LUKA 19:41-44
UTANGULIZI
Yesu Kristo ni yeye jana leo na milele. Kristo ni yeye yule aliyelilia mji wa Yerusalemu. Injili ndio inayechangia amani yako. Kristo aliwaona jinsi walikataa siku ya neema kwao. Kristo kweli yuko tayari kuwaokoa wenye dhambi wote. Hebu tuone kwanini Kristo alilia siku ya jumapili –Mitende (Palm Sunday):-
I. KUTOFAHAMU NA UJINGA WAO (19:42)
- Siku moja mfalme Napoleoni na jeshi lake walikuwa wakipata Uswiji (Switzerland) kila mahali walipita watu wengi waliwashangilia “ishi milele mfalme wetu, viva la france!. Sifa kwa mfalme Napoleoni”. Lakini mfalme Napoleoni hakujibu salamu zao, lakini alipoulizwa kwanini, Napoeloni alisema “Hawa watu wanao nisifu sasa, kesho ndio watasema hatumpendi tena !. Napoleoni alifahamu nia na moyo wa wanadamu. Yesu Kristo pia alifahamu mwanadamu ni nani. Yesu alilia juu ya Yerusalemu.
- Kati ya watu laki moja hau mbili walimshangilia Kristo jumapili lakini wale wale wale ndio walisema “Msulumbishe” siku ya ijumaa.
- Kwa nini hawa watu walimkataa Kristo
- Walitarajia kristo awakomboe toka utawala wa Roma, lakini Kristo alipenda kuwaokoa kutoka dhambini.
- Walimtaka Kristo aketi kutawala katika kiti cha babaye Daudi, Yesu alitaka kutawala mioyo yao.
- Walitaka uhuru kisiasa, Yesu alitaka wapate uhuru Kiroho.
- Walitaka Kristo awaletee Enzi na ufalme wa dunia hii– Kristo alileta ufalme wa kiroho
- Hawa watu walifunga macho na nia zao kwa kweli.
- Hawa watu walikuwa na Torati, Zaburi, Musa na manabii– lakini walitaka tafsiri yao wenyewe.
- Je, sisi nasi tunafahamu kweli, je tunamjua Mungu?
II. UFAMIZI JUU YA YERUSALEMU (19:43-44)
- Watu hawa walipomshangilia na kuimba nyimbo za sifa kwa kristo.
- Watu hawa walipoimba “Hossana” (V.38-39)
- Kristo aliyaona yatakayowajia watu wa Yerusalemu miaka 40 ijayo.
- Warumi wataharibu mji wa Yerusalemu.
- Nyimbo za hosanna– zitakuwa kilio kwao, mitaa iliyotandazwa na mitende, siku hio itatandazwa na damu yao na watoto wao.
- Kristo aliona mauti, hofu na kilio Yerusalemu mika 40 baadaye.
- Mapenzi yake kwao ilimfanya Kristo kulia sana.
III. YERUSALEMU WALIANGUKA MTIANI NA INSPECTION YA MWOKOZI (19:44)
- “Hawakutambua majira ya kujiliwa kwao”
- Kujiliwa (Visitation) ni wakati Mwenye mamlaka anafika kuukangua mji, nyumba, kazi, miradi.
- Yesu Kristo alipokuja ,nyumba ya Israeli aliwakuta katika hali mbovu.
- Dini yao hekaluni ilikuwa tupu, ibada zao na sheria zao zilikuwa duni kabisa.
- Yerusalemu hawakutubu dhambi zao kama jinsi Ninawi katika mahubiri ya Yona.
- Walipooneka kama watakatifu, ndani yao walikuwa wahofu sana.
- Yesu Kristo aliwalilia hawa watu!!
MWISHO
- Kila moja wetu siku moja tunapitia katika inspection ya Mungu.
- Kazi na matendo yetu mema haitasaidia katika uganguzi wa Mungu. Anapenda utakatifu wa ndani.
- Lakini baadaye palikuwa ijumaa njema, jumapili ya kufufuka na siku ya pentecoste.
- Je, unatambua majira ya kujiliwa kwako?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
