Swahili Service

MAKOSA KATIKA HATIMA

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: MHUBIRI 10:5-7; 2 WAFALME 4:1-7

 

Makosa ya hatima yanaonekana kila mahali leo. Unapotazama maisha yako na kuona kwamba mahali na hali yako sio mahali ungalikuwa, basi makosa yaliingia katika maisha yako.

Unapoona mpaka sasa ungali unanyenyekea shetani na umeokoka-makosa.

Ikiwa mpaka leo unakopa fedha, chakula, badala yako kukopesha mataifa ni makosa katika hatima yako.

Unapoona maisha yako unaishi katika mabonde bila kuinuka ni makosa ya hatima.

Kisa hiki katika 2 Wafalme, mjane wa mtumishi wa Mungu na watoto wake wawili ni kisa cha kuuzunisha sana.

Mume wake alipokuwa hai aliishi katika deni, maisha yake yote aliishi katika deni!! Maisha ya umaskini.

Huyu nabii, mtumishi wa Yehova aliishi maisha ya umaskini, ufukara.

Katika maisha na katika mauti alikuwa mwenye deni.

Sasa kizazi chake pili kimeingia katika shida zake za madeni. Kukopa ni utumwa zaidi.

Mtego wa umaskini  unakuwa na hatua nne:-ujinga, magonjwa, kukosa hajira na kutawaliwa vibaya (ignorance, diseases, lack of livelihood, bad governance).

Ukiwa maskini unatawaliwa vibaya na watu. Huyu mjane angetawaliwa vibaya na wanaume.

Katika shida zake alikumbuka mtumishi wa Mungu Elisha, akamwendea. Makosa yake yalirekebishwa. Hebu tuone alichofanya kusaahisha makosa yake na ya mume wake marehemu.

Alifuata hatua saba-hizi ni kanuni za kufuata na kujiokoa kutoka utumwa wa maisha ya deni:-

  1. Alipata maono ya kujiokoa.
  • Alikataa kukaa nyumbani, alikataa manunguniko, alikataa kumlaumu Mungu-Mathayo 11:28.
  • Alimlilia mtumishi wa Mungu.
  • Alimkimbilia mtu anayefaa-wengi wanawakimbilia watu ovyo.
  • Mjane alikimbia kwa Elisha nabii wa Mungu.
  1. Alijitambua (she discovered herself).
  • Aliona karama zake, alijitambua kwamba anaweza kujisemea kwa mtu wa Mungu.
  • Kila mtu anao kipawa, karama ya kumwezesha kuwa mtu mkuu.
  • Kunao ukuu ndani ya kila mtu. Kipawa chako kitakutengenezea njia.
  • Kila mmoja wetu lazima kutambua kipawa na karama uliyopewa na Mungu.
  • Utakachooona ndani yako, ulichopewa na Mungu ndicho kitakupeleka mbali.
  • Yusufu alitambua karama ya kutafsiri ndoto-Mwanzo 39:2.
  • Daudi alitambua karama kucheza kinubi alipokuwa malishoni. Karama yake ilimpeleka mbele ya mfalme.
  • Wewe na mimi tunao kipawa au karama ya kuipa dunia hii, kipawa chako kitakutengezea njia.
  • Lakini omba Mungu akufunulie siri ya maisha yako.
  1. Tambua mahitaji yako (identify your needs).
  • Huyu mwanamke mjane alitambua mahitaji yake na ya watoto wake.
  • Elisha alipomuuliza shida yake alisema mara moja.
  • Kipofu Batimayo alipoulizwa shida yake alisema mara-Marko 10:51.
  • Itaji yako ni nini?
  1. Uwe mwema kwa kila mtu (Be good to people).
  • Elisha nabii alimwambia huyu mjane kuazima vyombo kutoka kwa majirani.
  • Kila mtu katika kijiji alimfahamu huyu dada.
  • Alikuwa mwanamke wa tabia nzuri.
  • Huwezi kupanda maisha peke yako, unahitaji watu.
  • Uwe mtu wa kuwasaidia watu, wape watu heshima zao.
  • Tabitha (Dorcas) alikuwa na heshima kwa kila mtu-Matendo 6:36.
  • Uwe mwema kwa Mungu-Toa sadaka na zaka zako zote kwa Mungu-Mithali 11:24-25.
  1. Mimina chupa ya mafuta yako (empty your container).
  • Mafuta kidogo yalikuwa ndani ya chupa, Elisha alimwambia aazime chungu.
  • Kila kitu ambacho hakitoshi ni mbegu.
  • Usile mbegu yako, tawanya, mwaga, panda ungojee mavuno-Mhubiri 11:4.
  • Mbegu haiwezi kusibisha, chupa ndogo pia.
  1. Funga mlango wako (shut your door).
  • Funga kinywa chako. Elisha alimshauri yule mjane funga mlango wa nyumba yako-Mithali 18:21.
  • Angalia sana maneno yako. Usipo nena shetani hawezi akakusikia. Fungua vitu lakini kinywa chako funga mpaka muujiza wako ukamilike.
  1. Endelea kumimina mpaka vyombo vyote (don’t stop).
  • Mafuta yalikatika vyombo vilivyojaa.
  • Huyu mwanamke mjane alisaaisha makosa ya hatima yake na nyumba yake kwa imani.
  • Hatima yake na watoto wake iliimarika kabisa.

MWISHO

  • Je, una nini katika nyumba yako?
  • Tumia ulichonacho katika nyumba na maisha yako.
  • Mjane alijitoa katika utumwa wa deni, kupitia biashara ya mafuta.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *