MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA
SOMO: YOHANA 2:1-11
Arusi ya Kana ndio ARUSI MASHUHURI SANA DUNIANI. Harusi hii ya Kana ilifanyika mwezi wa pili mwaka 27AD. Mpaka leo hakujakuwa na harusi kama harusi ya Kana. Hii ni kwa sababu ilikuwa na nguvu za Mungu (Divine power). Arusi hii hatujui Bwana na Bi. Arusi, hatujui walikutana wapi (shule ya upili, kanisani au kwa maonyesho).
Hatujui uchumba wao ulikuwa wa miaka mingapi. Hatujui ni watu wangapi walihudhuria arusi yao, hatujui umri wao, cheo chao, daraja yao kiuchumi. Hatujui kama walipata watoto, hatujui kama waliendelea katika ndoa mpaka kifo kuwatenganisha.
Lakini arusi yao hakujaonekana ingine kama yao. Ilipita ile ya Prince Charles na Diana arusi ya Kana. Yesu Kristo, wanafunzi wake na mama Mariamu walikuwepo. Hapa ndipo Kristo alifanya muujiza wa kwanza katika huduma yake duniani!!
Hapa Kristo aliidhinisha ndoa. Hii arusi haikuwa ya kwanza ya Yesu kuhudhuria kwa maana Kristo alikuwa kwa arusi ya Adamu na Hawa- Mwanzo 1:26-27; 2:22-24.
Yesu Kristo anajua kwamba arusi inahitaji kuheshimiwa na kila mtu na kitanda cha ndoa kuwa takatifu- Waebrania 13:4. Kristo anapenda kila ndoa kuendelea mpaka mwisho wa maisha. Mpango wa Kristo kwa ndoa ni tofauti na mpango wa mwanadamu. Mwanadamu hapendelei ndoa ya kudumu.
- Wengi wetu tunapenda kuishi nje ya arusi.
- Wengi wa wanaume hawapendi kujitoa (committment) lakini Kristo anasema ndoa ni ya kudumu (best interest)- Mithali 31:12.
- Ndoa za dhambi ni ngumu sana- Mithali 13:15.
- Ndoa bila Mungu ni sarakasi (drama).
- Dhambi inatupeleka mbali kuliko jinsi tulikusudia. Dhambi ni gharama ya juu zaidi kuliko jinsi ulikuwa umepanga, dhambi itakuweka wakati zaidi ya jinsi ulipanga kukaa!! (kuingia ni rahisi na kutoka ni ngumu)- Warumi 6:23.
- Ndoa inaleta urafiki (companionship) na furaha- Mithali 5:18.
- Ndoa inaleta usalama na udhabiti katika tendo la ndoa (satisfaction and enjoyment)- Mithali 5:19; 1 Wakorintho 7:1-4.
- Ndoa inaleta afya nzuri kuliko wasio katika ndoa!!- Mhubiri 9:9; Mithali 18:22.
Yohana mlango wa pili- unatupatia visa viwili; arusi ya Kana na Yesu kusafisha hekalu mle Yerusalemu kutoka ufisadi uliondelea pale. Leo tutazame arusi kule Kana- Galilaya. Kuhudhuria arusi ya Kana, Yesu anatuonyesha kwamba yeye ni Mwana- Adamu.
Hebu tuone:-
KRISTO ALISHIRIKI KATIKA TUKIO ZA MAISHA- Yohana 2:1-2
Hali: Arusi mle Kana.
- Arusi za Wayahudi zilikuwa tukio kubwa kabisa.
- Sherehe za arusi zilitendeka kwa siku saba.
- Katika arusi ya Kana, Yesu Kristo, Mariamu na wanafunzi wake walialikwa- V.1, 3, 5.
- Kwa kuhudhuria arusi, Yesu Kristo anatufundisha kwamba, Yesu si wa Jumapili pekee, anapenda kuhusishwa kwa kila tukio ya maisha yako!!
- Yesu Kristo ni Bwana juu ya yote- Matendo 10:36.
Mwito:
- Yesu Kristo alialikwa kwa arusi. Usikose kumwalika Yesu Kristo kwa tukio zako zote- 1 Wakorintho 6:19-20.
- Mfungulie Kristo kila sehemu ya maisha yako.
- Usimwache Yesu Kristo nje ya sehemu yoyote katika maisha yako- Ufunuo 3:20.
Kristo alizingatia mwaliko:
- Kristo alipoitwa na kualikwa, alihudhuria tukio- Mathayo 7:7-8; Yeremia 33:3.
- Badala ya kufadhaika mwite mkombozi wako- Wafilipi 4:6-7.
- Yesu Kristo atakupeleka mbali kwa haraka zaidi.
UWEZO WA KRISTO KATIKA TUKIO ZA MAISHA- Yohana 2:3-9
Shida v. 3.
- Wakati mwingi katika tukio za maisha divai inamalizika.
- Katika Uyahudi, kuishiwa na chakula na divai katika sherehe ilikuwa ni dhambi kubwa.
- Kuishiwa na divai ilikuwa ni kukosa heshima mbele ya wageni.
- Kuishiwa na divai ilikuwa ni dharau kwa walioalikwa.
- Kwishiwa na divai kulifanya umma kuwapiga faini jamii ya Bwana arusi.
- Kumbuka arusi na sherehe ziliendelea mpaka siku saba.
- Lakini maisha hayaendelei jinsi tumepanga. Wakati mwingine mambo yanaenda mrama- noma- Ayubu 14:1; Yohana 16:33; Mhubiri 2:23.
- Lakini Yesu Kristo anapokuwa katika sherehe zetu, miujiza itafanyika!!- Waebrania 4:15.
Katika shida ya bwana arusi, Mariamu.
- Mariamu alipendekeza mambo mawili kutatua ile shida.
Mkimbilie Yesu Kristo.
-
- Shida inapotokea, tumkimbilie yeye anao uwezo wa kugeuza mambo- Wafilipi 4:6-7.
Fuata maagizo na amri yake Kristo.
-
- Mariamu aliwaomnyesha watu Yesu Kristo.
- Mariamu alipata kibali na neema ya kuwa mama yake Kristo lakini Mariamu hana neema ya kuwagawia watu.
- Hivyo, usimwabudu Mariamu, bali Kristo.
- Mkimbilie Yesu Kristo- Mathayo 11:28; 1 Petro 5:7; Warumi 8:28; Matendo 16:31.
Matendo ya Yesu Kristo- v.6-9.
- Yesu Kristo alibadilisha hali.
- Hakuna mtu ajuaye shida zako kama jinsi Yesu Kristo.
UTOAJI (provisions) YA YESU KRISTO KATIKA TUKIO ZA MAISHA- Yohana 2:10-11
Utoaji wa Kristo katika mahitaji ya mwili.
- Yesu Kristo aliwapa walichohitaji.
- Yesu Kristo atakufanyia vivyo hivyo- Wafilipi 4:19.
- Twaona utoaji wa Kristo kwa Eliya- 1 Wafalme 17:1-6. Mjane wa Zarepathi- 1 Wafalme 17:10-16.
Utoaji (provisions) wa Yesu Kristo juu ya imani- V. 11.
- Wanafunazi wa Yesu Kristo walimwamini.
Utoaji wa Yesu Kristo juu ya kesho.
- Imani yao ilijengwa juu ya siku za kesho. Tumaini la watu juu ya Kristo iliinuliwa juu zaidi.
- Unapoona jinsi Kristo amekutendea leo, imani na tumaini yako juu ya kesho inajengwa zaidi.
MWISHO
- Yesu Kristo yuko katika kila tukio (event) katika maisha yako- Mathayo 11:29-31.
- Yesu Kristo anahusika katika kila jambo katika maisha yako.
- Yesu Kristo yuko tayari kukutana na kila hitaji yako, wokovu, uponyaji, hali mbaya.
- Leo, fanya kama jinsi Mariamu- mletee Kristo shida zako.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI. - October 19, 2025
- THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR. - October 19, 2025
- GOD DEFENDS HIS CHILDREN. - October 12, 2025