Swahili Service

NDOTO NA TUMANINI ZAKO ZINAPOKUFA

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: 2 WAFALME 4:8-37

 

Hiki ni kisa cha mama aliyekuwa tasa kwa muda mrefu. Baadaye akapata muujiza na kujaliwa mtoto wa kiume. Lakini baada ya miaka yule mtoto akafa. Lakini huyu mama akashikilia imani mpaka Mungu akamfufua yule mtoto. Huyu mama wa huko Shunemu alikuwa mkuu kwa imani na ukarimu wake. Hebu tuone:-

JE, UKUU WAKE ULITOKA WAPI?

  1. Alikuwa mwanamke wa ukarimu mkuu-Vs. 8.
  • Alianza kumpa chakula Elisha na Gehazi hata kabla hajawafahamu kabisa.
  • Alimua kumjengea mtumishi wa Mungu chumba cha wageni juu ya nyumba yao.
  • Alifuata desturi na kanuni ya kuwakaribisha wageni.
  • Ibrahimu alikuwa na desturi ya ukarimu, aliwakaribisha wageni kumbe ni Mungu na malaika zake-Mwanzo 18:1-15.
  • Tunahitaji kuwafadhili na kuwakaribisha wageni kama desturi-Waebrania 13:2
  1. Alikuwa mwanamke mkarimu na Matendo mema-Vs. 9-10.
  • Huyu mwanamke kwa ruhusa ya mumewe alijenga chumba cha wageni kwa ajili ya Elisha na mtumishi wake Gehazi.
  • Unam’barikia Mungu kwa kuwatumikia watumishi wa Mungu.
  1. Alikuwa mwanamke wa kubarikiwa na Mungu.
  • Elisha alivutiwa sana kiasi kutafuta kum’bariki huyu mwanamke kwa ukarimu wake.
  • Huyu mwanamke Mshunemu alizidisha ukarimu kwa upendo aliowaonyesha Elisha na Gehazi.
  • Kweli, hatuwezi kutoa zaidi kuliko Mungu wetu.
  • Unapotafuta njia ya kum’barimi Mungu wako, basi uwe na hakika baraka zitakurudia wewe.
  1. Alikuwa mtoaji wala si mchukuaji.
  • Elisha alipomwambia mwanamke Mshunemu atamtafutia kazi ya cheo kwa mfalme hau kwa jemedari mkuu, alikataa.
  • Alisema yeye hatafuti kibali kutoka kwa wakuu wa nchi.
  • Alikuwa na hali ya kutosheka na mahali pake na kuwatumikia watu wa kawaida.
  1. Alikubali hali ya utasa.
  • Katika maisha yake yote alipigana na utasa, kukosa mtoto.
  • Kwa miaka mingi alijaribu kushika mimba akakosa.
  • Miaka 5, 10, 15, 20, 30 ilipita bila kupata mimba.
  • Baada ya miaka, tumaini lake liliyeyuka kabisa, alikubali kwamba hakuna mtoto atakayezaliwa.
  • Nguvu zake zote alizielekeza kwa mambo mengine kama jinsi kuwasaidia watu.
  • Alikubali, alijipanga na kuendelea na maisha yake (Accept, Adjust, Advance-A.A.A)

IMANI YAKE ILIJARIBIWA.

  1. Ahadi ya maisha mapya.
  • Elisha alimpa ahadi kwa neno la Bwana.
  • Baada ya mwaka mmoja utapata mtoto wa kiume.
  • Kwa neno la Mungu mwanamke Mshunemu alichukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume.
  1. Huyu mwanamke aliogopa sana kuchukua tumaini lilopotea miaka mingi tu.
  • Aliogopa kumpoteza yule mtoto kwa mauti.
  • Upendo mkuu unateseka pakuu.
  • Mtoto alipogonjeka baba yake alisema, “Mrudishe kwa mama yake.”
  • Huyu mzee mume wa Mshunemu alikuwa mtu asiyehusika (hands off).
  1. Ahadi, ndoto, tumaini walikufa!!
  • Siku hiyo illipata kuwa giza kwa Mshunemu na mume wake!!
  • Kijana aliyetoka nyumbani na kwenda shambani kuvuna akiwa mzima, alirudishwa nyumbani akiwa maututi!!
  • Kitambo kidogo kijana alikufa katika mikono ya mamaye!!
  • Huyu alikuwa mtoto wa miujiza, mtoto wa ahadi, tumaini na ndoto za wazazi wake-Amekufa!
  • Je, Mungu alinidanganya? Kwa nini nilipata matumaini?
  1. Mama Mshunemu aliamini katika ufufuo wa wafu!!
  • Aliendelea kushika imani yake, aliendelea kuungana imani katika mauti.
  1. Huyu mama alifunga kinywa chake.
  • Alipoulizwa na mume wake, na nabii kama mambo yote ni sawa sawa, alisema SAWA!!
  • Alielewa kwa sababu mtoto alikuja kimuujiza, pia anaweza kuishi tena kimuujiza.
  • “Vitu vya muujiza, vinaishi kimuujiza.”
  • Mtoto alikuja kumuujiza, mtoto ataishi kimuujiza, atakufa kumuujiza (kichwa, kichwa) atafufuka kimuujiza!!
  • Mwanamke Mshunemu alikuwa amesikia juu ya jinsi Mungu alimfufua mtoto wa mjane wa huko Zeraphathi-1st Wafalme 17:22.
  • Alielewa roho mara dufu ya Eliya ilikuwa juu ya Elisha. “Imani huja kwa kusikia, neno la Mungu”-Warumi 10:17.
  • Kwa sababu ya imani badala ya kutengeza matanga na mazishi, alimlaza mtoto mfu juu ya kile kitanda cha nabii Elisha!!
  • Katika mfano wa Biblia kitanda cha Elisha ni Kristo na chumba chote ni kaburi la Kristo.

MTOTO ALIFUFUKA AKAREJESHWA KWA MAMA YAKE.

  1. Maombi ya mwanamke Mshunemu.
  • Elisha alikuwa mbali sana huko shule ya unabii-Karmeli.
  • Mshunemu alitembea mwendo wote mpaka kwa Elisha.
  • “Je, sinilikwambia usiyainue matarajio na tumaini langu?”
  • Huyu mwanamke anamwambia Elisha, “kwa nini ulinidanganya kama jinsi zawadi ya mhindi?”
  • Elisha alimtuma Gehazi lakini Mshunemu alitaka Elisha mwenyewe!!
  • Lazima kumtumaini “Mungu peke yake.”
  1. Elisha alimfufua mtoto.
  • Nabii alipofika chumbani alimkuta mtoto mfu amelazwa katika kitanda chake.
  • Yeye na Gehazi walimwombea yule mtoto-Vs. 33.
  • Elisha alimlilia yule mtoto, uso kwa uso, mwili kwa mwili-Vs. 34-mtoto alikataa kufufuka!!
  • Elisha aliteremka mpaka chumba cha chini na kurudi tena chumba cha juu.
  • Akamlilia mtoto tena, mpaka mtoto akapiga chafya mara saba.
  • Watu wa siku hizo waliamini chafya mara saba kulianza na Adamu-kama ishara ya uhai.
  • Elisha alimchukua mtoto hai na kumkabidhi mama yake.

MWISHO

  • Kisa cha (David Lloyd George) mama yake alipatwa na baridi, kutoa nguo zake zote kumpamba mtoto-hata mama alipokufa mtoto aliishi). David alikuwa waziri mkuu Uingereza!! Upendo wa mama.
  • Je, mama umewapoteza watoto wako? (madawa, uchungu, kuvunjika uhusiano, kukosa imani, pombe na anasa).
  • Kwa imani wadai wanao.
  • Simama katikati ya shetani na watoto wako, omba mpaka mwisho.
  • Mungu ni m’weza katika yote. Amen.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *