SOMO: ZABURI 90:12.
Leo ni Jumapili ya mwisho ya maka 2025. Kuna majuma 52 kila mwaka.
Mungu amakuwa mwaminifu kwa maisha yako na nyumba yako mwaka mzima.
Ujumbe wa leo unafundisha jinsi sisi Wakristo tunaweza kumaliza mwaka katika amani, shukrani, ujasiri na furaha, huku tukitembea katika hekima, utii na kujiweka mikononi kwa Mungu.
Biblia inasema:-
Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima”-Zaburi 90:12.
Mungu uhesabu umri kwa siku, wala si kwa miaka kama wanadamu-Zaburi 39:4.
Mwaka huu wa 2025 umekaribia kwisha, tunahitaji kutazama nyuma kuona jinsi ulivyotumia mwaka mzima. Lakini tunapo tazama nyuma, tukawe na shukrani kwa ushindi tuliopewa na Mungu. Mapenzi ya Mungu kwetu ni kumaliza kila mwaka na kila msimu (season) bila shaka na majuto, huku tukiwa tumefungwa na rehema na neema zake na kuongozwa na hekima yake.
Majuto yanakuja kwa sababu ya kupoteza wakati, kutotii, uhusiano uliovunjika na nafasi tuliopoteza.
Pamoja na hayo yote, Biblia inatufundisha kwamba rehema za Mungu ni mpya kila ashubuhi. Neema ya Mungu inakomboa wakati uliopotea tunapojiweka katika mapenzi yake.
Hivyo, mwito wa Mungu kwetu leo, ni kumaliza mwaka bila majuto, huku tukinyenyekea chini ya mikono ya Mungu, tukiishi ka imani na kumtumaini Mungu kila siku. Pamoja na kufahamu kwamba yote yaliyotendeka kwetu yawe mazuri au mabaya, yote yalichangia mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Hebu tutazame:-
TAMBUA REHEMA ZA MUNGU KWA MWAKA MZIMA (2025).
- Kumaliza mwaka bila majuto kunaanza na kutambua rehema za Mungu kila siku ya mwaka unaokwisha.
Mungu alidumisha maisha yako-Maombolezo 3:22-23.
- Rehema za Mungu zilikulinda kutoka hatari zinazoonekana na zile zisizoonekana.
Mungu alikujalia nguvu kila siku-Isaya 46:4.
- Neema yake ilikubeba wakati wa dhiki na udhaifu.
Mungu alikuwa mwaminifu kwako hata wakati ulishindwa
–2 Timotheo 2:13.
- Hata ulipopoteza uaminifu wake au kukoma.
Mungu alikuongoza miguu na kila hatua-Mithali 16:9.
- Kila siku ya mwaka ulikuwa chini ya uangalizi wake Mungu.
- Mfalme Daudi aliona Mungu akiwa mwaminifu hata katika dhambi, alipokea urejesho wa Mungu-Zaburi 51; 103:1-5.
WACHILIA MAJUTO YA MWAKA YAENDE.
- Uhuru kutokana na majuto inahitaji kuachiliwa na kutazamia nehema ya Mungu kutawala maisha yako.
Mungu ameamuru tutazame mbele-Wafilipi 3:13-14.
- Kutazama nyuma kutazuia kwenda mbele.
Mungu anarejesha wakati uliopotea-Yoeli 2:25.
- Mungu anarejesha miaka iliyopotea, iliyoharikika na iliyoibiwa na adui.
Mungu anasamehe dhambi tunazotubu-Yohana 1:9.
- Kuungama dhambi huleta kuoshwa, si hukumu.
Mungu anafanya makosa tuliyofanya kuwa somo-Warumi 8:28.
- Hakuna kitu kinapotea mikononi mwa Mungu.
MALIZA MWAKA KATIKA UTII NA SHUKRANI.
- Majuto yetu yanatoweka panapo utii na mioyo ya shukrani.
Utii unaleta amani-Isaya 1:19.
- Tunapotii, utii unavuta kibali cha Mungu kwetu.
Shukrani inalainisha mtizamo wetu-1 Wathesalonike 5:18.
- Tunapokuwa watu wa kushukuru, ukosefu wetu utarudi kuwa baraka.
Sifa na ibada inafungua mwaka vizuri-Zaburi 92:1-2.
- Sifa zetu zinamheshimu Mungu.
Unyenyekevu unavutia neema ya Mungu kwetu-Yakobo 4:6.
- Mungu anawainua wanaotambua usaidizi wake.
- Yesu Kristo alishukuru mbele ya kufanya muujiza, kuonyesha nguvu za kuwa mtu wa shukrani-Yohana 6:11.
HEKIMA YA KUPANGA MWAKA UJAO.
- Tunapomaliza mwaka vizuri Maanake ni kuanza mwaka mpya vizuri.
Hekima inafanya moyo kuwa tayari-Mithali 4:7.
- Hekima inatuongoza kufanya uamuzi bora.
Maono yanafanya njia yetu kuwa wazi-Habakuki 2:2.
- Tunapoandika maono yetu, tutakuwa makini zaidi kufuata.
- Maombi yanatufanya kuweka maisha na mipango yetu mikononi mwa Mungu-Mithali 3:5-6.
- Tumaini inatufanya kutia nanga yetu katika Bwana-Warumi 15:13.
- Mungu anajaza siku zetu na amani na furaha.
MWISHO
- Kumaliza mwaka bila majuto ni kujiweka katika rehema za Mungu, hekima yake na mipango yake.
- Tunapotambua uaminifu wake, kuachilia yaliyopita, tunapotembea katika utii, amani ya Mungu itamaliza kabisa majuto yetu.
- Tunapomaliza mwaka huu, chagua kuwa mtu wa shukrani na imani. Changua kuwa tumaini na ujasiri.
- Maisha yako yapo imara katika mikono ya Mungu.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU - January 25, 2026
- DEEP CALLS TO DEEP-A JOURNEY INTO GOD - January 25, 2026
- MUNGU NI MUNGU WA MABONDENI - January 18, 2026
