Swahili Service

TUMEKARIBIA MWISHO WA DAHARI

MFULULIZO:  SIKU YA MWISHO IMEKARIBIA]

SOMO:   MATHAYO 24:1-44

Kwa miaka 2000, watu wa dunia wameuliza swali hii, “je, Yesu Kristo atarudi lini?” swali la pili wameuliza ni “je, dalili za kurudi kwa Kristo ni  nini? Ujumbe wetu leo ni kujibu maswali haya. Kichwa cha ujumbe wetu leo ni “Tumekaribia   mwisho wa Dahari.

Katika Mathayo 24, wanafunzi wa Yesu Kristo walimliza maswali hayo. Tayari tumesema ni vizuri sana kujiepusha na kutaja siku na saa ya kurudi kwa Yesu Kristo, kwa sababu Kristo ametweleza saa na siku ni Mungu pekee ajuaye.

Katika somo letu, Yesu Kristo ametupa  dalili za kuja kwake na onyo kadhaa za kuepuka kudanganywa. Kwa kweli Yesu Kristo aliwakemea watu wa siku zake kutoelewa na ishara na dalili za nyakati zao na dalili za kuja kwake mara ya kwanza.

Katika Mathayo 16:2-4, kuna mambo mengi yametendeka kwa miaka 100 iliyopita kuonyesha “dalili za nyakati” usafiri na ufahamu umeongezeka zaidi. Katika mwaka wa 1914, mwendo wa motokaa ulikuwa kilometa 35 kwa kila saa, leo ni kilomita 120 kwa saa. Rocketi na satellites zina mwendo wa kilomita 40,000 kwa kila saa!! Ufahamu unaenda pamoja na usafiri. Hii ni dalili moja ya kuja kwa Yesu Kristo (Daneil 12:4)

Katika jumbe hizi tunazingatia zaidi Mathayo 24 and 25.

  • Hebu tuone dalili hizi tuone zile tayari zimefanyika na zile bado.
  • Katika Mathayo 24:1-8, twaona wanafunzi wa Yesu Kristo walikuwa wakipendezwa na umaridadi wa hekalu pale Yerusalemu.
  • Yesu Kristo alitoa unabii juu ya Hekalu kwa Hekalu litabomoshwa katika wakati wao.
  • Historia latueleza kwamba katika mwaka wa 70AD, jeshi kubwa la Roma, chini ya uongozi wa Generali Tito lilifika Yerusalemu na kulibomoa Hekalu. Moto mkubwa uliyeyusha hata na dhahabu ya Hekalu, askari wa Roma kupata ile dhahabu iliwapasa kuchukua kila jiwe na kulipitisha kwa moto hili wapate ile dhahabu, hii ilitimiza unabii wa Kristo hakuna jiwe litaachwa juu na jiwe lingine.
  • Hebu tuone dalili za kuja kwa Kristo:-

I.  DALILI YA UDANGANYIFU (MATHAYO 24:4-5, 11, 23-26)

  • Kumekuwa na udanganyifu na mafundisho ya uongo duniani, lakini leo umezidi zaidi.
  • Dini za uongo zimeongezeka kila kuchao.
  • Yesu Kristo ametueleza kwamba udanganyifu utaongezeka zaidi.

II.  DALILI YA VITA NA MATETEZI YA VITA (MATHAYO 24:6-8)

  • Tangu dunia hii kuumbwa kumekuwa na vita 15,000 katika historia ya mwanadamu.
  • Yesu Kristo alisema vita na matetezi ya vita yataongezeka, lakini mwisho wa dunia bado!!
  • Yesu Kristo alisema huo ni utugu wa kuzaa!!
  • Katika Mathayo 24:33, “nanyi kadhalika, myaonapo haya yote, tambueni ya kuwa yu karibu mlangoni.”

III. DALILI YA ISRAELI (Ezekieli 37:1-14)

  • Taifa la Israeli limeamishwa, na kutawanywa duniani na kutengana jamii, lakini ahadi za Mungu kwa taifa la Israeli, Mungu awezi kusahau kamwe.
  • Katika mwaka wa 1917, kulikuwa na wayahundi 25,000 katika Palestina.
  • Katika mwaka wa 1945 Wayahudi 500,000 waliishi mle Palesitina.
  • Tangu mwaka wa 1948 tangu Israeli kupewa utaifa wao na umoja wa mataifa mpaka leo idadi ya   wayahudi wanaoishi Israeli ni zaidi ya wayahudi millioni sita (6 Million)

IV.  DALILI YA NYAKATI ZA WATU WA MATAIFA (WAYUNANI) (LUKA 21:24-28)

  • Wakati huu tunaoishi unaitwa “majira ya mataifa hau “times of the Gentile”
  • Majira ya mataifa umewekewa wakati wake kwa kipimo.
  • Majira ya mataifa yalianza na Babeli “babylonia,” wakati wa uamisho wa Babeli mwaka wa (6060 B.C) wakati wa mataifa utaendelea mpaka wakati wa dhiki kuu duniani na kurudi kwa Kristo.
  • Huu ni wakati wa umoja wa mataifa yaani (United Nations)
  • Mungu ametoa nafasi kubwa kwa mataifa kumtumikia – lakini umoja wa mataifa (UN) umemkataa Mungu.
  • Katika mwaka wa 1967. Israeli walishika sehemu kubwa zaidi ya Yerusalemu tangu wakati wa Babeli.
  • Kilichobaki sasa ni uamusho mkuu wa kiroho kwa wayahudi kuliitia jina la Masihi Yesu waliyemkataa na kumuangika msalabani.
  • Pia pamebaki kujengwa upya Hekalu mle Yerusalemu.

V.  DALILI YA KIZAZI HIKI (MATHAYO 24:32-34)

  • Yesu Kristo alitumia mfano wa mti wa mtini (fig tree).
  • Mtini unatumika kwa kuonyesha Israeli.
  • Tangu mwaka wa 1948 Israeli imekuwa mtini mkamilifu.
  • Yesu aliposema “kizazi hiki” inawezekana maana yake ni nne (4).
  1. Kizazi cha wanafunzi wake
  2. Kizazi kilichoona vita vya kwanza vya dunia (W.W.I)
  3. Kizazi kilichoona Israeli kuwa taifa 1948.
  4. Kizazi kilichoona vita vya siku sita (six days war 1967) wakati Israeli waliteka mji wa Jerusalemu.
  • Uenda ni kizazi cha 1948 hau 1967
  • Swahili ni “je, kizazi ni miaka migapi?” 20,33,40,70,80,100
  • Hivyo uenda sisi tunaishi sasa ndicho kizazi kitakachoona mwisho wa Dahari

MWISHO

  • Je, mafundisho haya yana maana gani kwetu leo kama Wakristo?
  • Yesu Kristo alisema nini katika (Mathayo 24:36-44)
  • Je, tunayaishi maisha yetu kama Kristo anaweza kuja ghafla?
  • Je, ikiwa huu ndio mwisho wa dahari, kwa nini hatukeshi na kuomba na kutangaza injili ya Yesu kwa bidi Zaidi.
  • Je, wewe uko tayari Yesu ajapo leo. Huu ndio mwisho wa Dahari.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *