MFULULIZO: TUMAINI HAI.
SOMO: 1 Petro 2:11-25.
Kunyenyekea ndilo neno linalochukiwa sana duniani. Wengi wetu tunafanya kama jinsi kijana mmoja alivyolazimishwa na mama yake kuketi chini.
“Johnny tafadhali keti chini.” Johnny alipokataa kuketi chini, mamake alitumia nguvu kumketisha chini. Ndiposa alipoketi alimwambia mamake, “Mama hata ingawa nimeketi kimwili, lakini katika roho yangu ningali nimesimama.”
Kunyenyekea ni jambo linachukiwa na watu wengi hata kanisani.
Biblia inatufundisha kwamba ikiwa watu watatutii na kutunyenyekea ni lazima sisi pia tunyenyekee mamlaka yaliyowekwa juu yetu. Iwe ni serekali, ndoa, polisi, walimu, waajiri, waume zetu katika ndoa na jamii na mamlaka ndani ya kanisa.
Hili tuwe na mamlaka juu ya watu ni lazima sisi pia tutii mamlaka yaliyowekwa juu yetu.
Hivyo Mtume Petro 1 Petro 2:11-3:12 ametufundisha juu ya kunyenyekea na kuheshimu mamlaka katika maisha ya mkristo.
Watu wengi wanapenda kuwa na mamlaka juu ya watu wengine, lakini wao hawapendi kujiweka chini ya mamlaka ya wengine.
Bibia inatufundisha mamlaka ya Kibiblia inaenda pamoja na kujificha chini ya mamlaka yaliyowekwa juu yetu na Mungu.
Katika kifungu hiki, Mtume Petro anatufundisha juu ya kunyenyekea kama watoto wa Mungu na wananchi wa mbinguni. Wananchi 1 Petro 2:11-17, waajiriwa (2:18-25) ndoa (3:1-7) washirika kanisani (3:8-12).
Kunyenyekea si utumwa, lakini ni kutambua mamlaka ya Mungu juu ya maisha yetu.
Neno la Mungu linatuonyesha jinsi Mungu ameweka mamlaka nyumbani, serikalini, kanisani.
Kutoka bustani Edeni mwanadamu alikataa mamlaka, majaribu ya shetani kwa Adamu yalikuwa juu ya jinsi ya kukataa mamlaka.
Kwa sababu ya dhambi mwanadamu alipoteza mamlaka na uhuru. Mwana mpotevu alifikiri anaweza kuwa na uhuru bila mamlaka ya babake.
Mwana mpotevu alipoacha kuwa chini ya mamlaka, alipokea utumwa wa dhambi, umaskini na njaa.
Uhuru aliupata tu wakati alipokuja chini ya uongozi wa Baba yake na mapenzi ya babake.
Mtume Petro anatufundisha mambo matatu-madhumuni ya kunyenyekea, kutii mamlaka na kuishi maisha ya kujitoa Kikristo. Hebu tuone:-
MWENENDO WA MAISHA YAKO UNATAZAMWA NA ULIMWENGU WOTE-1 Petro 2:11-12.
- Kwanza, Mtume Petro anatukumbusha sisi ni nani.
- Sisi ni watoto wa Mungu.
- Petro anatujulisha sisi tuliookoka ni wapenzi wa Mungu-1 Petro 4:12; 2 Petro 3:1; 3:8; 3:14; 3:17.
- Petro anatufundisha kwamba unyenyekevu wetu unatokana na ule uhusiano wetu na Mungu wetu-Waefeso 1:5-6.
- Sisi sasa ni watoto wapendwa wa Kristo Yesu na Mungu Baba-Yohana 14:15.
- Pamoja na kuwa watoto, wateule, wapendwao wa Mungu, sisi ni wasafiri, wageni, tuwapita njia. Hatujafika kwetu-bado safari ni ndefu sana!!
- Petro anatueleza tena, kwamba sisi ni askari katika vita vya kiroho, tunapigana na tamaa za miili yetu (jihadi).
- Pamoja na kuwa katika vita vya kiroho habari njema ni tumeshinda vita tayari-Na tuzaidi ya washindi.
- Petro anaendelea kutueleza kwamba sisi ni shahidi kwa dunia iliyopotea katika ugiza wa dhambi.
- Kama Mkristro huwezi kusema “maisha haya ni yako, kuishi kama upendavyo (it is not your life or your lifestyle).
- Watu wa dunia wanakutazama.
- Hili tupate kuishi maisha yanayompendeza Mungu, Petro anatuhimiza kufanya mambo manne:-
- Ishi maisha matakatifu. Koma kuyatimiza mapenzi ya mwili.
- Usiwache nafasi ya kutusiwa na ulimwengu. Lazima tuwe na uadilifu wa binafsi
- Fanya matendo mema kwa wasioamini Mungu.
- Wafanyie wema walio mbali na Kristo, wageni na wapita njia.
- Wasiookoka wanatutazama kwa mbali na kwa karibu- Watendee mema.
Kumbuka wengine wanakutazama- Ishi kuwa mfano mwema katikati ya watu wa mataifa, matendo Yako yawe Nuru kwao.
- Wengi wakavutiwe na kumjua Mungu wako kiasi waingie katika sherehe atakaporudi Bwana Yesu Kristo.
- Dunia yote inatutazama waone kama Yale tunahubiri ni kweli katika maisha na mwenendo wetu.
- Ushuhuda wetu si kwa maneno tu, lakini kwa matendo (Mathayo 5:16).
MUNGU WAKO APATE SIFA NA UTUKUFU-(1 Petro 2:13-20).
- Tunaponyenyekea na kutii mamlaka yaliyoko Mungu anapata UTUKUFU.
- V. 23– “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana, ikiwa ni Mfalme, kama mwenye cheo kikubwa.”
- Unyenyekevu sio jambo rahisi hata wakati wa mtume Petro.
- Lakini Mtume Petro anasema Kila aliyeokoka ni lazima kutii Kila mamlaka ya mwanadamu.
- Mfalme, kama mwenye cheo kikubwa- (V. 23)
- Tii Gavana- Amepewa mamlaka ya kuweka amani katika County.
- Magavana na makomishoma wa makaunti wamepewa iwezo na mamlaka ya kuweka Sheria na amani katika eneo za utawala- (V. 14)
Utii kwa watawala wote ni mapenzi ya Mungu wetu tuliookoka- (V. 15).
- Usitumie uhuru wako katika Bwana kama chombo cha kufanya mabaya-(V. 16)
- Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu, Mcheni Mungu. Mpeni heshima Mfalme- (V. 17)
- Uhuru wa kweli na wa kibiblia unapatikana tunapojiweka chini ya mamlaka ya Mungu.
- Yesu alitupa mfano wa mamlaka-(Mathayo 8:8-9).
- Warumi walielewa vizuri sana jambo la mamlaka. Mamlaka yote yalikuwa mikononi mwa mfalme, lakini Mfalme aliwapa watawala wake sehemu ya ule utawala na mamlaka.
- Hivyo kutotii askari wa Roma ulikiwa ni kutotii Mfalme mwenyewe.
- Hivyo, uhuru na mamlaka yatapatikana tu, wakati tunapo chagua kunyenyekea mamlaka Yale Mungu ameweka katika mikono ya watawala- iwe ni katika serikali au katika jamii.
“Watumishi, waitiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio na wema na wenye upole tu, bali wao walio wakali” (V. 18).
- Mtume Petro anawahimiza wa Kristo kuwaheshimu waajiri wao kama ishara ya kumtii Bwana Yesu Kristo.
- Hivyo si dunia pekee inayotazama maisha na mwenendo wetu, lakini Mwokozi na Bwana wetu Yesu Kristo anatazama.
- Utii wetu kwa mamlaka ya dunia hii ni lazima, lakini pia hatuwezi kutii mamlaka yaliokinyume na mamlaka ni Neno la Mungu.
- Ikiwa, mkubwa wako kazini anakulazimisha kufanya dhambi hapo ni lazima kukataa na kupinga-(V.20).
- Shabaha na lengo letu duniani kama wakristo ni kumtukuza Mungu-(1st Wakorintho 10:31).
TUNAENDELEA KUBADILISHWA TUKAFANANE NA YESU KRISTO-(1 Petro 2:21-25).
- Tumeitwa tukafanane na Mwokozi wetu Yesu Kristo- V. 21.
- Tunapoteswa ni lazima tufuate hatua za Yesu Kristo na mfano wake.
- Yesu Kristo alipoteswa na wanadamu, aliendelea kunyenyekea na kujitiisha chini ya mikono wa Mungu Baba, Mungu Baba ni yeye pekee anayehukumu kwa haki.
- Baada ya mambo yote, lazima kujitiisha chini ya Mungu.
- Jitiishe chini ya Mungu Baba yako yeye ndiye mchungaji na Mwangalizi wa roho zetu.
- Unapoteswa na wanadamu, viongozi serekali usilipize kisasi.
- Usichukue sheria mikononi mwako, nyenyekea katika mikono ya Mungu Baba.
- Unapojipigania kwa nguvu zako, hapo unajiweka kando na uwepo na utetezi wa Mungu juu ya maisha yako.
- Lakini unapoanguka katika mikono ya Mungu, Mungu anachukua kesi yako, anakulinda, anakupigania, yeye ndiye Mchungaji na Mwangalizi wa roho yako.
MWISHO.
- Kwa chochote kile kinachoendelea katika maisha yako ni lazima kujiweka mikononi mwa Bwana.
- Hata katika mateso yote nyenyekea mbele za Mwokozi wako, ishi takatifu, mwache Bwana akupiganie.
- Mungu ametupa nguvu na uwezo wa kushindana na kila hali ya maisha.
- Yesu Kristo aliyapitia yote mabaya katika mikono ya mwanadamu mwenye dhambi, lakini Kristo alijitiisha chini ya mikono yake aliyekuwa na uwezo na mamlaka ya kuokoa.
- Kumbuka, Yesu Kristo ndiye Mchungaji na mwangalizi wa roho yako!!
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
- UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI. - October 19, 2025
- THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR. - October 19, 2025
