MFULULIZO: RUTHU
SOMO: RUTHU 2:2-19.
Kabla Ruthu kupata kupenya kwa Boazi, Ruthu aliomba kibali na neema. Hatima yako inahitaji sana kibali na neema.
- Ruthu 2:2, “Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, sasa niende kondeni niokote masaza ya masuke nyuma yake, yule ambaye nitaona kibali machoni pake, akamwambia, haya mwanangu nenda.”
- Ruthu 2:10, “Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi akamwambia jinsi gani nimepata neema machoni pako, hata ukanifahamu mimi niliye mgeni?”-Ruthu 2:13; 2:19.
- Neema ni kupata baraka bila kufanyia kazi.
- Neema inatoka kwa Mungu, kibali kinatoka kwa mwanadamu, waume kwa wake-Luka 6:38.
- Kwa kweli baraka zote zinatoka kwa Mungu lakini Mungu anawatumia watu kukubali na kukubarikia.
- Kweli Ruthu alibarikiwa na Mungu (YHWH) kwa sababu alipogeuka kulikuwa na mtu wakum’bariki.
- Ni jambo la kawaida kupokea kibali cha Mungu na kibali cha mwanadamu.
- Hivyo, kibali na neema zinafanya kazi pamoja kwa wao wampendao Mungu.
- Wewe pamoja nami tunaweza kutembea katika neema ya Mungu na kibali cha watu.
- Hivyo kibali na baraka zinaleta baraka saba:-
KIBALI KINASIMAMISHA MAUTI-Danieli 2:24.
- Danieli na wenzake waliokolewa na kibali cha Mungu.
- Malkia Esta aliwakomboa Wayahudi huko Persia kwa kibali cha Mungu-Esta 5:2 (Purim).
- Mtume Petro kwa kibali cha Mungu aliokolewa kifo katika mikono ya mfalme Herode-Matendo 12:3-7.
- Wakristo wa Yerusalemu hawakusadiki Petro amefunguliwa gereza-Matendo 12:9-12.
- Kibali mbele ya Mungu, kilisimamisha kifo na mauti.
- Unapopata kibali cha Mungu, watu pia watakukubali.
- Kibali cha Mungu kinasimamisha mauti, kinaponya magonjwa na kupinga mbinu za shetani.
KIBALI HULETA BARAKA ZA FEDHA.
- Kwa masaa 24, Ruthu alipata kutoka kuwa mjane, masikini na kuwa mashahuri katika mji wa Bethlehemu ya Yuda. Kibali cha Boazi kilileta baraka kwa maisha yake Ruthu.
- Inawezekana Mungu anawaleta watu walio na kibali cha Mungu, kuingia ndani ya maisha yako. Hawa ni watu watakao kuletea neema na kibali katika maisha yako.
- Yakobo alipoenda kwa nyumba ya mjomba wake Labani mle Syria, baraka za fedha ziliingia katika nyumba ya Labani maana Yakobo alikuwa na kibali cha Mungu.
- Labani alifahamu kwamba Yakobo ndiye alileta neema na kibali cha fedha-Mwanzo 30:27-30.
- Kwa kweli Mungu ndiye kiini hasa cha baraka zote, lakini Mungu atawatumia watu kama chombo cha kukubarikia.
- Kila wakati tafuta watu walio na kibali cha Mungu na neema. Ishi karibu na watu wa kibali lakini si watu wa laana.
- Unapotafuta mchumba tafuta mchumba aliye na kibali na neema, lakini si maskini wa laana, mateso, chuki na wasiwasi.
- Pengine kampuni unayofanya kazi inabarikiwa kwa uwepo na kibali cha Mungu juu yako.
- Viwanda vingi vinabarikiwa si kwa sababu ya management, mpango wa biashara na elimu ya viongozi pale, lakini kwa sababu ya wenye kibali cha Mungu wanaofanya kazi pale!!
- Kibali na neema huleta baraka nyumbani, kazini na popote pale!!
KIBALI HULETA BARAKA MARA DUFU.
- Ayubu alipoteza vyote; mali, fedha, watoto, heshima zake, marafiki.
- Ayubu aliazimu kukaa karibu na Mungu wake, baadaye Ayubu alipewa mara dufu ya mali, watoto, heshima na baraka-Ayubu 42:10.
- Elisha alipata kibali kwa kukaa na kumtumikia nabii Eliya mpaka mwisho-1 Wafalme 2:7-13.
- Wana wa manabii walitazama Elisha na Eliya wakienda. Kwa kufuata mtu wa kibali Elisha alibarikiwa mara mbili ya Eliya.
- Wana wa manabii walitazama, lakini Elisha alimfuata Eliya mpaka mwisho.
- Kila wakati tafuta kuambatana na wenye kibali na neema. Tafuta kuwa katika mahali pa baraka (location).
KIBALI KINA HAKIKISHA HATIMA YAKO.
- Je, umengojea miaka mingi kuona ahadi za Mungu kutimia kwako, kisha kwa mara moja tu, mtu anatokea ghafla na baraka za Mungu zinakujia?
- Esta alikuwa mwanamke aliyefanya mapenzi ya Mungu siku moja. Kwa kusimama mbele ya mfalme aliwaokoa Wayahudi wote kutoka mauti.
- Ruthu alikuwa mjane, maskini aliyeishi nchi ya ugenini, alifanya kazi ya kusaza, pembeni ya shamba. Kwa siku moja Ruthu alipata mchumba, mume, shamba, fedha, heshima na sifa.
- Ruthu alipata kuwa mashuhuri zaidi mle Bethlehemu ya Yuda na neema ya Mungu.
- Yusufu alipanda kutoka shimoni, gerezani mpaka ikulu ya mfalme wa Misri kwa sababu ya kibali cha Mungu.
- Billy Graham alikuwa mwinjilisti bila sifa yoyote. Siku moja Randolph Hearst mwenye gazeti kuu “La Times” aliamuru waandishi wake kumwangazia Billy Graham.
- Mara moja Billy Graham akawa mhubiri mashuhuri Amerika na Canada.
- Tunachohitaji ni kibali na neema ya Mungu kubadili historia ya maisha yetu.
- Katika mwaka wa 1948, Oral Roberts alikuwa mhubiri wa Hema mle Oklahoma. Siku moja gaidi alimpiga risasi Oral Roberts lakini bila kumuua!! Magazeti waliandika habari hizo, kila jimbo la Marekani Oral Roberts akajulikana duniani. Crusade yake ikaendelea kwa wiki 9, watu wakaokoka kwa wingi.
- Kwa masaa 24, kila mtu Marekani alimjua Oral Roberts.
- Kibali cha Mungu kinaweza kubadilisha laana kuwa baraka na kuharakisha hatima yako.
KIBALI KINAWEZA KUFANYA YASIOWEZEKANA KUWEZEKANA.
- Mfalme Daudi hata katika dhambi yake na Bathsheba, na mtoto wa kufa alipata kibali cha kumzaa Suleimani kupitia Bathsheba!!
- Mungu anakuweka mahali sahihi na watu sahihi kukupa kibali chake-2 Samweli 12:22-23.
KIBALI KINAKUJA KUPITIA MAOMBI.
- Kuokoka si dhibitisho ya kibali. Unaweza kuwa mtu wa kuokoka, lakini bado kibali.
- Kibali ni kama jinsi hekima, hatuzaliwi na hekima lakini tukiomba hekima tutapewa.
- Hata kuwahubiria ninyi ni kibali ambacho Mungu amenipa. Ikiwa washirika hawakupendi hawatasikia mahubiri yako-Kibali na neema lazima.
- Unapoenda kwa maofisi ya serikali lazima kibali. Mungu atawaondoa watu wabaya na kuwaweka wale wazuri kwa kibali.
- Kibali kinakuja kwa sababu ya maombi.
KIBALI SI KUSEMA HAUTAKUWA NA SHIDA.
- Nyakati nyingi pamoja na kuwa na kibali cha Mungu bado shida na hasara!!
- Kuwa na kibali cha Mungu ni kuwa na ushindi katika dhoruba za maisha.
- Bado watu watakuchukia wewe pamoja na kibali na neema za Mungu.
MWISHO
- Neema zinatoka kwa Mungu, kibali kinatoka kwa watu.
- Kiini cha baraka, kibali na neema ni Yehova Mungu.
- Tunahitaji kuomba kibali na kuvunjiwa laana na kutokubalika na watu.
- Uamkapo, uendako, omba kuwa na neema na kibali cha Mungu mbele ya watu wote.
- Mtumaini Bwana, enda mbele mpaka hatima yako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025