MFULULIZO: YAKOBO; ALIFANYA MIEREKA NA MUNGU.
SOMO: MWANZO 30-31
Tunaishi katika ulimwengu ambao watu wanatafuta sana kwa bidii fedha, utajiri, mali na ustawi. Kustawi ndio lengo la wengi wetu. Naye Mungu pia anapenda kutupa ustawi maana ni ahadi yake kustawi kwetu. Mungu alimwahidia Yakobo kumbariki na kumpa ustawi, hivyo Yakobo alistawi sana katika miaka ya maisha ngumu sana mle Harani. Mwanzo 30:43- “Kuwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi na vijakazi, watumwa, ngamia na punda.” Katika kuishi kwake Yakobo, katika nyumba ya Labani mjomba wake na pia shemeji, Yakobo alipokea udanganyifu kwa udanganyifu. Yakobo alidanganywa sana na Labani, pia katika nyumba yake Yakobo palikuwa na vita vikali katika wake zake Lea na Raeli. Labani pia alimdanganya Yakobo kimshahara wake. Yakobo kweli alikimbia Beer-Sheba kutorokea uhasama lakini akapata zaidi mle Harani. Hivi ndivyo Yakobo anawaambia wake zake. Mwanzo 31:6-7-“Ninyi mmejua ya kwamba kuwa nguvu zangu zote nimemtwikia baba yenu. Na baba yenu amenidanganya akabadili mshahara wangu mara kumi, lakini Mungu hakumwacha kunidhuru.” Labani alipoona Yakobo anastawi, Labani alibadili nia na sheria za kazi. Labani alijaribu sana kumweka Yakobo chini. Kwa sababu ya shida, Yakobo aliamua kurudi Beer-Sheba kwa baba yake Isaka. Mwanzo 30:25- “Ikawa Raeli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, nipe ruhusa niende kwetu na kwenye nchi yangu.” Labani alijitoa kumsaidia Yakobo-Mwanzo 30:31- “Akamuuliza, nikupe nini? Yakobo akasema, usinipe kitu, ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda.” Yakobo hakutaka kuwa mdeni kwa yeyote yule. Yakobo alikubali kuwalisha kondoo wa Labani, walio wa madoadoa na marakaraka na pia mbuzi walio madoadoa na marakaraka kama mshahara wake. Mungu akiamua kukubariki hakuna atakayekataa. Yakobo alijiweka katika mkono wa Mungu wake, kamtumaini Mungu kwa matokeo ya kazi ya mikono yake- Mwanzo 30:33-36. Mwishowe Yakobo aliamua kurudi nchi ya babaye- Mwanzo 31:3; 17-18. Kwa miaka 20 miaka ya shida Yakobo alipata kuwa tajiri sana akastawi zaidi na zaidi- Mwanzo 30:43; Mwanzo 32:10. Tunakuwa zaidi katika shida zetu kuliko wakati wa utulivu na amani.
- Yakobo alibarikiwa na jamii, watoto, watumishi, wanyama na mali. Lakini je, ni nini siri ya ustawi na Baraka za Yakobo? Hebu tuone siri na kanuni saba za kustawi kibiblia:-
KANUNI ZA USTAWI: BARAKA ZINAFUATA UTII
- Mtu anapo mtii Yesu Kristo, Baraka lazima kumfuata.
- Katika Biblia kila amri ya utii inafutana na ustawi.
- Kumbukumbu 28:2- “Na Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana Mungu wako.”
- Zaburi 23:6, Mwanzo 12:2- masharti ya kubarikiwa kibiblia ni utii. Tunapomtii Mungu tunapata kibali cha Mungu.
- Pia wengine wanabarikiwa wanapomtii Mungu- Mwanzo 30:27.
KANUNI ZA USTAWI: UWE NA TAMAA YA KUFAULU NA KUSTAWI- Mwanzo 30:30
- Yakobo alikuwa na tamaa ya kustawi kibinafsi.
- Tamaa ya kustawi inahitaji kuwa kubwa zaidi kuliko hofu yao kuanguka- Zaburi 37:4.
- Unapotamani sana kustawi, utastawi.
KANUNI ZA USTAWI: BIDII YA KAZI INALIPA
- Methali 14:23-“Katika kila kazi kuna faida. Bali maneno ya mdomo huleta hasara tu.”
- Methali 21:5-“Mawazo ya wenye bidii huwaletea utajiri tu, bali kila mwenye pupa, humletea uhitaji.” (Hasty short-cuts lead to poverty).
- Hakuna chema kitakuja rahisi. Yakobo alifanya kazi kwa bidii nyingi zaidi. Mwanzo 31:6-“Nanyi mmejua ya kwamba kuwa nguvu zangu zote nimemtwika baba yenu.” Mwanzo 30:26; 31:40.
- Yakobo alifanya kazi kwa bidii miaka 20 na Mungu akambariki sana.
KANUNI ZA USTAWI: UWE MKWELI
- Mungu anawabariki walio kweli- Methali 28:20; 13:11, Mwanzo 30:33.
- Yakobo alikuwa mwaminifu katika kazi yake kwa Labani- Mwanzo 31:38-42.
- Matokeo ya uaminifu na ukweli wa Yakobo ulizaa matunda- Mwanzo 31:9.
KANUNI ZA USTAWI: USITOROKE UTOSHELEVU WA MUNGU
- Shida yetu moja ni kuwa baada ya kufanya kazi ngumu na miaka ya kazi nyingi, tunatoroka kazi wakati wa shida.
- Kumbuka Baraka na kibali cha Mungu kinaanguka mahali Mungu amekuweka.
- Yakobo alikuwa na shida nyingi sana nyumbani mwa Labani- lakini hapo ndipo Mungu alimbariki Yakobo.
- Mungu anakudumisha mahali pa shida, usihame mpaka upate sauti ya Mungu kuhama.
- Elimeleki na Naomi walihama Bethlehemu wakati wa njaa, wakaenda Moabi. Elimeleki na wanawe wawili walikufa mle- Ruthu 1:1-6.
- Usihame toka pale Mungu amekuweka kazi, ndoa, nyumba, mji, kanisa mpaka Mungu aongee nawe- Mwanzo 31:13.
KANUNI ZA USTAWI: TAFUTA AMANI NA WATU WOTE
- Wakati unapofika wa kuachana, wachaneni kwa amani.
- Fahamisha jamii yako ili wawe na amini kuhama na kuachana.
- Yakobo alitafuta idhini ya jamii yake kabla kuhama Harani- Mwanzo 31:4.
- Jamii ilikubali kuhama- Mwanzo 31:15-17.
- Sawazisha mambo kabla hujaenda zako.
- Yakobo alifanya amani na Labani- Mwanzo 31:43-44.
- Labani aliwapa Yakobo na jamii kwaheri ya kuonana- Mwanzo 31:54-55.
KANUNI ZA USTAWI: FANYA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KUWA MKUU
- Yakobo alifanya uhusiano wake na Mungu kuwa mkuu zaidi.
- Uhusiano wa Yakobo na Mungu ulianza pale Betheli na umedumu mpaka Betheli mara ya pili.
- Mungu aliongea na Yakobo kwa ndoto, maono na uso kwa uso.
- Yakobo alijitoa kumtolea Mungu sadaka na fungu la kumi- Mwanzo 28:22.
- Yakobo alimjengea Bwana madhabahu- Mwanzo 35:1.
- Yakobo alihusisha jamii yake katika ibada- Mwanzo 35:3.
MWISHO
- Mungu anapenda sana kutubariki lakini mara nyingi tunahama mbali na uwepo na utoshelevu wake.
- Shetani anapenda kukuweka katika vita na watu mpaka nguvu zake zote zinaisha.
- Fuata kanuni hizi za ustawi na hakika wewa na fadhili zitakufuata siku zote za maisha.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
