SOMO: ISAYA 3:10-11.
Kuna neno la unabii juu ya mwenye haki kwamba mwenye haki atakuwa heri.
Katika mipango na makundi ya mwanadamu watu wanapangwa kulingana na misingi ya utajiri, rangi ya ngozi zao, kabila na pia jinsia.
Lakini Mungu anapomtazama mwanadamu anawagawanya wanadamu kulingana na ufalme wake, mwanadamu ni mwenye haki au mwenye dhambi.
Kwa mfano Hebeli alikuwa mwenye haki kwa sababu alitafuta sana kumpendeza Mungu. Kaini naye alikuwa mwenye dhambi kwa maana alitafuta njia ya nafsi yake.
Wenye haki wanafanya haki kwa sababu wanampenda Mungu. Wenye dhambi wanafanya dhambi maana wanatafuta kufanya mapenzi yao na mapenzi ya nguvu za giza-1 Yohana 3:10-12.
Mungu mwenye nguvu zote ndiye ametuambia tuwaambie wenye haki watakuwa heri katika mambo yao yote.
Dhamana ya maneno inategemea ni nani ameyasema yale maneno.
Mungu Mwenyezi, Alfa na Omega, mwanzo na mwisho ndiye amenena-Ufunuo 2:13.
Mungu ni yeye anayesema maneno yake kutoka mwisho na mwanzo wake-Isaya 46:10.
Hakuna kitu kinaweza kubadilisha neno lake. Swali muhimu ni, Je, ni nani mwenye haki?
- Hatua ya kwanza kuwa mwenye haki ni kuokoka.
- Yaani kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mkombozi wa maisha yako.
- Yesu Kristo pekee ndiye anayeweza kukufanya mwenye haki na mtakatifu-Warumi 10:4.
- Hatua ya pili ni kukaa na kudumu ndani ya Yesu Kristo mpaka kuzaa matunda mengi zaidi-Yohana 15:4-5.
- Basi ikiwa wewe mwenyewe unayatimiza mambo haya mawili, neno la unabii katika Isaya 3:10 ni neno kwako, “Itakuwa heri kwako, katika jina la Yesu Kristo.”
Hebu tutazame:-
MIPAKA YA NENO HILI LA UNABII.
Neno hili la unabii lina maana tofauti kwa watu tofauti duniani.
- Kwa maskini Maanake ni utajiri utapokea kwa sababu Mungu ndiye anawapa watu wake nguvu za kutengeneza utajiri-Kumbukumbu 8:18.
- Kwa walio mateka na watumwa, Maanake ni utapata ukombozi wako. Mungu wetu ni Mungu wa majeshi. Mungu wa majeshi atawaangamiza maadui wako na kila nguvu ambazo zimekushika mateka-Isaya 49:25.
- Kwa walio wagonjwa, Maanake ni kwamba Bwana atakuponya magonjwa yako yote na kukupa amani-Isaya 53:3-6.
- Kwa walio tasa, Maanake ni kwamba tasa atapata watoto, atashika mimba, kwa maana Mungu anainua watoto kutoka kwa miamba na mawe-Mathayo 3:9.
- Kwa yule hajapata kufaulu katika maisha Maanake ni kwamba kufaulu kwako kunakuja. Kwa maana Mungu ndiye mwenye kupandisha watu cheo na daraja-Zaburi 75:6-7.
- Kwa walio chelewa Maanake, Mungu atakutembelea na matarajio ya moyo wako yatatimia haraka sana, ajabu za Mungu zitaonekana kwako.
- Kwa walio tafuta haki ya Mungu, Mungu kwa neema yake atakushika mkono wako mpaka mwisho.
- Mungu anao mpango wa ajabu kwa watoto wake.
- Kumbuka kwa msimu huu, neno lake halitapotea kamwe. Alicho ahidi lazima kutendeka kwako.
- Basi, shikilia neno lake kwa imani, itakuwa HERI kwako, katika jina la Yesu Kristo.
HAKI NA DHIBITISHO YA NENO LA UNABII HUU.
- Je, ni kwa nini Mungu anasema waambiwe wenye haki, “itakuwa heri kwao?”
- Kuna dhibitisho kadhaa kuamini neno hili la unabii:-
- Kwa sababu dhambi zao zimesamehewa.
- Dhambi ndio ubaya na uovu mkuu zaidi-Mathayo 11:28.
- Wamebarikiwa wale walio samehewa dhambi zao-Warumi 4:7.
- Kwa sababu Mungu hawezi kuwaacha wenye haki kuona uaribifu-Zaburi 16:5-6.
- Kwa sababu Mungu atawalinda watu wake-Zaburi 91:1-5.
- Mungu atawapigania watu wake katika kila vita.
- Macho ya Bwana yako juu ya wenye haki-Zaburi 34:5.
- Mungu anawapa wenye haki muongozo na kibali.
- Mungu anasikia kilio cha wenye haki. Mungu hawezi kuwaachilia wenye haki, bali Mungu anawakumbuka wenye haki milele-Zaburi 112:6.
- Hatua za wenye haki zinaongozwa na Mungu-Zaburi 37:23.
- Watoto wa mwenye haki hawawezi kukosa chochote kile-Zaburi 37:25.
- Njia ya mwenye haki inajulikana na Mungu.
- Mungu anajua kinacho endelea na kitakachofanyika kwa mwenye haki-Warumi 8:28.
HUKUMU KUPITIA NENO LA UNABII HUU.
- Mungu alimtuma nabii Isaya kuwapa moyo wenye haki na kuwapa wenye dhambi onyo kubwa sana.
- Kwa wote walio ndani ya Yesu Kristo neno la faraja na baraka nalikujie.
- Kwa wenye dhambi haitakuwa vyema kwao-Zaburi 1:1-5.
- Mungu kila wakati anafanya tofauti kwa wenye haki na wasio haki.
- Kwa wenye dhambi Mungu anangojea toba-Isaya 55:5-7.
- Maisha bila Yesu Kristo ni dharau na mwisho wake ni mauti.
- Wenye dhambi hawatambuliwi kama watoto wa Mungu, katika ufalme wake-Yohana 1:11-14.
- Wenye dhambi wako mbali na Mungu na baraka zake.
- Wenye dhambi waishi katika laana na chini ya ubatili na ufisadi-Wagalatia 6:6-8.
MWISHO
- Tutafute sana kutembea katika haki katika kila eneo ndani ya maisha yetu-2 Wakorintho 5:15.
- Tunahitaji kupokea neno hili la unabii juu ya maisha yetu na maisha ya watoto wetu kwa imani.
- Tunahitaji kutembea katika makubaliano na neno hili la unabii na kukata maungamo kinyume chake.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025