MFULULIZO: KRISMASI NI KUFUNULIWA KWA YESU KRISTO.
SOMO: LUKA 2:8-14.
Krismasi inafunua jibu la Mungu la furaha katika dunia ya dhiki, shida na farakano.
“Malaika akawaambia, msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote”-Luka 2:10.
Dunia hii tunayoishi ni mahali pa dhiki, shida, magumu ya uchumi, magonjwa, hofu na kuchanganyikiwa kiroho.
Mioyo mingi imevunjika na imebeba mizigo mizito sana-Mathayo 11:28-30.
Furaha katika maisha, jamii, dunia na nchi imekuwa jambo la mbali sana. Hakuna furaha duniani.
Katika dunia ya shida, Mungu alileta Krismasi kama njia yake kuleta furaha katika ulimwengu.
Kuzaliwa kwa YESU KRISTO hakukufanyika katika ikulu ya furaha na amani, lakini kulifanyika wakati wa ukoloni na utumwa wa Roma duniani kote.
Mungu hangojei kuwa na amani hili aweze kuachilia furaha yake.
Krismasi inatuonyesha kwamba furaha sio ukosefu wa dhiki na shida, lakini ni kuwepo kwa YESU KRISTO.
Krismasi hivyo, si tu sherehe ya siku fulani, lakini ni tangazo ya kwamba mbingu imeleta furaha kwa ulimwengu wa dhiki.
Furaha hii sio ya wakati au msimu, bali ni furaha ya milele, furaha ya nguvu, furaha inaobadilisha maisha. Hebu tutazame:-
KRISMASI NI TANGAZO YA FURAHA YA MUNGU KWA ULIMWENGU WA HOFU.
- Krismasi ilianza na tangazo ya furaha kwa ulimwengu hofu na hali ya heka heka.
- Mbingu ilitangaza furaha wakati wa hofu nyingi ulimwenguni.
- Hii ni kuonyesha kwamba furaha ya Mungu inao uwezo mkuu kuliko hofu ya mwanadamu.
Furaha inapigana na hofu-Luka 2:9-10.
- Wachungaji wa kondeni walihofu, lakini walipopokea habari ya furaha, hofu zao zilitoweka.
- Hivyo, furaha ya Mungu ni silaha dhidi ya hofu zetu-Nehemia 8:10.
Furaha ni ujumbe wa mbinguni-Luka 2:10.
- Furaha haikutengenezwa na mwanadamu-furaha inatangazwa na wale malaika.
- Furaha ya kweli inatoka kwa Mungu pekee.
Furaha ya mbinguni ni kwa watu wote-Luka 2:10.
- Furaha ya Krismasi ni kwa watu wote, maskini kwa tajiri, wenye nguvu na kwa wadhaifu, kwa waliokoka na wenye dhambi.
Furaha ya Mungu huvunja roho ya kudhoofika na kuvunjika moyo-Isaya 61:3.
- Mahali pote Yesu Kristo anapopokelewa, roho ya sifa na furaha inatawala.
- Wale wachungaji walimwona Mwokozi wao-Luka 2:20.
KRISMASI ULETA FURAHA KATIKA DHIKI.
- Yesu Kristo hakutangaza ulimwengu usio na dhiki-lakini Kristo aliahidi furaha inashinda dhiki.
- Krismasi inafunua furaha inaostahimili dhiki, shida na magumu yote ya maisha.
Dhiki ni lazima hapa duniani-Yohana 16:33.
- Yesu Kristo alisema dhiki itakuwa sehemu moja ya maisha hapa duniani.
- Lakini pia Yesu Kristo alisema tujipe moyo, maana yeye ameushinda ulimwengu.
Furaha imo ndani ya Kristo, si katika hali ya dunia na maisha-Yohana 15:11.
- Furaha inatoka kwa uhusiano bora na Mungu, lakini haitoki kwa hali nzuri duniani.
Furaha ya Mungu inaleta amani panapo taharuki-Wafilipi 4:7.
- Yesu Kristo anapotawala ndani, amani inamiliki mioyo yetu hata katika dhoruba zote.
Furaha ya Mungu inatupatia nguvu kama Wakristo-Nehemia 8:10.
- Furaha ya Mungu inakuwa nguvu zetu hata panapo majaribu.
- Paulo na Sila walifurahi hata katika mateso gerezani-Matendo 16:25.
KRISMASI UREJESHA FURAHA KATIKA MIOYO ILIYOVUNJIKA.
- Watu wengi wamepoteza furaha yao kwa kufiwa, kupoteza mali yao, dhambi na kwa dhiki ndefu.
- Krismasi ni wakati wa mwaliko wa urejesho wa Mungu kwako.
Mungu uponya mioyo iliyovunjika-Zaburi 147:3.
- Yesu Kristo alikuja kuponya mioyo na majeraha yasioweza kuponywa na wakati, juhudi na furaha za watu.
- Kilio kinavunjwa na furaha ya Mungu-Zaburi 30:5.
- Furaha inakuja kupitia wokovu wa Yesu Kristo-Isaya 12:3.
- Furaha ya kweli inatiririka kutoka kwa wokovu na upatanisho na Mungu.
Furaha inatoka kwa Roho Mtakatifu.
- Furaha ni tunda la Roho Mtakatifu- Warumi 14:17.
- Roho wa Mungu anatupa furaha ya kudumu.
KRISMASI INAFUNGULIA FURAHA YA MILELE KWA ULIMWENGU.
- Furaha ya Krismasi si kwa muda tu bali ni furaha ya milele kupitia mpango wa Mungu wa ukombozi.
Yesu Kristo ndiye mfalme wa amani na furaha-Isaya 9:3.
- Popote Kristo anapotawala, furaha inazidishwa bila kikomo.
- Furaha ni urithi wa ufalme wa Mungu-Warumi 15:13.
- Furaha ya Bwana inashinda giza-Yohana 1:5.
- Giza haiwezi kuzima furaha ya Kristo ndani yetu.
Furaha yetu itakamilika katika utukufu wa Mungu mbinguni-Ufunuo 21:4.
- Furaha ya milele inatungojea. Huko hakutakuwa na kilio na uchungu wowote milele na milele.
- Mamajuzi walifurahi kwa furaha kuu walipomwona Mwokozi Yesu Kristo-Mathayo 2:20.
MWISHO
- Krismasi ni dhibitisho kwamba Mungu anapoingia katika dhiki zetu anabadilisha hatima zetu.
- Aliyezaliwa katika hori ya ng’ombe alienda msalabani, alifufuka kwa nguvu, huyu Kristo Yesu ndiye anabadilisha dhiki zetu zikawa furaha, aibu zetu zikawa utukufu na majaribu yetu kuwa ushuhuda.
- Leo hii, msimu wako wa dhiki unabadikilishwa kuwa furaha. Usiku wako mrefu na uishe leo.
- Krismasi hii, wacha furaha ya Mungu iwe nguvu zako. Pokea kwa imani furaha ya milele sasa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE - December 25, 2025
- CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME? - December 24, 2025
- KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA - December 21, 2025
