Swahili Service

SIRI YA MAFANIKIO

MFULULIZO: MAFANIKIO

SOMO: KUTOKA 33:12-23

 

Siri ya kufanikiwa, ushindi na nguvu za utendaji na upako wa Mungu, inakaa katika uwepo wa Mungu pamoja nasi na katikati yetu. Je, unataka ushindi juu ya matatizo yako katika Bwana? Basi unahitaji nguvu za uwepo wa Mungu. Ujumbe huu wa leo ni kukufungua macho upate kuona kwamba uwepo wa Mungu unaleta manufaa makuu sana. Hebu tusome tena Kutoka 33:13-15.

Huyu alikuwa ni Musa akimuuliza Mungu waende safari pamoja.

Musa hakumuuliza Mungu ishara na miujiza bali alimuliza Mungu amwonyeshe njia zake.

Mungu alimjibu Musa na kumwakikishia ya kwamba uwepo wake utakuwa pamoja naye.

Wakristo wengi sana hawaelewi na uwepo wa Mungu. Wachungaji wengi pia hawajaelewa na nguvu za uwepo wa Mungu.

Mtu awaye yote ambaye hajajua na kuelewa na uwepo wa Mungu hana ruhusa ya kuwaeleza wengine juu ya Mungu. Mtu awe ni mchungaji, askofu, mwimbaji, mzee wa kanisa hana ruhusa kuwaeleza watu chochote ikiwa yeye ni mgeni kwa mambo ya uwepo wa Mungu na nguvu zake.

Kuwa na uwepo wa Mungu pamoja nasi ni faida kubwa zaidi kuliko hata Utajiri, heshima, sifa na mamlaka. Tunaweza kwenda pande zote ikiwa Mungu yupo pamoja nasi.

Katika uwepo wa Mungu kuko na furaha kamili, lakini pasipo na uwepo wake patakuwa na kuvunjika moyo, kukata tamaa, maangaiko na kupungukiwa.

Je, wewe unao uwepo wa Mungu kwa maisha yako?

Zaburi 51:11, “Usinitenge na uso wako wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee.”

Daudi alimwambia Mungu anaweza kuchukua mambo mengine yote, lakini uwepo wa Roho Mtakatifu amwachie.

Daudi alisema katika jambo la uwepo wa Mungu, Mungu asinyamaze, hata iwe nidhamu-lakini Mungu asichukue uwepo wake kutoka kwa Daudi.

Musa kweli alikuwa na shida  nyingi za wana wa Israeli, mara walitaka kumpiga mawe, lakini alikumbuka ahadi ya Bwana “Uwepo wangu utaenda pamoja nawe na nitakupatia amani.”

Hivyo unaweza kuwa na shida, kila mahali matisho ya kila aina-lakini panapo uwepo wa Mungu, hakuna shida.

Unapo songa karibu na Mungu ndivyo uweza na uwepo wake uko karibu nawe.

Unapo kuwa mbali na Mungu ndivyo uko karibu na shetani.

Mwanzo 4:16, “Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.”

Mwanzo 4:13, “Kaini akamwambia Bwana adhabu yangu imenikulia kubwa haichukuliki.”

Ni hukumu kubwa sana kuwa mbali na uwepo wa Mungu.

Omba sana usipate hukumu kubwa kama ya Kaini.

Afadhali kupigwa na radi au kuangukiwa na milima na mawe kuliko kuwa mbali na uwepo wa Mungu.

Afadhali kukatwa mkono, mguu au kutolewa macho yako kuliko kuishi mbali na uwepo wa Mungu.

Kaini alienda Nodi mashariki mwa Edeni mbali na uso wa Mungu.

Mwanzo 3:8, Adamu na Hawa walienda mbali na uso wa Mungu.

Adamu na Hawa walianza kulaumiana. Unapoenda mbali na Mungu ni wewe ulaumiwe, lakini si kanisa, mke wako, au mume wako, au wazazi wako au shetani-shida ni wewe.

Kazi ya shetani ni kuiba, kuua na kuaribu.

Unapojikuta katika dhambi, tubu, mlilie Bwana, tengeneza ushirika wako na BWANA,omba utakatifu, omba uwepo wa Mungu.

Yona alopoenda mbali na Mungu, alitubu dhambi zake-Yona 2.

Isaya, Yakobo, Musa-walipoona uwepo wa Mungu walibadilika.

Tunapokuwa katika uwepo wa Bwana hakuna shetani, uchawi na nguvu za giza haziwezi kukushinda.

JINSI YA KUJUA NGUVU ZA UWEPO WA MUNGU

  1. Usicheze na wakati wa utulivu (quiet time). Tunahitaji kila mmoja wetu kuwa na wakati wa binafsi-kutilia mbele za Bwana kila siku.
  • Kila siku lazima kukariri neno na kuazimia neno lake.
  1. Usikatae ushirika wa watakatifu.
  • Usikose ibada pasipo sababu kubwa kama kifo-Waebrania 10:25.
  1. Uwe na njaa na kiu ya haki.
  • Ishi katika utakatifu, tafuta Bwana kila siku.
  1. Fuata kanuni ya maombi-1 Wathesalonike 5:16-22.
  2. Kuwa karibu sana katika ushirika na Roho Mtakatifu.
  3. Omba sana Mungu akuonyeshe njia zake.

KITU KIMOJA KUNAHITAJIKA

  • Nyenyekea kwa Bwana.
  • Tafuta kuokoka kamili-kabisa.
  • Amua kabisa kutembea na Mwokozi wako.
  • Ishi katika imani na kumtegemea Mwokozi wako.
  • Mlilie Bwana siku zote kwa utakaso na ujazo wa nguvu zake, kwa mafanikio

MAOMBI

  • Mungu wangu nionyeshe njia zako katika Jina la Yesu Kristo.
  • Roho wa ishara, maajabu na miujiza tawala juu ya maisha yangu katika Jina la Yesu Kristo.
  • Kila mbinu na agenda ya shetani juu ya maisha yangu na nyumba yangu, shindwa sasa katika jina la Yesu Kristo.
  • Nguvu za uchawi juu ya maisha yangu toweka sasa-katika Jina la Yesu Kristo.
  • Kila giza ndani ya maisha yangu toweka sasa, katika Jina la Yesu Kristo.
  • Kila kambi ya adui zangu sambaratika sasa katika Jina la Yesu Kristo.
  • Uwepo wa Mungu enenda pamoja nami siku zote-Katika Jina la Yesu Kristo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *