MFULULIZO: WASHINDWA WAKUU KATIKA BIBLIA
SOMO: 2 MAMBO YA NYAKATI 26:1-23
Je, kuna shida gani kuwa na kiburi kidogo tu? Leo tunatazama mfalme Uzzia na jinsi na jinsi kiburi kilimfanya kupoteza maisha yake. Jinsi kiburi cha mfalme Uzzia kilichangia juu ya maisha ya nabii Isaya. Hebu tuone:-
JINA LAKE ALIITAA UZZIA- 2 Mambo ya Nyakati 26:3-5.
- Mfalme Uzzia alikuwa na fursa ya kuwa mfalme aliye mkuu zaidi katika historia ya Israeli na Yuda.
- Uzzia alikuwa miaka 16 alipopata kuwa mfalme.
- Uzzia alitawala Yerusalemu kwa miaka 52.
- Jina la mama yake ni Yekolia wa Yerusalemu.
- Uzzia alifanya yaliyo mema mbele za Mungu kama jinsi baba yake Amazia alivyokuwa.
- Uzzia alimtafuta Bwana Mungu wake kwa makini katika siku za kuhani mkuu Zakaria aliyemfunza Uzziajinsi ya kumwogopa na kumtii Mungu.
- Mungu alimpa Uzzia kufaulu sana sana.
- Uzzia alikuwa mjenzi mkuu, alijenga miji, alijenga minara jangwani, alichimba visima vingi katika nchi tambarare.
- Uzzia alikuwa na mifugo, ng’ombe, kondoo, ngamia, pia alikuwa mkulima hodari wa mizabibu juu ya milima na Karmeli.
- Uzzia alifaulu sana katika jeshi lake. Alikuwa na askari 307, 500 hodari zaidi.
- Uzzia alishindwa vita juu ya adui mkuu wa Israeli- Philisti.
- Uzia alijenga mashine kubwa za kutupa mishale na mawe kwa adui zake.
- Jeshi lake lilikuwa hodari zaidi ya majeshi ya Amoni na Misri.
- Amoni na Misri waliogopa Uzzia zaidi kiasi wakamlipa Uzzia fidia na fedha wasifanye vita.
KWA NINI UZZIA ALIPATA NGUVU NA KUFAULU SANA?
- Mungu wa mbinguni alimsaidia Uzzia-2 Mambo ya Nyakati 26:5.
- Uzzia angalikuwa mfalme aliye mkuu zaidi ya Daudi na Suleimani lakini mambo yake yalienda mrama- 2 Mambo ya Nyakati 26:16.
- Kiburi ni chukizo kwa Mungu wa mbinguni. Mithali 16:5- “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA hakika hatakosa adhabu.”
- 1 Petro 5:5- “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, nyinyi nyote jifungeni unyenyekevu, mate kuhudumiana kwa sababu Mungu huwapinga wenye KIBURI, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
- Mithali 16:8- “Je, kuna shida kujivunia kazi, gari, nyumba, jamii, watoto na mafanikio katika maisha?”
- Ikiwa tutajivunia, basi na iwe katika Yesu Kristo pekee kwa sababu hakuna ulicho nacho ambacho haukupewa na Mungu wa Mbinguni.
- Iwe ni watoto, mke, uhai, shamba, elimu, afya, urembo.
- Hakuna mtu aliyejijenga au kujiumba (self-made). Ikiwa ulijiumba basi utajisifu!!- Kumbukumbu 8:10-14.
- Tunaposahau Mungu ndiye mwenye yote mema, tuliyepokea- basi kiburi-sana Uzzia.
- Uzzia alipata nguvu zaidi na moyo wake ukapata kiburi.
UZZIA ALIONA KAZI YA KUTOA DHABIHU NI YAKE
- Lakini- ni makuhani peke yao walikuwa na fursa ya kuingia patakatifu pa Mungu.
- Kila mwana- Israeli alifahamu kazi ya ukuhani na kazi ya makuhani.
- Zakaria pia alikuwa amemfunza mfalme Uzzia tangu utotoni.
- Uzzia aliingia hekaluni pa Mungu kufanya kazi ya kuhani mkuu.
- Kuhani mkuu siku hizo alikuwa kuhani mkuu- Azaria. Yeye pamoja na makuhani (80) walimzuia Uzzia lakini askari wa Uzzia walikuwa na nguvu zaidi.
- Mungu hakupenda!! Hivi Mungu alimpiga Uzzia na tauni ya ukoma juu ya uso wake!! Kichwa chake kikawa cheupe kama pamba!! Kwa ukoma.
- Uzzia alijaa hofu, akakimbia kwenda kujificha mbali na watu mpaka kifo chake!!
- Kutoka siku hio, Uzzia hakuweza kwenda hekaluni, ofisini, hakuweza kuomba tena!!
- Mwanaye Jothamu alichukua mahali pa babaye- Uzzia- KIBURI KIBURI.
- Je, watu wanao kiburi hiki leo? Ndio.
- Wengine hawataki kwenda kanisa kwa kustawi.
- Yesu Kristo alikufa kwa dhambi zetu, pia Kristo aliifia kanisa lake- Waefeso 5:25.
- Lakini ikiwa tunampenda Kristo, ni lazima kwenda kanisa.
- Ikiwa mtu hapendi kanisa, basi hampendi Kristo.
- Ikiwa unampenda Kristo, basi utapenda kanisa Lake na kulitumikia.
- Unapokuja kanisa, pia tumika, tumika kwa injili yake.
JE, WAPI MAMBO YALE MENGINE YA UZZIA ALIYOYAANDIKA ISAYA MWANA WA AMOZI?- Mambo ya Nyakati 26:22.
“Basi Mambo yote ya Uzzia yaliyosalia ya kwanza na ya mwisho, aliyaandika Isaya mwana wa Amozi.”
- Wapi Mambo haya yaliyosalia na kuandikaa na Isaya mwana wa Amozi?
- Jibu liko katika Isaya 6.
- Isaya kabla ya (Isaya 6) alikuwa amejaa Uzzia lakini Uzzia alipokufa, Isaya alimwona Mungu.
- Mwaka Uzia alipokufa, Isaya alisikia mwito mkuu wa kumhubiri Yesu Kristo.
- Isaya aliona hekalu limejaa Mungu na utukufu wake.
- Tunaweza kumtumikia mwanadamu, tukasahau Mungu.
- Leo, amua ni nani utakayemtumikia, ni Uzzia au Yehova? Dhehebu au Kristo?
MWISHO
- Hapo zamani za kale (1014 AD) palikuwa na mfalme mmoja wa Uigereza (England) kwa jina Canute (Kanute). Alikuwa mfalme mkuu sana na mcha Mungu. Kama mfalme Canute alitembelewa na watu waliomsifu sana. Lakini Canute hakuwa kama mfalme Uzzia- Kiburi.
Siku moja mfalme Canute aliamrisha kiti chake cha Enzi kupelekwa ufuo wa bahari. Alipoketi mle baharini, mfalme Canute aliamrisha bahari kutulia na mawimbi ya bahari kutomjia miguuni. Lakini hata kwa kuikemea bahari na mawimbi yake, bahari haikutii amri ya mfalme Canute!!
- Mfalme Canute alitoka baharini akaenda kanisa, akatoa taji yake akaiweka msalabani. Hakuivaa tena maisha yake yote.
- Pengine wewe leo utahitaji kuamua kutoa taji zako zote na kumpa Yesu Kristo na kumwacha Kristo apate njia katika maisha yako- (“Have your way my Lord, have your way.)
- Pengine bado kuokoka, pengine bado utasema kama Isaya, “Niko hapa nitume BWANA.”
- Pengine unahitaji kujitoa kamilifu kaa Mungu wako leo- MADHABAHU NI WAZI.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
