto wako, tumia wakati na wao
  2. Usiwalinganishe watoto hau kumpendelea moja
  3. Toa nidhamu katika upendo, uwe mfano mwema kwao
  • Niwaheshimue wakuu wetu na wazee (I Petro 5:5)

MWISHO

  • Tukanyenyekee Mungu kwanza. Jamii, viongozi wa kanisa, moja kwa mwingine, serikali na waajiri wetu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *