Swahili Service

EFESO-KANISA LILILOACHA UPENDO WA KWANZA

MAKANISA SABA YA UFUNUO

UFUNUO 2:1-7

Yesu Kristo anatembea katikati ya makanisa yake. Anaelewa sana na hali na shughuli katika kanisa lake. Haya makanisa saba ya ufunuo yanaweza kutazamwa kwa njia tatu.

  1. Tunaweza kuyatazama kiunabii.
  • Makanisa haya ya ufunuo yanaakilisha hatua saba za kanisa kwa miaka 2000 iliyopita. Kwa hio ni kweli, basi kanisa la Efeso ndilo kanisa la kwanza kabisa , yaani kutoka siku ya Pentekoste mpaka mwaka wa 100AD. Hili lilikuwa kanisa la juhudi nyingi kwa kueneza injili duniani kote lakini pia kanisa la kwanza lilianza kupoteza upendo wao wa kwanza mwisho wa Karne ya kwanza.
  1. Tunaweza kuyatazama tekelezi kawaida.
  • Nyaraka hizi zilitumwa kwa makanisa yaliyo kuweko Asia. Lakini ujumbe kwa haya makanisa saba unanena nasi katika kanisa la sasa. Mungu yuko na ujumbe kwetu hapa FBC Athi river kupitia nyaraka hizi saba.
  1. Tunaweza kuyatazama makanisa haya saba ya ufunuo kibinafsi. Yaani kwa ujumbe huu Mungu ananena na kila mmoja wetu na uhusiano wetu kibinafsi na Mungu wetu.

Hebu tutazame nyaraka hizi kama ujumbe tulioandikiwa sisi wenyewe na kanisa letu. Kanisa la Efeso, lilikuwa pale mji wa Efeso. Hili tupate kuelewa na ujumbe wa Yesu Kristo kwa kanisa la Efeso, kwanza ni kuelewa na jinsi mji wa Efeso ulivyokuwa.

  1. Efeso ulikuwa mji mkuu na wa maana sana kiuchumi. Mji huu ulijengwa kando ya mto wa Castor karibu na Bahari ya Aegean.
  • Efeso ni mji uliojulikana sana kwa sababu ya kilindi chake.
  • Wafanyi biashara kutoka dunia nzima walitembea Efeso ki biashara, hivyo Efeso ulikuwa mji tajiri sana. Kwa kweli Efeso ulikuwa mji tajiri zaidi kwa miji mingine Asia.
  1. Efeso ulikuwa mji wa maana sana kisiasa.
  • Roma ilikuwa imeipa Efeso cheti cha kuwa “mji huru,” Efeso ilijitawala “self-government.” Hivyo mji wa Efeso uliwavutia wambali.
  1. Efeso ulikuwa mji wa maana kidini.
  • Mle Efeso palikuwa na hekalu kuu la Diana hau Artemis. Efeso ilikuwa moja ya mashangao saba ya dunia wakati ule.
  • Diana alikuwa mungu wa kike, mungu wa uzazi na mapenzi.
  • Sanamu kubwa ilijengwa kwa Diana, mwanamke mwenye matiti mengi.
  • Hekalu la Diana lilijaa makahaba elfu elfu. Waliokuja kumwabudu Diana walifanya mapenzi na hawa makahaba.
  • Hekalu hili pia lilikuwa benki kuu.
  • Mji wa Efeso ulikuwa mji wa dhambi za kila haina. Mwana philosophia Heraclitus alisema “Huwezi kuishi Efeso usilie, kwa sababu ya dhambi zake.”
  • Ni kwa mji huu, Mungu alimtuma mtume Paulo kuhubiri habari njema-Matendo 18:19-21.
  • Mtume Paulo alipokuwa pale Efeso, ndipo aliandika kitabu cha 1na 2 Wakorintho.
  • Mchungaji Timotheo ndiye alikuwa askofu wa kwanza wa kanisa la Efeso-1 Timotheo 1:3.
  • Yesu Kristo anasema mambo manne juu ya kanisa hili la Efeso. Kanisa lilipoteza upendo wao wa kwanza, Hebu tujifunze:-
  1. YESU KRISTO ANATAZAMA SIFA ZAO (Ufunuo 2:2-3, 6)
  • Kristo anatazama kazi za Waefeso zilizo bora na kuwapongeza.
  • Efeso walikuwa na mengi mema, Kristo anawaeleza kwamba ameona kazi yao kwake na kwa ajili ya jina lake.
  1. Kwanza Kristo anawapongeza kwa huduma yao (Vs. 2)
  2. Matendo yao-Kazi zile tayari walikuwa wanafanya kwa ajii ya jina lake na utukufu wa jina lake.
  3. Taabu yao-Kristo ameona jinsi katika dhiki Waefeso walijikaza sana kumtumukia Kristo.
  • Efeso walimtumikia Kristo kila siku, kwa nguvu zao zote na kujitoa sadaka kutumika.
  1. Subira yao-Efeso walivumilia mateso na dhihaka, walivumilia upinzani na kukataliwa.
  • Hawa wakristo wa Efeso, walijua kwamba kanisa haliwezi kujijenga.
  • Hawa wakristo wa Efeso, walijua kanisa haliwezi kujidumisha lenyewe.
  • Hawa wakristo wa Efeso walijua kwamba kazi ya Mungu inahitaji fedha zao, wakati wao, karama na mali yao.
  • Hawa wakristo wa Efeso, walifahamu kazi ya Mungu si kama country club, bali ni mahali pa kufundishwa na kutoka nje kueneza habari njema.
  • Hawa wakristo wa Efeso walifahamu kwamba wameokolewa hili watumike (saved to serve).
  • Hawa wakristo wa Efeso walielewa kuokoka ni kutumia na kutumika katika kazi ya Bwana mpaka atakaporudi (spend and be spend)-Waefeso 2:10, Yakobo 2:18.
  1. Yesu Kristo anawapongeza kwa kujitenga kwao (2:2)
  • “Huwezi kuchukuliana na watu wabaya.”
  • Hawa Waefeso walijitenga na dhambi na wenye dhambi.
  • Uasherati na uovu ulikuwa pale Efeso lakini hawa walikataa kushiriki na wao.
  • Hawa waefeso walichukua msimamo, kukataa dhambi na kuishi tofauti na dunia yao.
  • Ndugu na dada, kuokoka ni kujitenga na dhambi na wenye dhambi (2 Wakorintho 6:17) “kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao asema Bwana, msiguse kilicho kichafu, nami nitawakaribisha” Waefeso 5:1-8.
  • Je, sisi nasi, tumejitenga na dunia hii na dhambi zake? Mathayo 5:16.
  1. Yesu Kristo anawapongeza kwa kushika mafundisho ya kweli ya Biblia (2:2,6)
  • Hawa wakristo wa Efeso walijaribu wale wajiitao mitume nao sio, wakawaona wakiwa waongo.
  • Waliopitia pale Efeso wakijiita mitume, watumishi wa Bwana, watu wa Mungu, waliwapima.
  • Waliwaona maneno yao hayalingani na Biblia, walikataa kuwasikiliza.
  • Waliwapima wale wajiitao “Nicolaitans”, “Nikao” =kuwashinda, “Laos”=watu.
  • Hawa Nokolaitans walipenda kuwatawala wakristo.
  • Leo pia, kuna wale wanaopenda kuwatawala wakristo kama wachawi.
  • Hawa wanapenda kukutawala kwa nyumba yako, pesa zako, mavazi yako na biashara yako.

“Nikolatans” walianzilishwa na mtu kwa jina Nicolas-Nicholas alifundisha hili ufahamu dhambi ni lazima kuitenda. Yaani endelea kumtumikia Bwana hata ingawa unaishi dhambini.

  • Leo hii mafundisho ya Nicolas yamekolea katika kanisa.
  • Waefeso walikuwa kama wakristo wa huko Brea-Matendo 17:11.
  1. Yesu Kristo aliwapongeza kwa kuvumilia na subra yao (2:3)
  • Kwa vyovyote vile, hili kanisa la Efeso lilipoteza sana mbele ya macho yao na yetu sisi.
  • Walimsimamia Kristo kwa vyovyote, iwe ni dhiki, mateso, majaribu na pingamiza zote-1 Wakorintho 15:58

 

  1. YESU KRISTO ANAFICHUA UKWELI WA NDANI (Ufunuo 2:4)
  • Baada ya kuwapongeza kanisa la Efeso, Kristo yuko na malalamishi juu ya kanisa hili la Efeso.
  1. Kristo alisitikika na mioyo ya wakristo wa Efeso.
  • Kristo anatazama mioyo-Waefeso 4:30.
  1. Kristo anaona ugonjwa wa mioyo yetu.
  • “Umeuacha upendo wako wa kwanza.”
  • Hawa Waefeso bado walikuwa wanampenda Kristo, lakini si kama hapo mwanzo.
  • Walipenda nyimbo zao lakini si Kristo.
  • Walipenda kazi ya Kristo, lakini si Kristo mwenyewe.
  • Hawakutosheka na upendo wa Kristo ndani yao.
  • Hii ndio shida ya kanisa la leo duniani.
  • Zamani ilikuwa ni ushuhuda ya jinsi tunapenda Kristo, leo tunasema juu ya kazi yake.
  • Kuokoka ni kuwa na mapenzi na Kristo.
  • Mungu anatafuta uhusiano bora na ushirika na watoto wake.
  • Kuna lugha tano za mapenzi:
  1. Wakati pamoja kwa pekee-(time spent together alone).
  2. Maneno ya sifa na pongezi-(Words of affirmation).
  3. Kuwa karibu na kuguzwa-(Touch of closeness).
  4. Zawadi za upendo-(Gifts).
  5. Matendo ya kuhudumiwa-(Acts of service).
  • Maisha ya kikristo ni upendo-Kumpenda Yesu Kristo kwa moyo wote.
  • Kukua katika Kristo ni kumpenda Kristo zaidi na kwa kina.
  • Tunapokosa kumpenda Kristo, basi utumishi wetu ni bure-1 Wakorintho 13:1-3
  • Upendo unakua (love grows). Kumpenda mke wako zaidi leo kuliko jana, watoto wako, kanisa lako, na kumpenda Kristo zaidi leo kuliko mbele.
  • Upendo wa kwanza unao moto, hauna kipimo.
  • Upendo wa Waefeso ulikuwa kama ule wa Martha-Luka 10:38-42
  • YESU KRISTO ANAWAPA DAWA YA SHIDA YAO (Ufunuo 2:5)
  • Yesu Kristo anawapa suluhisho na njia ya kusahihisha makosa yao.
  1. Kumbuka ni wapi ulikoanguka.
  • Anawaambia watazame nyuma.
  • Anataka wakumbuke aliyowatendea.
  • Anataka wakumbuke siku zile za kwanza wakati huduma yao kwake iliongozwa ni upendo.
  • Kumbuka jinsi ulivyompenda Yesu Kristo siku za kwanza za kuokoka.
  • Hatua ya kwanza kufufuliwa na uamsho wa Kristo ni kukumbuka.
  1. Ukatubu
  • Geuza akili na nia ili matendo yako yageuke.
  • Tubu dhambi ya kutompenda Yesu Kristo Bwana wako.
  • Ikiwa jamii, kazi, starehe hata kazi ya kanisa imekufanya usimpende Yesu Kristo vilivyo, tubu.
  1. Ukayafanye matendo ya kwanza
  • Rudi ukayafanye yale uliyoacha kutenda. Kusoma Biblia, kuomba, kukesha, ushirika, Injili, ushuhuda, kulia na hata kusifu.
  1. Yesu Kristo anasema ikiwa hatutatubu dhambi atakiondoa kinara chetu mahali pake.
  • Efeso walikataa kutubu, leo hamna kanisa la maana katika Efeso.
  1. YESU KRISTO ANAWAAHIDI DHAWABU YAKE WAKITUBU (Ufunuo 2:7)
  2. Dhawabu ipo kwa washindi.
  3. Washindi watapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu-Mwanzo 3:22-24
  • Washindi watapata ruhusa ya kuingia na kula matunda ya Edeni.

MWISHO

  • Je, umeacha upendo wako wa kwanza?
  • Je, umejipa shughuli nyingi za kutumika lakini bila upendo kwa Mwokozi?
  • Je, umeokoka? Je, umerudi nyuma? Rudi kwa upendo wako wa kwanza leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

5 thoughts on “EFESO-KANISA LILILOACHA UPENDO WA KWANZA”

  1. Pingback: My Homepage

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *