Swahili Service

REHEMA ZAKE HAZIKOMI

SOMO: MAOMBOLEZO 3:22-24.

 

Tunahitaji rehema za Mungu kuishi, ulinzi na kupandishwa katika kila eneo katika maisha yetu.

Safari ya maisha ni ngumu kueleza wakati mwingine mambo yanatujia bila repoti.

Wakati mwingine si walio na nguvu wanapona, si kila wenye hekima na akili, si kila wenye fedha na mali wanapona lakini wale tu wanaongojea rehema zake Mungu-(1 Samweli 2:9)

Rehema ni moja ya tabia za Mungu. Kwa rehema zake Mungu hawawezi kuwaacha wanyonge katika shida na udhaifu wao-Hesabu 14:18.

Kwa mwaka wote wa 2024, tumemwona Mungu, rehema zake zilikuwa dhahiri katika Maisha yetu. Kwa kweli hatukuangamia-1 Wakorintho 4:7-11.

Hebu tutazame;

MSINGI WA BIBILIA . TUNALIDWA NA NEEMA ZAKE.

  • Kuna mifano nyingi kwa Biblia, Mungu huwalinda watu wake kupitia rehema zake
  1. Wana wa Israeli katika nchi ya misiri walilindwa na rehema zake Mungu-Kutoka 2:23-25; 3:6-10
  2. Mungu aliwalinda miaka 400 mle Misri na kila changamoto za safari kurudi kwao Kanaani nchi ya ahadi.
  • Muujiza wa ukombozi kwa mwanamke aliyevamiwa na shetani katika Luka 13:10-18)
  • Huyu mwanamke hakutarajia ukombozi wa Yesu Kristo.
  • Kwa miaka 18, huyu mwanamke aliteseka, lakini hakupata rehema zake Mungu.
  • Wakuu wa sinagogi hawakupenda, lakini walinyamazishwa na rehema zake Mungu.
  1. Neema ilimponya yule mwanamke aliyetoka damu.
  • Yesu alikuwa anaenda mahali kwingineko.
  • Rehema zake Mungu zilimwona yule mwanamke na kumponya-Luka 8:41-48.
  1. Ukombozi juu ya Lazaro kutoka nguvu za mauti.
  • Kesi yake Lazaro ilikuwa ya huzuni zaidi. Rehema zake Mungu ziliingilia kati-Yohana 11:30-36.
  1. Ukombozi juu ya vijana Waibrania kutoka kwa tanuri ya moto-Danieli 3:16-25.
  • Mfalme alifikiri amefaulu kuwaangamiza – lakini rehema zake Mungu ziliingilia kati na kuwaokoa.
  1. Eutiko alianguka katika dirisha mpaka kifo lakini rehema zake ziliingilia kati na kumfufua Eutiko.
  2. Esta, alikuwa mtumwa wa kawaida, Mungu alimtumia kuwaokoa Waibrania katika nchi ya mbali – Rehema zake ziliwonekania-Esther 2:17.

UKWELI MKUU JINSI NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU ZINAWALINDA WATU. 

  1. Tunamtumikia Mungu mwenye uwezo wote. Huyu ni mwingi wa rehema-Kutoka 15:11; 1 Yohana 4:8.
  2. Mungu anawakomboa watu tayari kutoka nguvu za adui.
  3. Rehema za Mungu ziko tayari kila wakati wa mahitaji. Rehema za Mungu zimetosha katika kila hali.
  4. Rehema zake Mungu zinawafikia watu wake kupitia Agano la Adamu ya Yesu Kristo-Waebrania 12:24.
  5. Rehema za Mungu zinapitia hukumu yake Mungu-Zaburi 136:17-20.

NJIA ZA KUTEKELEZA REHEMA ZAKE MUNGU.

  1. Rehema za Mungu hazitegemei nguvu, uzuri au cheo, bali neema yake Mungu-Warumi 9:16.
  2. Rehema za Mungu pekee zinapitia katika neema za Mungu pekee-Waebrania 4:16.
  • Kuna njia ambayo tunajiweka katika mahali na njia za neema ya Mungu (positioning).
  1. Wale wanamfahamu na wanakuwa marafiki wake-Mithali 3:1-4.
  • Tunaingia katika ufalme wa Mungu kwa rehema zake, basi ni lazima kukaa katika ufalme wake, kuendelea kufurahia rehema zake-Yohana 1:11-12.
  1. Wale wanaotii neno la Mungu wanakaa katika station ya rehema-Zaburi 25:10; Kutoka 20:6.
  • Mungu ni Mungu wa Agano na Mungu anatimiza ahadi na Agano zake kwa wale wampendao-Nehemia 1:5.
  1. Neema na rehema zake Mungu zinawafikia wale wanao waonea wengine rehema-Mathayo 5:7.
  • Heri walio na rehema kwa maana wao watapata rehema.
  1. Wale wanaotembea katika haki-Zabari 1:1-5.
  2. Wale wanaoweka mizigo ya dhambi na maisha ya kale na kumtazamia Mungu-Wafilipi 3:13.
  • Rehema zake zinawajia wale wanao mtazamia na kutarajia mambo makuu kutoka kwa Mungu-Isaya 43:18-19.
  1. Wale walio na imani katika Mungu kiasi kumtegemea yeye pekee-Zaburi 32:10.
  2. Wale wanaomba na kumshukuru Mungu katika maisha yao-Yakobo 1:5-8; Yohana 6:11-12; Zaburi 106:1; Zaburi 118:1-3.
  • Kila wakati tukamwombe Mungu kutupatia rehema zake.

MWISHO

  • Kama si rehema zake tungeamgamia 2024.
  • Tukazidi kuomba Mungu kwa rehema zake kila siku.
  • Rehema ya Mungu inaponena kwa ajili yako yote yawezekana.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *