MFULULIZO: NGUVU ZA KUISHI
SOMO: ZABURI 62:11
Nguvu ni zake Mungu. Kuna nguvu za aina nyingi lakini kuna nguvu zilizo juu zaidi ya zote, nguvu za Yehova Mwenyezi Mungu.
Mungu ni mkuu, nguvu zote ni zake. Mungu hawezi kulinganishwa na yeyote yule. Nguvu za Mungu ziko juu ya yote duniani, mbinguni na juu ya viumbe vyote- Isaya 45:21.
Nguvu za Mungu ziko katika Yesu Kristo. Yesu Kristo amepewa jina lililo juu ya majina yote, uwezo na nguvu zote mbinguni na duniani- Mathayo 28:18.
Hebu tuone:-
- UTOFAUTI WA NGUVU ZA MUNGU
- Kuna aina nyingi za nguvu duniani.
- Nguvu za cheo.
- Kuna watu walio na nguvu za vyeo vyao na mamlaka katika roho na katika maisha ya kawaida.
- Mfalme Nebukadneza alikuwa na nguvu kiasi akatisha vijana watatu Waebrania.
- Aliwauliza, je, ni Mungu yupi anaweza kuwaokoa kutoka kwa mikono yangu- Danieli 3:13-15.
- Nguvu za cheo na uongozi ni za muda. Zinamalizika na muhula wa “mamlaka na enzi ya mtu na ofisi yake.”
- Kama mtu anakutisha na nguvu za cheo na mamlaka ya ofisi yake, unaweza kuongea na Mungu na kuvunja nguvu za huyo mtu.
- Nguvu za kuungana na mamlaka (power of personality connection.)
- Hizi nguvu zinakuja kwa kuungana na mtu aliye katika mamlaka.
- Hawa watu hawana nguvu zao wenyewe lakini ni kwa sababu ya kuungana na wenye nguvu.
- Nguvu hizi zinatumika kujinufaisha binafsi au kutisha watu.
- Hamani alitumia nguvu hizi kuwanyanyasa Wayahudi na zaidi Mordekai- Esta 3:5-10.
- Nguvu za kudanganya na kutongoza.
- Wanawake kama jinsi Delila, alitumia nguvu hizi kumwangusha Samsoni- Waamuzi 14:15-18; 16:4-20.
- Roho zipo za kudanganya watu- Timotheo 4:1-2.
- Nguvu za utajiri na mali.
- Wanatumia utajiri na mali kupata chochote.
- Naamani alifikiri utajiri utampa uponyaji wa Mungu- 2 Wafalme 5:5-12.
- Mchawi mkuu wa Samaria pia alifikiri anaweza kununua nguvu za Mungu kwa fedha- Matendo 8:18-24.
- Nguvu za uaguzi- Divination.
- Hizi ni nguvu za kishetani kama jinsi uchawi, unabii wa uongo, uganga na uaguzi.
- Wanatumia nguvu hizikuona yajayo na kutatiza hatima ya watu- Matendo 16:16-18.
- Nguvu za kunyanyasa kimapepo- Luka 8:28-39.
- Nguvu za Roho Mtakatifu.
- Hizi ni nguvu za Mungu aliye mbinguni.
- Hizi ni nguvu bila kipimo, nguvu za Mungu.
- Nguvu za Mungu ziko ndani ya Yesu Kristo.
- Yesu Kristo anawapa wanawe hizi nguvu- Matendo 1:8; Luka 10:19-20.
- UKUBWA NA KIPIMO CHA NGUVU ZA MUNGU
- Kuna vipimo vya nguvu za Mungu kwa kadri ya mapenzi yake.
- Nguvu za Mungu kuumba.
- Mungu aliviumba vitu vyote mbinguni na duniani kwa uwezo wa nguvu zake- Wakolosai 1:16.
- Leo hii watoto wa Mungu wamepewa uwezo wa kufanya miujiza ya kuumba upya viungo vya mwili katika uponyaji- Isaya 43:18-19.
- Nguvu za Mungu kulinda.
- Nguvu za Mungu zina uwezo wa kulinda watu wake kutoka kwa kila ubaya, hatari na janga- Marko 4:37-40; Isaya 54:17.
- Nguvu za Mungu urejesho.
- Mungu anazo nguvu za kurejesha uzima, afya, nguvu, mali, tunapomwita kwa imani.
- Nguvu za Mungu kuvunja na kuharibu.
- Nguvu za Mungu kuharibu nguvu za shetani na giza katika maisha ya watoto wake- 1 Yohana 3:8; Kutoka 15:1, 19.
- Nguvu za Mungu kuokoa na kukomboa.
- Mungu anao uwezo na nguvu wa kuokoa wote wenye dhambi, wenye dini, upumbavu, kuudhi, wabaya, Sauli, Towashi, Kornelio, mwanamke msamaria- 2 Wafalme 7:1-2.
- Nguvu za kutosheleza (Provision).
- Wote wenye kukosa vitu, maskini, kukosa mvua- Wafilipi 4:19.
- Nguvu za kufanya kazi yake (Impartation).
- Nguvu za utendaji- Matendo 2:1-4; marko 16:17-18.
- UTAWALA KUPITIA NGUVU ZAKE
- Utawala juu ya dhambi na tabia za dhambi- 1 Wakorintho 15:57; Warumi 6:9-14.
- Utawala juu ya mwili- Wagalatia 5:16-21.
- Utawala juu ya ulimwengu- Waefeso 1:19; 1 Yohana 5:4-5.
- Utawala juu ya shetani na ufalme wake- Luka 10:19-20; Wakolosai 1:13.
- Mamlaka na utawala juu ya magonjwa na udhaifu wote- Isaya 53:5-6.
- Utawala juu ya hofu- 2 Timotheo 1:7; Warumi 8:15.
- Utawala juu ya shida , dhiki, na magumu katika maisha yetu- Yohana 16:33.
MWISHO
Masharti ya kupata nguvu za Mungu;
- Lazima kuokoka kamilifu- Yohana 1:12.
- Tembea kila siku na Mungu- Zaburi 45:7.
- Ishi kwa imani kila saa- Isaya 1:19.
- Omba bila kukoma- Matendo 16:25-26.
- Zaa matunda ya Roho Mtakatifu.
- Shuhudia Yesu Kristo kwa wote.
- Ishi katika kutarajia kurudi kwa Yesu Kristo kila saa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
