Series Swahili Service

MIAKA ELFU YA MBINGU JUU YA DUNIA.

MFULULIZO : KURUDI KWA YESU KRISTO

SOMO : UFUNUO 20:1-15

 

Ufunuo mlango wa 20 unataja kipindi cha miaka 1,000 mara sita (6) Ufunuo 20:2-7. Kipindi hiki cha wakati ndicho kinaitwa ‘millenium.’ ‘Millenium’ni neno la Latin maanake 1,000 ya miaka. Kwa miaka hii 1,000 Yesu kristo mwenyewe atatawala dunia hii-utawala wa Yesu Kristo utaleta wakati na enzi ya amani, ustawi na haki jinsi dunia haijaweza kuona tangu mwanadamu alivyofanya dhambi bustani Edeni.

Mpaka sasa tumeona na kujifundisha juu ya-

  1. Kunyakuliwa (rapture).
  2. Dhiki kuu.
  3. Kiti cha hukumu cha Kristo (BEMA).
  4. Harusi ya Mwana kondoo
  5. Kurudi kwa Yesu Kristo duniani.

Leo tunatazama miaka 1,000 ya utawala wa Kristo duniani, yaani millenium.

MWOKOZI YESU KRISTO WAKATI WA MILLENIUM-Ufunuo 20:4-6.

  • Je, Yesu Kristo atakuwa anafanya nini wakati huu?
  1. Atakuwa anaongoza.
  • Sasa Kristo ataongoza na kumiliki kiti cha enzi cha baba yake Daudi-Isaya 9:6-7.
  • Kristo ataongoza dunia kwa nguvu, haki na utukufu.
  • Utawala wake utaleta amani, ustawi na fanaka zaidi. Utawala wake utakuwa pamoja na kuleta haki, utakatifu na utukufu.
  • Viongozi wa ulimwengu huu wameahidi mambo mengi lakini kwa sababu wao wametawaliwa na ubinafsi, ufisadi, ukabila na chuki.
  • Lakini utawala wa Yesu Kristo utakuwa wa furaha, amani, upendo, utakatifu, haki na ukamilifu.
  1. Yesu Kristo atatawala.
  • Kristo atatawala na fimbo ya chuma-Ufunuo 19:15.
  • Atatawala jamii yote ya dunia hii.
  • Wasiomtii Kristo watakabidhiwa kwa haraka sana.
  • Uasi hautakubalika katika ufalme wa Kristo.
  1. Yesu Kristo atapokea utukufu.
  • Watu wa kila kabila, jamii na taifa watasujudu na kumwabudu Kristo pekee-Isaya 40:5.
  • Utakuwa wakati wa Yesu Kristo kupokea utukufu na sifa.

SHETANI WAKATI WA MILLENIUM-Ufunuo 20:1-3, 7-10.

  1. Shetani atakuwa jela-Vs. 1-3.
  • Kwa miaka 1,000 shetani na pepo zake hawatazuia kazi ya Mungu!!
  • Hakutakuwa na majaribu ya shetani.
  • Leo hii shetani ndiye mfalme wa dunia hii-2 Wakorintho 4:4.
  • Kazi ya shetani ni kupinga mpango wa Mungu duniani.
  • Ona majina anayopewa Vs. 2, joka, yule nyoka wa zamani, ibilisi, shetani.
  • Siku hio na wakati huo shetani hatakuwako duniani.
  • Hebu fikiri dunia bila shetani, Kristo akitawala bila shetani-Utukufu-Haleluya!
  1. Shetani atahukumiwa-Vs. 7-10.
  • Hapo Biblia inaeleza kwamba baada ya ile miaka 1,000, shetani atatolewa jela na kurudi tena duniani.
  • Shetani atakusanya jeshi kubwa zaidi.
  • Shetani na jeshi lake watauvamia mji wa Mungu (Yerusalemu) mahali Kristo anatawala. Hapa shetani anataka kuipindua serikali ya Kristo!!
  • Hukumu itashuka kutoka mbinguni, moto, wote waliomfuata shetani na jeshi lake watauliwa wote.
  • Shetani atatupwa katika ziwa la moto na kiberiti-milele na hata milele.
  • Tunashangaa sana!! Hata Kristo akitawala kwa haki, upendo, utakatifu, mwanadamu atachagua kwenda na shetani.
  • Haijalishi-moyo wa mwanadamu ni dhaifu na mdanganyifu. Haijalishi upendo wa Mungu juu ya mwanadamu-mwanadamu anahitaji wokovu-kwa neema.
  • Mungu amejaribu kumpenda na kuokoa mwanadamu lakini mwanadamu ameasi!!
  • Ona vizazi na nyakati (dispensations).
  1. Nyakati za bila lawama (age of innocence)-Mwanzo 3. Matokeo –uasi.
  2. Nyakati za dhamiri (age of conscience)-Mwanzo 5-6. Matokeo-ufisadi duniani kote.
  3. Nyakati za mwanadamu kujitawala (human government/self determination)-Mwanzo 11. Matokeo-ibada ya shetani-Babeli.
  4. Wakati wa ahadi (age of promise)-Mwanzo 12; Kutoka 1. Matokeo-utumwa wa Misri.
  5. Nyakati za sheria ( the age of law)-Kutoka 2; Mathayo 27. Matokeo-Mwanadamu alimuua muumba wake-msalabani.
  6. Nyakati za kanisa (the age of the church). Matendo 1. Matokeo-maasi duniani kote-kanisa litaasi Mungu duniani kote (worldwide apostasy).
  7. Nyakati za dhiki kuu (the great tribulation)-Ufunuo 19. Matokeo-vita vya armageddon.
  8. Nyakati za millenuim (miaka 1,000)-Ufunuo 20. Matokeo-mwanadamu na shetani watajaribu kupindua serekali ya Kristo.
  • Moyo na nia ya mwanadamu ni kuasi. Hakuna chema katika mwanadamu-Warumi 3:10-11.
  • Tumaini pekee ya mwanadamu ni kumjia Kristo na kuokoka.
  • Yesu Kristo anabadilisha maisha na mwelekeo.
  • Je, leo unasimama wapi-je, umeokoka?

WATAKATIFU WAKATI WA MILLENIUM-Vs. 4-6.

  • Je, watakatifu watakuwa wakifanya nini wakati wa millenium?
  1. Watatawala pamoja na Kristo-Vs. 4.
  • Tutatawala pamoja na Yesu Kristo-2 Tim. 2:12-13; 1 Peter 5:1.
  1. Watafufuliwa-Vs. 4.
  • Katika mwanzo wa millenium watakatifu wote tangu Agano la Kale na wote waliokufa wakiwa katika Yesu Kristo katika dhiki kuu watafufuliwa miili yao.
  • Hebu fikiri watakatifu wa Agano la Kale waliokufa katika imani, walitazamia siku hii-Yohana 8:56.
  1. Watapokelewa-Vs. 4.
  • Wale watakataa chapa ya mpinga Kristo, Wayahudi na Wayunani katika ufalme wa Mungu-Mathayo 25:31-46.
  • Imani ndani ya Yesu Kristo pekee ndio njia pekee ya kuingia mbinguni. (Imani pekee, kwa neema pekee, katika Yesu Kristo pekee, kwa utukufu wake pekee).
  • Wokovu ni katika Yesu Kristo pekee.

WENYE DHAMBI WAKATI WA MILLENIUM.

  • Je, kutakuwa na wenye dhambi wakati wa millenium? Ndiyo.
  • Kutakuwa na wale watazaliwa wakati wa millenium (1,000 miaka).
  • Unaona kwamba kuna Wayahudi na Wayunanai watakao ingia katika millenium kutoka kwa dhiki kuu, wakiwa katika miili yao (mwili na damu).
  • Hawa watu wameokoka lakini watoto watakao wazaa watazaliwa katika mwili hivyo wanazaliwa wenye dhambi, wamepotea wanao asili ya dhambi-wanahitaji kuokoka!!
  1. Uhusiano wao na Mwokozi.
  • Kwa sababu shetani yuko jela, mwenye dhambi atakuwa kama mwokovu!!
  • Lakini bado anahitaji kuokoka.
  1. Watalazimishwa kuabudu sahihi.
  • Kila mtu lazima atapiga magoti mbele ya Yesu Kristo.
  • Kila mmoja atakiri Yesu Kristo ni Bwana-lakini bila kumpenda Kristo ni bure!!
  • Kutoka nje hakutakuwa na tofauti lakini kutoka ndani ya mioyo kutakuwa tofauti sana.
  1. Watalazimishwa kutembea sahihi.
  • Kutakuwa na kutii hata bila kumpenda Yesu Kristo kwa mioyo dhati.
  • Wakati shetani atafunguliwa kwa muda mfupi-hawa watu watadanganywa na shetani-Warumi 2:4.
  • Watapata fursa ya kumchagua Yesu Kristo kama Mwokozi wao au kumkataa-Yohana 14:6.

UMMA WAKATI WA MILLENIUM (Society)

  • Wakati wa millenium (miaka 1,000) kutakuwa na mabadiliko mengi.
  1. Amani-hakuna vita popote duniani!!
  • Maendeleo tele.
  • Utakuwa wakati wa maendeleo na amani na binafsi-na dunia yote-Isaya 2:4; 9:4-7: 32:17-18; 33:5-6; 60:18.
  1. Furaha-furaha ya milele-Isaya 12:3-6; 14:7-8.
  2. Utakatifu-ufalme wa Mungu ni mtakatifu-Isaya 31:6-7; 35:8-9; Eze. 36:24-31.
  3. Utukufu-ufalme wa Mungu utakuwa dhahiri-Isaya 4:2; 35:2; 40:5; 60:1-9.
  4. Faraja-Kristo atashughulikia kila hitaji-Isa. 12:1-2.
  5. Haki-Haki kwa kila mtu itatendeka-Isa. 9:7; 32:16; 42:1-4; 65:21-23.
  6. Ufahamu kamili-hakutakuwa na tashwishwi-Isaya 11:1-2; 41:19-20; 54:13; Hababuki 2:14.
  7. Hakuna laana tena-laana zote zitatolewa-Isaya 11:6-9; 65:25.
  8. Hakuna magonjwa-hakuna kifo-Isaya 33:24; Yeremia 30:17; 33:6.
  9. Hakuna ulemavu wowote-Isaya 29:17-19.
  10. Ulinzi utakuwa wakutosha, hakuna utoto na ujinga.
  11. Utauwa na ufanisi utaleta wingi wa kila kitu chema-Isaya 35:1-2; 30:23-25; Yeremia 31:5; Yoeli 2:21-27; Amosi 9:13-14.
  • Lakini bado tutangojea hali yetu ya mwisho (final state) mbinguni milele na milele.

MWISHO

  • Leo, unapompokea Yesu Kristo, utawala wake ndani yako unaanza.
  • Je, kuna wakati ulimpokea Kristo kabisa ndani ya maisha yako?
  • Sasa ni wakati wako-Haleluya-Amina.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *