MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO.
SOMO: 1 WAFALME 20:23-28.
Mabonde si mahali pa kuachwa lakini ni mahali pa kumkabidhi na kukutana na Mungu. Mabonde katika maisha ni sehemu ya safari yetu ya kiroho, hapa bondeni ndipo tutaona uaminifu wa Mungu kwa kina.
Bonde katika maisha ni picha ya nyakati za maumivu, kuvunjika mioyo, kukata tamaa, nyakati za kupoteza na wakati wa kukosa hakika.
Watu wengi wanamwona Mungu wao zaidi juu ya milima ya maisha, lakini wanakosa kuona uwepo wake wanapopita katika bonde.
Mungu ni Mungu wa milimani na pia ni Mungu mabondeni!!
Majeshi ya Shamu walikosa waliposema Mungu wa Israeli ni Mungu wa milimani, lakini si Mungu wa mabondeni na chi tambarare-1 Wafalme 20:23-28. Mungu wa Israeli aliwaonyesha kwamba yeye ni Mungu wa bondeni na nchi tambarare.
Hii ni kuonyesha kwamba uwepo wa Mungu, nguvu zake na makusudi yake yako kila mahali hata wakati wa shida na dhiki za maisha.
Katika ujumbe wetu hivi leo, tutajifunza jinsi Mungu anatembea pamoja nasi katika bonde, jinsi anatupigania na kufanya bonde liwe mahali pa ufufuo na urejesho. Hebu tutazame:-
MUNGU YU PAMOJA NASI KATIKA BONDE LA MAISHA.
- Hakuna bonde kubwa zaidi kwa Mungu wetu!! Mungu wetu anapatikana katika kila bonde la maisha yetu.
Mungu anatembea nasi bondeni-Zaburi 23:4.
- Tujapopita katika bonde la uvuli wa mauti Mungu yuko pamoja nasi, kutufariji na kutuongoza.
Bondeni sio mwisho wa safari-Hosea 2:14-15.
- Mungu anabadilisha bonde la Akori (dhiki) kuwa mlango wa tumaini.
Uwepo wa Mungu huleta ujasiri bondeni la maisha-Joshua 1:9.
- Hofu haiwezi kukaa panapo uwepo wa Mungu.
Bonde inatufundisha kumtumaini Mungu zaidi-Warumi 8:28.
- Hata bonde ya maumivu itafanya kazi pamoja na kuleta mema kwa wale wampendao Mungu, walioitwa kwa kusudi zake.
- Mfalme Daudi alikuwa na ujasiri katika bonde la uvuli wa mauti-Zaburi 23:4.
MUNGU ANATUPIGANIA KATIKA BONDE LA MAISHA.
- Mungu anaonekana si tu katika nguvu zetu lakini zaidi katika udhaifu wetu.
Adui zako wanadharau Mungu wako unapokuwa katika bonde la maisha-1 Wafalme 20:28.
- Mungu alijibu adui za Israeli, kwa kuonyesha yeye ni Mungu kila mahali, wakati wote.
Bonde lako ndipo uwanda wa ushindi katika vita-2 Mambo ya Nyakati 20:15-17.
- Vita ni vyake Bwana, hata katika bonde za maisha yako.
Mungu anatumia bonde za maisha yako kuonyesha ukuu wake-Zaburi 44:3-7.
- Ushindi wetu si kwa sababu ya nguvu zetu bali ni kwa nguvu za Mungu.
Unaposimama wima, Mungu atajidhihirisha kwako-Kutoka 14:13-14.
- Kusimama wima katika bonde la maisha yako kunampa Mungu nafasi ya kutenda miujiza.
MUNGU ANAREJESHA UZIMA WAKO KATIKA BONDE LA MAISHA.
- Bonde ni mahali pa ufufuo na urejesho.
Bonde ni mahali pa unabii-Ezekieli 37:1-10.
- Mifupa mikavu inapata kuishi tena Mungu anaponena bondeni.
Mungu anapopumua uzima kwa chochote kilicho kufa-Ayubu 14:7-9.
- Hata mahali pasipo na tumaini, Mungu anausha chochote kilicho potea.
Neno la Bwana lina nguvu bondeni-Isaya 55:11.
- Neno la Mungu linabadilisha mambo yote, palipo na hofu, Mungu anawapa watu wake ushuhuda.
Urejesho unaonekana mahali utii unaanza katika lile bonde la mauti-Ezekieli 37:7.
- Tunapotii, bonde la mauti linakuwa bonde la ufufuo na uzima.
- Bonde la mifupa mikavu lilifanyika la jeshi hai-Ezekieli 37:1-10.
MUNGU ANAONGEA KATIKA BONDE LA UAMUZI.
- Bonde la maisha ni mahali hatima za watu zinabadilika na maamuzi kufanyika.
Mabonde yanafichua hali ya mioyo yetu-Kumbu kumbu 8:2.
- Mungu anatujaribu kufichia na kusafisha imani yetu.
Bonde ni mahali pa uamuzi-Yoeli 3:14.
- Wengi wa watu wamo katika bonde la kukata maneno. Wako katika njia panda katika maisha yao.
Mungu anatuita kujitoa kamilifu katika bonde la maisha-Warumi 12:1-2.
- Katika bonde la magumu Mungu anatufanya upya.
Bonde la maisha inatufanya kuwa tayari kwa mlima unaokuja mbele zetu-Yakobo 1:2-4.
- Uvumilivu katika bonde la maisha unatuongoza kupandisha daraja na cheo juu ya mlima.
- Eliya aliongozwa mpaka mlima wa Herobu-1 Wafalme 19:4-8.
MWISHO
- Bonde la maisha si ishara ya kushindwa bali ni ishara ya kukutana na nguvu, uwepo na utoshelevu wa Mungu.
- Milima ni ishara ya utukufu, lakini bonde ni ishara ya neema ya Mungu.
- Je, leo hii wewe uko wapi? Bondeni au mlimani? Mungu anatawala milimani na mabondeni?
- Mungu anatembea nawe, atakupigania, atakurejesha, ataongea.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU - January 25, 2026
- DEEP CALLS TO DEEP-A JOURNEY INTO GOD - January 25, 2026
- MUNGU NI MUNGU WA MABONDENI - January 18, 2026
