MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA.
SOMO: YOHANA 6:15-21.
Maisha ni mfululizo wa changamoto na shida. Kila wakati pengine uko katika bonde la changamoto hau uko karibu kuingia hau unatoka. Sababu ni kwamba Mungu anakujenga tabia yako, kwa maana kwa Mungu tabia ni maana zaidi kuliko starehe.
Mungu anapenda zaidi utakatifu wako kuliko furaha yako.
Lengo la Mungu kwetu ni kukua katika tabia na kufanana na Yesu Kristo.
Maisha ni kama jinsi reli na line zake mbili, upande moja mema upande mwingine mabaya.
Katika somo letu leo, Yesu Kristo alikuwa amemaliza siku yenye shughuli nyingi mno za huduma nyingi.
Yesu Kristo alikuja kufanya mambo matatu-
- Kuhubiri ufalme wa mbinguni.
- Kufundisha juu ya ufalme wa Mungu.
- Kuwaponya wote, udhaifu na kuwaweka huru walioonewa na shetani-Mathayo 4:23.
Yesu Kristo alikuwa amechoka kweli kweli. Hivyo Kristo aliwaamuru wanafunzi wake wakwee kwenda upande mwingine wa bahari ya Galilaya, lakini Yesu Kristo hakuingia katika chombo na wao.
Walipokuwa katikati ya bahari, bahari ilichafuka sana, dhoruba kuu ikawapata.
Dhoruba ilikuwa kuu kiasi Mathayo anasema ilikuwa kama tetemeko ya ardhi (Sunami). Luka naye anasema dhoruba ilikuwa kubwa kiasi maji yaliingia katika kile chombo.
Hivyo, dhoruba ilikuwa kubwa, maji yakapiga kile chombo, maji yakaingia ndani, chombo kikawa katika kuzama baharini!!
Biblia inasema watu (Wayahudi) walikuwa wanataka kumlazimisha Yesu kuwa mfalme wao (Yohana 6:15).
Wanafunzi wa Yesu walishuka kwenda baharini (6:17) naye Yesu Kristo alipanda mlimani peke yake-6:16.
Wanafunzi tayari waliingia baharini, lakini baada ya maili tatu hau nne (5-6km) dhoruba iliwapata wao (6:19).
Katika dhoruba ndio walimwona Yesu Kristo akitembea juu ya maji akiwajia, wakaogopa sana (6:20).
Yesu Kristo alinena na wao na kuwaambia “ni mimi, msiogope”-6:21 walipokea chomboni kwza furaha, wakafika walipokuwa wanaenda.
Kisa hiki chaonyesha kwamba kuna wakati shida zinakuja ndani ya maisha yetu.
Wakati wa dhoruba za maisha “Je, Yesu Kristo yuko wapi?” kunao kweli tatu juu ya dhoruba za maisha. Hebu tutazame:-
KWANZA, DHORUBA ZINAKUJA KAMA SEHEMU YA KILA MTU.
- Ukweli wa mambo ni kwamba, hakuna yeyote atapitia maisha haya bila dhoruba.
- Kuna dhoruba za ugonjwa-haraka hau sugu.
- Kuna dhoruba za mauti na kifo-mauti ya mtu aliye karibu nawe.
- Kuna dhoruba za kukataliwa-kutengana hau kuachana (taraka).
- Kuna dhoruba za kuingiliwa na watu-watu wengine watakushambulia na kukuzoa.
- Kuna dhoruba za matatizo ya jamii.
- Kuna dhoruba za kukosa kazi, fedha na ajira.
- Dhoruba zingine zinatujia kwa sababu ya ujinga wetu, dhambi, uamuzi m’baya, watu.
- Hivyo dhoruba zinawajia watu wote bila shaka.
DHORUBA ZINAKUJA HATA TUNAPOKUWA KATIKATI YA MAPENZI YA MUNGU.
- Huenda sasa hivi uko katika dhoruba na unajiuliza “Bwana nilifanya nini niweza kuwa katika hii dhoruba?”
- Huenda hakuna dhambi wala makosa umefanya.
- Pengine ulifikiri mtu akiokoka, basi maisha yatakuwa tambarale.
- Yesu Kristo hakutufundisha kwamba tunapookoka maisha yatakuwa tambarale!!
- Yesu Kristo alifundisha “katika ulimwengu huu dhiki za kila haina zitakuwako.
- Hawa wanafunzi wa Yesu Kristo walikuwa katika mapenzi ya Mungu!! Huduma.
- Bwana alikuwa amewatuma na wakatii sauti yake.
- Hivyo, unawezakuwa katika mapenzi ya Mungu na uwe katika dhoruba za maisha-Mathayo 14:22.
- Bila dhoruba katika maisha hatuwezi kuona nguvu za Mungu wetu.
- Dhoruba zunakuja kujaribu imani yetu-Yakobo 1:2-3.
DHORUBA MAANAKE SI ISHARA YA KUTOKUWAKO KWA MUNGU-Yohana 6:16-21.
- Bwana anayajua yote, yuko kila mahali.
- Bwana Yesu Kristo anaona.
- Dhoruba haziwezi kumkwepa Mwokozi.
- Mwokozi alikuwa akiwatazama kwa umbali!!
- Yesu Kristo anajali maisha yetu.
- Kujali kwake kulimvuta kwao.
- Yesu alipokuwa juu mlimani aliona dhoruba, chombo na kazi nzito walikuwa nayo.
- Mwishowe, Kristo aliwajia lakini kwa nini alichelewa?-Yohana 11:21 utukufu wa Mungu.
- Mungu hakutuahidi kwamba dhiki, dhoruba na shida hazitakuweko lakini aliahidi uwepo wake-Waebrania 13:5; Mathayo 28:19-20.
- Petro anaeleza kwamba tunapokuwa katika dhoruba za maisha kumpa Yesu Kristo fedheha zetu zote-1 Petro 5:7.
MWISHO
- Je, unapitia dhoruba katika maisha sasa?
- Basi, elewa Bwana anaona, anakujali, anakuja kwako sasa.
- Je, wewe ni mgonjwa? Leo uponyaji upo.
- Je, unataka kuokoka? Mjie sasa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025