MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO.
SOMO: I WAKORINTHO 3:10-15.
Tunapoendelea na mafundisho yetu juu ya kuja kwa Yesu Kristo duniani kwa mara ya pili , tunafikia sherehe kuu itakayo fanyika huko mbinguni . Sherehe hii itafanyika wakati dhiki kuu inaendelea hapa duniani.
Kanisa litakapo nyakuliwa mbinguni (Rapture) taharuki kuu itafanyika hapa duniani, taharuki hii inaitwa dhiki kuu hau thabu zake yakobo. Dhiki kuu inapoendelea duniani, Kuna mambo mawili yatakayo endelea mle mbinguni :
- Hukumu mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo-(Judgement sit of Christ)
- Karamu ya Arusi ya mwana kondoo-(The marriage supper of the lamb)
Leo twatazama jambo la kwanza , yaani kiti cha hukumu cha Kristo (BEMA)-(II Wakorintho 5:10 , Warumi 14:10-12)
Mistari hii yote pamoja na (I Wakorintho 3:10-15), inaongea juu ya jambo Moja tu; Kiti cha hukumu cha Kristo (BEMA SEAT).
Kila Mwana wa Mungu lazima kutoa hesabu ya kazi yake tangu kuokoka. Hesabu ya kazi zetu litatolewa mbele ya Bwana Yesu Kristo. Leo wacha Mungu apate kuongea nawe. Mambo matatu yatafanyika mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Hebu tuone:
SIKU HII ITAKUWA SIKU YA KUTAMBUA JINSI ULIVYO-( I Wakorintho 3:10-13)
- Mtume Paulo anaeleza kwamba maisha ya Mkristo ni kama jinsi mjengo wa nyumba .
- Mtume Paulo anaeleza kwamba yeye tayari amesha weka msingi wake imara lakini sasa ni jukumu yetu kujenga juu ya ule msingi imara .
- Mtume Paulo anaeleza mjengo huu ni kwa wale wameokoka pekee.
- Hivyo kama haujengi kutoka kwa imani yako ndani ya Yesu Kristo, basi wewe hautakuwa katika hukumu hio.
- Ikiwa wewe hautakuwa katika hukumu hii basi utakuwa katika dhiki kuu, baadaye, utasimama mbele ya kiti kikubwa cheupe cha hukumu, kuingia jehanamu ya milele na milele.
- Kila mtu ni lazima kuwa tayari kukutana na Mungu wake kwa wema hau kwa ubaya !!
- Kila siku kila mmoja wetu yuko karibu na milele, katika mbinguni au jihanamu.
- Je, ni kitu gani kitatambulika juu yako siku hio?
v.10- njia na mbinu zetu zitajulikana-(our methods-motives).
- Paulo anaeleza kwamba jinsi tunavyo jenga juu ya ule msingi ni jambo la maana sana.
- Kile unajenga saa hii kitapita katika moto wa Mungu.
- Ulipookoka, cheki, Yesu Kristo alikuweka juu ya msingi imara, yaani YESU KRISTO.
- Tangu kuokoka ulianza kujenga maisha.
- Maisha unayojenga eitha ni kwa utukufu wa Mungu hau utukufu wako binafsi.
- Tutakaposimama mbele zake tutajibu tulimwishia nani na kumjengea nani?
- Katika wakati wa Mtume Paulo palikuwa na mahali katika kila mji paitwao BEMA, hau kiti cha hukumu. Hii ulikuwa ni jukwaa ( platform) katikati ya mji hapa matangazo ya mji ulifanyika, hukumu na pia zawadi zilipeanwa kwa washindi.
- Ni katika BEMA zawadi za ushindi wa michezo ya Ugiriki zilifanyika .
- Hapa ndipo taji za ushindi zilipeanwa kwa kila mshindi, hapa ndipo walioshindwa walionekana kwa aibu.
- Kuna mambo mawili ambayo haitatajwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo-
- Wokovu – salvation.
Mambo ya wokovu wako ilimalizika pale msalabani – ikiwa umeokoka, basi umeokoka milele. Hakuna mtu asiyeokoka atasimama mbele ya BEMA-(Warumi 8:1)
2. Dhambi-sin.
- Dhambi zako na zangu Yesu Kristo alilipa pale msalabani, deni ya dhambi imelipwa kamilifu (Yohana 19:30; II Wakorintho 5:21).
- Sisi ni mawakili (I Petro 4:10, I Wakorintho 4:2)
Materials tuliojenga nayo itajulikana-(v.12 )
Kuna Material nzuri ya kudumu.
- Dhahabu, Fedha, Mawe ya dhamani
- Hizi tatu maanake ni vitu vya dhamani nzuri vitu ngumu kupata.
- Hizi ni vitu vinaostahimili moto,
- Jenga kwa dhamani, kazi ya Bwana si kazi hoihoi.
Vitu rahisi, vitu vya bure.
Miti, majani na nyasi.
- Hizi ni vitu vya rahisi, bure, sura mbaya.
- Mungu ni wa thamani sana, kazi yake ni ya thamani zaidi .
- Je, tunatumia wakati, mamlaka, karama, pesa namna gani?
Huduma zetu, zita julikana na Kila mtu-(V.13).
- Je, lengo lako kutumika ni nini? Kuonekana, kujisifu, kujipa utukufu ?
ITAKUA NI SIKU YA FURAHA KUU-( V. 14)
Kazi zote zitapitia moto, tutalipwa kwa mabaki.
Ahadi – tutalipwa kwa mabaki ya moto.
- Taji tano ziko kwa waaminifu wa Mungu.
Taji isioweza kuaribika-(I Wakorintho 9:25)(Kwa uaminifu katika kazi )
- Taji ya uzima.
- Kwa walioshinda majaribu (Yakobo 1:12
2.Taji ya furaha.
Kwa wote wanaomshuhudia Kristo-(I Wathesalonike 2:19)
3.Taji ya haki – wanaomngojea Kristo kwa hamu (II Timotheo 4:8)
4. Tajibya utukufu – kwa watumishi wanaochunga kundi ya Mungu -(I Petro 5:4)
- Kila jambo njema lililofanywa kwa utukufu wa Yesu Kristo litalipwa-(Mathayo 25:34-10; Marko 8:41).
- Kwa nini tupewe taji hizi? (Ufunuo 4:9-11)
ITAKUA SIKU YA HUZUNI KUU-( V.15)
Kazi za wengine zitachomeka zote, itakua siku ya kilio.
- Hakuna siku ya kilio.
- Itakua siku ya kupoteza yote – Aibu.
- Ahadi tunayopewa.
- Watakao kosa taji, bado wataokolewa. Lakini kama kupitia moto !
- Wataokoka lakini watakaa maskini mbinguni.
MWISHO:
- Kuna njia mbili ya kuaribu nyumba nzuri – Msingi mbaya, na material bure.
- Je, umejenga juu ya msingi gani? ( Mathayo 7:24-27)
- Je, unajenga na material gani?
- Je, umeokoka, Je utakuwa katika karamu ya kutukuzwa mbinguni?
- Siku hio inakuja- Amen.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
