SOMO: WAFILIPI 3:13-14.
Katika siku hizi za mwisho, watu wamebeba na kubebeshwa mizigo zaidi. Je, utafanya nini? Je, utaongea na pasta wako, rafiki yako au utamwendea mshauri wa kulipa?
Katika Wafilipi 3:13-14, Mtume Paulo anatueleza jinsi ya kutwika mizigo yetu nzito kwa Mungu. Je, nitafanya nini na mizigo yangu nzito?
SAHAU NA SAMEHE YALIYO NYUMA-Vs. 13.
- Je, utafanya nini na mizigo yako?
- Sahau na samehe yaliyopita, makosa, kuanguka, mikosi ya maisha.
- Sahau na samehea waliokutesa, waliokudanganya.
- Sahau na samehea waliokupora mali na kukusumbua.
- Yusufu alisamehea ndugu zake. Huko Misri alisahau shimo waliomtupa, alisahau jinsi walimuuza kwa Waishmaeli.
- Yusufu alisahau mke wa Potiphah, alisamehea marafiki wake waliomwahidi kumtendea mema, lakini wakamsahau-Mwanzo 50:18-26.
- Nawe sahau na usamehe yaliyopita.
CHUCHUMULIA YALIO MBELE.
- Je, utafanya nini na mizigo yako inayokulemea?
- Chuchumilia yalio mbele yako, usifikiri juu ya yale yamepita, usiyaongee, usiyaongee mbele za watu kama hadithi ya kukariri.
- Katika maisha haya kunao mambo mengi mbele yako, yakufanya, ya kuona, ya kufurahia.
- Tazama ya mbele-ona mbele yako.
- Watu wakikuletea yalio nyuma yako waeleze kwamba wewe ulienda mbele (I have moved on)-Wafilipi 3:7-12.
KAZA MWENDO-MTAZAME KRISTO-Vs. 14.
- Je, utafanya nini na mizigo yako ya kale?
- Mtazame Kristo, wacha Kristo awe katika maisha, roho, nyumba yako na tabia yako-Vs. 14.
- Mtazame Kristo, chuchumilia yalio mbele yako.
- Kuna yale yalifanyika katika maisha ya hawali lakini yakubali, yasahau, enda mbele (Accept, Adjust, Advance-A.A.A).
- Mtazame Mwokozi anapoongoza.
MWISHO
- Je, utasahau, utasamehe, utaenda mbele?
- Mbele kunao Yesu Kristo, kunao makuu usiyoyafahamu sasa.
- Muulize Yesu Kristo ni yapi mapya kila siku ya maisha.
- Toa mzigo wako kwa Yesu Kristo leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025