UJUMBE: USHINDI KATIKA VITA VYA MAISHA
SOMO: 2 YOHANA 4:4
Ushindi wako uko karibu zaidi kuliko hapo Mwanzo. Hii ni kwa sababu ulizaliwa kuwa mshindi. Wewe ni mshindi kwa sababu ndani yako kuna kitu ambacho shetani hawezi kuvunja. Maisha na uhai uliopokea tangu kuokoka.
Kesi yako haijafungwa mpaka wewe mwenyewe kuifunga. Haijalishi mahali ulipo sasa, au hali yako ya sasa, ulizaliwa mshindi.
Maisha ni vita na kila atakaye faulu ni lazima kupigana. Jiinsi unavyopigana ndivyo ushindi wako utakuwa mwingi. Hakuwezi kuwa na ushindi bila vita, ni baada ya vita mshindi hutangazwa.
Wakristo wengi bado hawajaamini wako vitani, lakini tunapigana kila siku na vita vyetu ni vya kiroho- 1st Wakorintho 2:14.
Hivyo ulizaliwa kupigana vita na pia ulizaliwa kushinda vile vita- 1st Yohana 4:4.
Shetani hakuogopi lakini anaogopa yeye aliye ndani yako- Yesu Kristo.
Ulitawazwa kushinda vita vyote lakini sharti upigane vile vita upate ushindi ulio tayari kwa ajili yako. Hebu tuone:-
- MFANO WA WASHINDI KATIKA BIBLIA
- Ayubu alipigana vita vikali vya maisha yake- Ayubu 1:14-22.
- Ayubu alipoteza kwa siku moja yote aliyofanyia kazi, watoto, mali na vyote viliteketea. Lakini Ayubu alichagua kumtumai Mungu wake katika vita.
- Katika mwisho wa vita vya Ayubu, Mungu alimrudishia Ayubu mara mbili ya alichopoteza.
- Vita unavyoendelea navyo katika maisha yako, haviwezi kushinda vile vya Ayubu. Lazima kupigana vita vyako kwa nguvu zako zote.
- Shetani anakupiga vita ili akutenganishe na Mungu wako na upendo wake.
- Lakini wewe kama Ayubu utashindana vita vyako.
- Daudi alipigana vita na Goliathi na Daudi akashinda vita- 1st17:45-51.
- Daudi aliamini kwamba Mungu amempa ushundi huo na Daudi akaungama ushindi huo.
- Daudi alipata ushindani mkuu kutoka kwa ndugu zake wakubwa- lakini Daudi hakufa moyo.
- Daudi alipata dhihaka kwa ndugu zake, kwa Sauli na watu wote lakini Daudi alishinda kwa kuwatolea ushuhuda wa uaminifu wa Mungu katika siku zake za kale.
- Daudi alitishwa na Goliathi, umbo lake, maneno yake ya kukashifu na matusi, lakini Daudi akayavumilia hayo.
- Daudi alitabiri ushindi wake juu ya Goliathi na kuungama imani yake ndani ya Bwana Mungu wake.
- Goliath wako anaweza kuwa na ujuzi mwingi zaidi, lakini Mungu wako hakuna wakati amepoteza vita hata moja.
- Mwamini Mungu, ungama ushindi wako, toa ushuhuda wa jinsi Mungu amekusaidia hapo mbele.
- Yabezi alishinda vita vya kukwama katika maisha- 1st Mambo ya nyakati 4:9-10.
- Yabezi alipambana na nguvu za kirho ambazo zilizuia maendeleo yake na kupenya katika maisha.
- Yabezi alikuwa na ujasiri mkuu juu ya Mungu wa Israeli, Yabezi aliomba maombi ya imani.
- Mungu aliyajibu maombi ya Yabezi yote, hivyo Yabezi akawa mtu wa heshima kuliko nduguze.
- Haijalishi vita vyako katika maisha, ushindi na kupenya kwako kuko katika Mungu.
- Filipo alishindana na yule mchawi kwa nguvu za Injili-Matendo 8:5-13.
- Filipo aliingia Samaria, mji uliokuwa chini ya nguvu za uchawi.
- Filipo alihubiri Injili kwa nguvu za Roho Mtakatifu, ishara na maajabu yalionekana.
- Kwa nguvu za Injili yule mchawi alipata kuokoka pamoja na watu wa mji wa Samaria.
- Paulo alishinda nguvu za shetani, changamoto na upinzani kwa mwito wake-Warumii 8:35-39.
- Palo alipokea ushindani mkuu sana katika huduma yake lakini nguvu za kushinda ziltoka kwa Mungu wake-Wafilipi 4:13.
- Hakuna vita vya kukushinda panapo Mungu. Tunao ushindi katika Yesu Kristo.
- HATUA ZINAZO HITAJIKA KWA WASHINDAJI.
- Maisha ya ushindi ndio maisha ya kawaida kwa walio katika Yesu Kristo.
- Ikiwa umeokoka na unaishi katika kushindwa basii mekataa Baraka zilizo katika wokovu.
- Unapoishi katika Roho Mtakatifu, huna haja ya kumwogopa shetani kwa maana unakaa katika ushindi.
- Tembea katika haki-2 Wakorintho 5:15.
- Kwanza ni lazima kutembea katika ujia wa uzima uliokatika Yesu Kristo.
- Lazima kuishi maisha yaliyo juu ya dunia hii na kawaida zake.
- Tembea katika upendo- 1st Yohana 4:17-21.
- Tembea katika utii- Kumbukumbu 11:26-28.
- Tembea katika msamaha- Mathayo 6:12-15.
- Tembea katika imani- Waebrania 11:6.
- Tembea katika umoja- Mwanzo 11:6.
- VIKWAZO VYA WASHINDI
- Usipende ulimwengu huu-1st Yohana 2:15-16.
- Urafiki wa ulimwengu utatufanya adui wa Mungu.
- Usipatie mwili nafasi- Warumi 8:8-13.
- Usishindwe na kuomba- Yakobo 5:16-18.
- Usinung’unike au kumlalamikia Mungu wako- Hesabu 14:1-5.
- Usimshuku Mungu wako hata wakati wa shida- Kutoka 14:13-16.
- Usidhubutu kujisalimisha kwa adui shetani- Mika 7:8.
MWISHO
- Pigana vita kwa ujasiri wote- Waefeso 6:11.
- Ushindi wako u karibu leo kuliko jana.
- Kumbuka yeye aliye ndani yako ni mkuu kuliko yule yuko nje- 1st Yohana 4:4.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- WHO IS SPEAKING TO YOU? - September 3, 2025
- CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO. - August 31, 2025
- THE GOD WHO BREAKS YOKES. - August 31, 2025
Great to get such knowleadge
My our heavenly God bless you for a wonderful and powerful sermon.