MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO.
SOMO: ISAYA 8:18.
Mungu wetu ni YEHOVAH. Yehovah si Mungu mtupu na kimya-bali ni Mungu wa ishara na maajabu. Kutoka Mwanzo mpaka Ufunuo, Biblia inaonyesha Mungu anayejidhihirisha kwa ishara, maajabu na miujiza. Ajabu zake zinapita fahamu zote za mwanadamu.
Ishara, maajabu na miujiza ya Mungu si ya kutumbuiza mwanadamu, bali ni njia zake za kutangaza uwezo, uwepo na mapenzi yake, huku akiwatafuta watu wamjie.
Ishara na maajabu ni njia za Mungu kuingilia kati na majira ya asili, hili mwanadamu aweze kumheshimu Mungu.
Ishara na maajabu zinaleta ukombozi kwa waliomateka ya shetani, kuwaponya walio wagonjwa, kuwalisha walio na njaa, kuwatosheleza walio na mahitaji na kujenga imani kwa walio dhaifu.
Ishara, maaajabu na miujiza ni maonyesho ya Mungu asiyeonekana.
Leo, tunapotazama asili na sababu za ishara, maajabu na miujiza, tukumbuke kwamba Mungu angali Mungu wa ishara, maajabu na miujiza. Leo kama zamani uwezo wa Mungu bado pungua na mapenzi yake kujionyesha kwa uwezo na nguvu zake ni kama zamani na zaidi leo kuliko zamani. Hebu tutazame:-
MUNGU ANAONYESHA NGUVU NA UWEZO WAKE KUPITIA ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA.
- Mungu anatumia ishara, maajabu na miujiza kudhihirisha nguvu na uweza wake juu ya viumbe vyote.
Ishara zinaonyesha uungu wa nguvu za Mungu juu ya viumbe vyote-Kutoka 14:21-22.
- Bahari ya Shamu ilirudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki. Mungu akawakomboa wana wa Israeli kutoka Misri.
Maajabu yanaonyesha mamlaka ya Mungu juu ya magonjwa na mauti-Yohana 11:43-44.
- Yesu Kristo alimfufua Lazaro kutoka kaburini huku akishinda nguvu za mauti.
Mungu anatumia ishara kudhibitisha watumishi wake-Matendo 2:22.
- Yesu Kristo alidhibitishwa na Mungu baba kupitia miujiza, maajabu na ishara.
Ishara ni sehemu ya Agano la Mungu na watu wake-Marko 16:17-18.
- Waamini wameahidiwa ishara wanapotembea katika utii wa imani.
- Katika nchi ya Misri, Mungu alitumia Musa kutenda ishara kumi (10) kuwakomboa wana wa Israeli kutoka utumwa wa Misri.
- Ukuu wa Mungu ulionekana kwa wote-Kutoka 7-12.
ISHARA NA MAAJABU YANAWAVUTA WATU KWA WOKOVU.
- Ishara na maajabu ni silaha za Injili na kuokoa watu.
Ishara zinadhibitisha habari njema na Injili-Waebrania 2:4.
- Mungu ushuhudia kwa ulimwengu kupitia ishara, maajabu na miujiza.
Ishara zinavunja kutoamini na pingamizi kwa Injili-Matendo 8:6-8.
- Watu wengi waliamini na kuokoka mle Samaria walipoona ishara zilizotendwa na mtume Filipo.
Maajabu yanafungua milango ya kuhubiri Injili duniani-Matendo 3:6-10.
- Uponyaji wa yule mtu kiwete uliwavuta watu wengi kwa wokovu na Yesu Kristo.
Ishara zinawarudisha watu wengi kwa Mungu-Yohana 2:11.
- Muujiza wa kwanza wa Yesu Kristo mle Kana ya Galilaya ulifanya wanafunzi wa Yesu Kristo kumwamini.
MUNGU ANGALI ANAFANYA ISHARA, MIUJIZA NA MAAJABU LEO.
- Miujiza haijaisha katika Biblia-miujiza inaendelea panapo imani.
Yesu Kristo bado ni yule jana, leo na milele-Waebrania 13:8.
- Nguvu zake Mungu hazijaweza kwisha, Mungu yuatenda miujiza, ishara na maajabu mpaka leo.
Mungu anaamkia panapo matarajio ya imani-Mathayo 9:29.
- “Kulingana na imani yako utatendewa.”
Ishara zinawafuata wanaoamini-Marko 16:17-18.
- Sisi tunabeba nguvu za Mungu kutenda miujiza, ishara na maajabu kupitia nguvu za Roho Mtakatifu.
Kanisa ni jukwaa na uwanda wa maonyesho ya uwezo na uwepo wa Mungu-1 Wakorintho 2:45.
- Injili ni lazima kuhubiriwa pamoja na ishara, miujiza na maajabu kuonekana.
- Mtume Paulo alitenda miujiza, ishara na maajabu kiasi hata kivuli chake kikaponya watu.
- Kanisa la karne ya kwanza lilikuwa na nguvu kiasi vivuli na vitambaa vikatumika kutenda miujiza-Matendo 5:15-16.
WAUMINI WANAHITAJI KUMFUATA MUNGU LAKINI SI KUTAFUTA MIUJIZA, ISHARA NA MAAJABU.
- Ishara zinahitaji kutuelekeza kwa Mungu si zile ishara ziwe sanamu.
Usikimbilie miujiza-lakini kimbilia Mungu wa miujiza-Mathayo 6:33.
- Tafuta kwanza ufalme wa Mungu na ishara, maajabu na miujiza zitakufuata kawaida.
Ishara zinadhibitisha neno, lakini si kuchukua mahali pa neno-Yohana 4:48.
- Yesu Kristo aliwakemea watu waliomfuata tu kwa sababu ya miujiza.
Tembea katika utakatifu na utii upate kubeba nguvu za Mungu-Matendo 5:32.
- Roho Mtakatifu anapokelewa na wenye utii.
Ishi maisha ya unyenyekevu na mpe Mungu utukufu wote-Matendo 3:12-13.
- Petro na Yohana walitangaza kwamba miujiza, maajabu na ishara zinatendeka si kwa nguvu za mwanadamu, bali kwa nguvu za Mungu.
- Simoni yule mchawi alipenda sana nguvu za kutenda miujiza, lakini hakupenda Mungu wa ile miujiza, ndipo Petro alimkemea vikali sana-Matendo 8:18-23.
MWISHO
- Mungu angali katika kazi ya kutenda ishara, maajabu na miujiza leo.
- Mungu hajakufa au kunyamaza, Mungu yu hai leo.
- Tunapomwamini Mungu wa miujiza, ishara na maajabu, maisha yetu yakamtegemee Mungu kutenda hayo yote kupitia kwetu.
- Wacha Mungu wetu akafanye miujiza, ishara na maajabu juu yetu sasa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU - January 25, 2026
- DEEP CALLS TO DEEP-A JOURNEY INTO GOD - January 25, 2026
- MUNGU NI MUNGU WA MABONDENI - January 18, 2026
