Swahili Service

KANISA LA SMIRNA-UAMINIFU HADI KUFA

MAKANISA SABA YA UFUNUO

SOMO: UFUNUO 2:8-11

Mji wa Smirna ulikuwa maili 35 (56 km) kutoka Efeso. Mji wa Smirna ulikuwa na uchumi mzuri sana. Idadi ya watu 100,000 wakati wa Yohana. Mji wa Smirna umekuweko tangu miaka 3000. Mbele ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, mji wa Smirna ulijengwa upya na kukua. Smirna uliitwa taji, yaani “crown city” kwa maana ulizungukwa na milima ukawa kama alama ya taji. Sifa zake zilitapakaa sana ukaitwa “Maua ya Asia” the “Flower of Asia.” Katika sarafu ya pesa zao-waliandika wakwanza  Asia, kwa ukubwa na urembo (First in Asia in size and beauty).

Mji wa Smirna ulijulikana sana kwa utoaji wa mane mane yaani (Myrrh). Smirna ulikuwa mji umepangwa kwa ujenzi wake. Hekalu nyingi zilijengwa pale kwa ibada ya miungu ya Roma. Hekalu kuu pale ilikuwa ya Zeus na Cybele.

Smirna kama jinsi Efeso ulikuwa mji huru. Smirna ulikuwa mji tajiri sana lakini  kanisa la Smirna lilikuwa maskini sana, kwa sababu ya kuteswa na Roma. Yesu Kristo aliwajia wa Smirna kwa faraja kwa sababu ya mateso waliopitia. Yesu Kristo analiambia kanisa la Smirna kwamba hata ingawa wao wamekuwa maskini, wao ni tajiri kupita kiasi!!

Kinabii, kanisa la Smirna limesimama kwa miaka ya 100AD-312AD kanisa katika mateso. Kuna neno kwa kila aliteokoka na zaidi kwa wale waliopitia majaribu kwa ajili ya Kristo Yesu.

Kristo anaaeleza Wakristo wa Smirna na kuwafariji kuwa waaminifu hata kufa. Tunahitaji kusimama imara hata wakati kila mtu ametuacha. Hebu tujifunze leo juu ya Smirna kanisa lililokuwa maskini, lakini tajiri katika Kristo. Smirna walikuwa waaminifu hata kufa:-

  1. SMIRNA ILIKUWA KANISA LILILO FINYIKA SANA (Ufunuo 2:9-10)
  • Kanisa la Smirna lilikuwa katika mateso mengi kwa sababu ua ushuhuda wa Yesu Kristo.
  • Kanisa la Smirna waliangaza kama nuru katika giza kuu.
  • Kwa sababu ya kuwa nuru ya ulimwengu Smirna waliteswa.
  • Hebu tuone jinsi Smirna walifinyika katika mateso.
  1. Walikuwa katika mateso na dhiki kuu, walifinywa kama jinsi ngano ya kusaga.
  • Mateso yao hayakutokana na wapagani tu, lakini kwa Wayahudi.
  • Wayahudi wa mji wa Smirna walijiunga na wapagani kuwaangamiza wakristo.
  • Yesu Kristo anawaita hawa Wayahudi “Sinagogi la Shetani.”
  • Kanisa la Smirna lilipokea matukano na mateso kutokana na hawa Wayahudi.
  • Kulikiwa na sababu kadhaa:-
  1. Hawa Wayahudi na wapagani waliwashitaki wakristo kuwa “wala watu” (cannibalism)
  • Hii ilikuwa kwa sababu ya meza ya Bwana yaani Holy communion.
  • Wakristo walipopokea divai na mkate na kusema huu ni mwili wa Kristo na damu yake, waliwaona kuwa wala-watu-(1 Wakorintho 11:24-26)
  1. Wakristo walipokutana walikula chakula pamoja kwa ushirika. Chakula hiki kiliitwa chakula cha mapenzi yaani “Agape feasts” or “love feasts”
  • Huu ulikuwa ushirika wa waumini, lakini walifitini kwamba walikuwa katika ngono.
  1. Wakristo walichukiwa kwa maana kuokoka kulitenganisha jamii.
  • Yesu Kristo tayari alisema kwa sababu ya kuokoka jamii zitatengana –(Mathayo 10:34-36)
  • Wakristo walionekana kutenganisha jamii.
  1. Wakristo walionekana kama wasioamini maana walikataa kuabudu miungu ya dunia, sanamu na kaisari (Emperor worship)
  2. Ilikuwa sheria ya Roma, kumwabudu kaisari na kusema “kaisari ni bwana”
  3. Wakristo wa Smirna waliona umaskini
  • Kwa sababu ya mateso, mali yao, biashara zao, shamba na nyumba zao zilichukuliwa na serikali.
  • Walikatazwa kazi, vyeo na uongozi.
  • Kumtumikia Kristo kuliwagharimu kila kitu.
  1. Wakristo wa Smirna walifungwa gerezani (Vs. 10)
  • Yesu Kristo aliwaambia mambo bado, dhiki itazidi.
  • Yesu Kristo anawaambia kwa “Siku kumi” majaribu kumi, hau kitambo cha muda mfupi ujao majaribu na mateso yataongezeka!
  • Gereza za siku za Roma zilikuwa ni kungoja kifo. Njia pekee ya kutoka gerezani ilikuwa ni kufariki.
  • Njia ya kifo Roma ilikuwa ni kuchomwa moto ukiwa hai, kukatwa shingo kwa upanga, kutupwa kwa wanyama wakali, msalaba na zinginezo.
  • Kanisa la Smirna lilikuwa katika taabu nyingi sana.
  • Askofu Polycarp, mzee wa miaka 86, alikataa kumwabudu kaisari, wakamchoma moto akiwa hai. Alisikika akisema “Kwa miaka 86, nimemtumikia Kristo na hakuna kibaya aliyenitenda, hivyo ninawezaje kumkataa mfalme na Mwokozi wangu?”
  • Biblia inasema “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa”-2 Timotheo 3:12.
  • Sababu kubwa kwa wakristo kuchukiwa siku zile ni “Kumpenda Yesu Kristo.”
  • Tunapoendelea hapa kwetu Kenya na dunia yote mateso ya wakristo yanazidi.
  • Shetani, Ibilisi ameamua kujitokeza peupe .Mpango mpya wa dunia umeanza sasa.
  1. Serikali ya dunia moja-(One world government)
  2. Kanisa na dini moja duniani-(One world religion)
  3. Pesa moja duniani-(One world currency)
  4. Masomo moja ya dunia-(One world school curriculum).

Umoja wa Mataifa tayari wametangaza vita juu ya kanisa la Kristo.

  • Mateso mengi yatatokea kwa kanisa lenyewe vile tumeona kwa “Inter-Faith Council”
  1. SMIRNA LILIKUWA KANISA LA KUTEGEMEA (Ufunuo 2:9)
  • Wakristo wa Smirna walilipa gharama kubwa ya imani yao.
  1. Walikuwa na ushuhuda timilifu.
  • Katika makanisa saba yaliopokea waraka kutoka kwa Yesu Kristo, ni kanisa la Smirna na Filadelfia pekee hayakupokea lawama kutoka kwa Mwokozi.
  • Yesu Kristo alikuwa akitazama mwenendo wa Imani yao, akawaona wakiwa timilifu.
  1. Walikuwa na ushuhuda wa nguvu sana.
  • Ninaijua dhiki yako, pamoja na giza kuu pale Smirna- walishika imani yao.
  • Hawakuogopa adui zao wala kutishwa na matukano yao.
  • Kama Mtume Paulo, Smirna walisimamia imani yao-(Wafilipi 3:8-10)
  • Tangu kanisa kuwa duniani wakristo milioni 70 wameuliwa kwa sababu ya imani yao.
  • Kila mwaka wakristo 300,000 wamekufa kwa ajili ya imani yao ndani ya Kristo.
  • Siku ya mateso ikifika hapa Kenya, Je, utakuwa tayari kufa?
  • Hebu tumwombe Mungu tuwe na imani timilifu.
  • KANISA LA SMIRNA LILIPATA FARAJA YA KRISTO (Ufunuo 2:8-11)
  • Yesu Kristo aliwajia wa Smirna na kuwafariji.
  1. Mbingu yote ilijiusisha kirasmi na shughuli za Smirna.
  • Kristo anasema nina matendo na dhiki yako.
  • Anawaeleza kwamba kile wanachopitia ni kuu kuliko wao wenyewe.
  • Anawaeleza Shetani anawatumia watu wa Smirna kuwadhiaki lakini si wao bali waanamdhiaki Kristo mwenyewe.
  • Kristo anataka wajue kwamba yeye yupo pamoja na wao katika mateso na matukano yao.
  • Yesu Kristo yuko pamoja nawe katika mateso yako-(Waebrania 13:5, 4:15; Yohana 14: 16-18)
  1. Mbingu yote ilihusika katika kazi zao.
  • Kristo amewajia kama “mwanzo na mwisho”. Maana yake ni kwamba Kristo ndiye “Mimi ndimi”
  • “Wa kwanza na mwisho” maana yake ni kwamba Kristo ni yeye anayeongoza mambo yote.

“Aliye kuwa amekufa, kisha akawa hai” Maana yake ni kwamba, Kristo tayari amepitia yale tunayopitia-(Waebrania 2:18, Yohana 10:29, 2 Timotheo 1:12).

  • Kwa chochote unachopitia, Kristo alipitia ili awe faraja kwako leo-(Warumi 8:37, 2 Wakorintho 2:14, Warumi 8:31)
  1. Rasili mali yao iko mbinguni (Vs. 9)

Yesu Kristo aliwaambia “Ninajua dhiki na umaskini wako (lakini wawe tayari)

  • Umaskini wao uliwanunulia utajiri mkuu mbinguni.
  • Walikuwa maskini hapa duniani lakini matajiri wa mbinguni- (Mathayo 6:19-21, 2 Wakorintho 6:10).
  • Siku yaja wakati dunia hii itachukua mali, mashamba na vitu vyetu; hii ikifanyika kumbuka faraja za Yesu Kristo.
  • Uwe mwaminifu mpaka mwisho.
  1. Walikuwa na urithi wao mbinguni (Vs. 10-11)
  • Imani yao ilikuwa tayari imewanunulia uzima wa milele mbinguni.
  • Kristo aliwaambia hata wakifa ni mara moja tu. Mauti ya pili haina nguvu juu yao.
  • Kristo amewaahidi uzima wa milele na taji la uzima “A crown of life”-“Stephanos.” Taji ya ushindi.
  • Kila aliyepotea atakufa mara mbili. Yeye atakufa na kutengana na Mungu duniani.
  • Ziwa la moto ni milele na milele, bila Mungu, tumaini na huruma-(Ufunuo 20:11-15).

MWISHO

  • Kanisa, huenda mambo yakawa mabaya zaidi hapa duniani kabla hatujahama dunia hii.
  • Huenda majaribu, dhiki na matukano yataongezeka.
  • Lakini baada ya vita-Tutafarijiwa na Bwana.
  • Hivyo vumilia, uwe mwaminifu hata kufa.
  • Je, umeokoka? Okoka sasa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “KANISA LA SMIRNA-UAMINIFU HADI KUFA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *