Swahili Service

JIPE MOYO KATIKA BWANA

SOMO: 1 SAMWELI 30:1-8

 

Kila mmoja wetu atapitia wakati wa kuvunjika moyo. Wakati wa kukata tamaa tunahitaji kumtazama Mungu na kuomba msaada wake.

Mioyo yetu inapomtazama Mungu, Mungu atatupa nguvu katika hali ya kukata tamaa.

Leo hii watu wengi wamekata tamaa na mioyo yao kuzimia katika taabu zao. Wengine wamekata tamaa kwa sababu ya watoto wao, mke, mme, jamii, kanisa na serikali.

Ni maombi yangu hivi leo wewe pamoja nami tutamtazama Mungu katika hali tatanishi. Mfalme wa Pilistia, mfalme Akishi alimpa Daudi mji wa Siklagi uwe mji wa salama kwa Daudi.

Siku moja Daudi na watu wake walipoenda vitani kuwasaidia Wapilisti, Daudi na watu wake walirudi mara kwa maana wakuu wa Wapilisti hawakuwa huru kuenda vitani huku wakisaidiwa na Daudi na watu wake.

Hivyo Daudi na askari wake walirudi nyumbani Siklagi.

Walipofika Siklagi waligundua kwamba Waamaleki walichoma Siklagi na kwenda zao huku wakiwachukua watoto wake na mali yote na kuchoma mji wote chini.

Biblia inatueleza jinsi watu wengi Shujaa wa imagine walivunjika mioyo yao na kukata tamaa. Musa, Eliya, Yona, kiasi wakataka kufa.

Daudi ni mtu aliyemtegemea Mungu zaidi na kuutafuta uso wa Mungu.  Nyakati zingine pia Daudi alivunjika moyo sana- Zaburi 38:6.

Lakini wewe pamoja nami, tunaweza kumtegemea Mungu katika hali ya shida zetu kwa maana tunazo ahadi nyingi kwa Mungu, atatusaidia.

  • Hivyo jipe moyo, jitie nguvu katika Bwana wakati wa janga, mateso na pia kuachwa.
  • Daudi alijua sana nguvu zake ziko kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi- Zaburi 121.
  • Daudi alijitia nguvu kwa ajili ya wote waliomfuata.
  • Je, umevunjika moyo? Jipe moyo, jitie nguvu. Hebu tutazame:-

HALI INAPOKUWA NGUMU NA KUVUNJIKA MOYO.

  • Kuvunjika moyo na kukata tamaa ni hali ya muda mfupi tunapopoteza mwelekeo na furaha kwa sababu ya hali mbaya maishani.
  • Kujipa moyo na kujitia nguvu ni wakati tunapopata mwelekeo na moyo wa kuendelea na safari kutoka kwa Mungu kwa hekima na ukweli wake.
  • Katika janga kuu iliyompata Daudi na watu wake pamoja, walivunjika moyo, walilia mpaka kuishiwa na nguvu lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA Mungu wake.

Kuvunjika moyo na kukata tamaa kulionekana kwa jinsi:-

  1. Walilia sana sana.
  • Kulia ni kipawa tuliopewa na Mungu kuonyesha hali ya kuvunjika moyo.
  • Kulia kunahitaji kufuatwa na maombi kali kali na imagine kwa Mungu- Nehemia 1:1-5.
  1. Hasira na jaribu ya mauaji.
  • Kaa sababu ya hasira na kilio chao, watu walimlaumu Daudi kwa yale yaliyotendeka.
  • Kwa hasira yao waliamua kumpiga Daudi make.
  • Kwa sababu ya haya yote, Daudi alikata tamaa.
  1. Daudi alijitia nguvu katika BWANA.
  • Katikati ya majaribu, dhihaka na masumbufu.
  • Katikati ya kulaumiwa na watu na kutishwa na kifo.
  • Daudi alijitia nguvu katika Bwana.
  • Baada ya dhiki, Daudi alipokea vitu vyote na jamaa zote waliochukua.
  • Leo unaweza kuwa katika shida ya uhusiano katika jamii, umekosa kazi na mapato, unatishwa pande zote, jipe moyo, kajitie nguvu jatika Bwana Mungu wako.
  • Marafiki wako wanapogeuka kuwa adui zako, jipe moyo.
  • Unapokosa usalama wa binafsi kwa sababu ya kuachwa na watu, jipe moyo katika BWANA Mungu wako.
  • Fahamu kuwa Yesu Kristo anakupenda hivyo sauti za watu, kuachwa na marafiki, kushushwa chini na marafiki na jamii, hakutakufanya kusikia maskini na kukataliwa.
  • Ukweli tulionao ndani ya Yesu Kristo ni kwamba tunapendwa, tumepokelewa, tumepewa nguvu, tuko salama, wenye haki mbele zake, dhamana na hatima yetu ni milele.
  • Lazima kuamua ni sauti gani tutakayo sikiliza.
  • Shetani anajua kuwa mtu aliye kata tamaa na kuvunjika moyo hawezi kusikia vyema.
  • Kuvunjika moyo kumewafanya wengi kuacha kanisa, ibada, shule, uhusiano, Mungu na kuacha vita vya maisha.
  • Jifundishe kulilia Mungu katika shida zako.
  • Jifundishe kuomba na kuweka shida zako msalabani.

JIFUNDISHE KUWA ASKARI MWEMA WA KRISTO.

  • Ilimpasa Daudi kuanza kumlilia Mungu na kusikia sauti yake.
  • Wana wa Israeli mle jangwani walikataa kusikiliza sauti ya Mungu.
  • Kuvunjika moyo ni chaguo letu, Daudi alielewa sana uwepo wa Mungu- Zaburi 16:11.
  • Daudi aliuliza kwa Bwana- 1 Sam.30:7-8.

WOKOVU WA MUNGU NA MSAADA WAKE.

  • Baadaye Daudi na watu wake waliwafuata na kuwashika Waamaleki, walinyakua vyote.
  • Daudi alitegemea ahadi ya Mungu.
  • Usiwache uchungu wa watu kukuongoza.

Hizi ndizo njia za kujitia nguvu katika BWANA.

  • Kumbuka na ungama ushindi aliokupa hapo awali.
  • Kumbuka na ungama ahadi za Mungu kwako.
  • Kumbuka na ungama ukuu wa Mungu na wema wake kwako.
  • Kumbuka Mungu wako ni nani, anatenda miujiza.
  • Kumbuka alichotendea wengine, atakutendea Mungu.
  • Imba sifa zake na kumwabudu kwa wimbo.

MWISHO.

  • Je, umevunjika moyo, umekata tamaa?
  • Kila mmoja wetu anapitia wakati wa shida na kuvunjika moyo.
  • Kumbuka furaha ya BWANA ndiyo nguvu yako- Nehemia 8:10.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *