Swahili Service

WAZAZI WA YOHANA WALIMPENDA MUNGU

LUKA 1:5-22 

UTANGULIZI

Tumefika Krisimas tena. Katika ibada hii        tuta tazama sana watu waliochangia pakubwa katika kuzaliwa, kwa Mwokozi wetu Yesu  Kristo. Nyuso za Krismasi ni nyuso za wale walikuwa karibu zaidi. Zakaria na mke wake Elisabeti walikuwa wazazi wa Yohana       mbatizaji .Wote wawili walimpenda Mungu  sana, wote wawili walimtumkia Mungu kwa moyo safi na utakatifu. Walikuwa wa kwanza kupokea habari za kuzaliwa Mwokozi wa   ulimwengu. Kwa miaka 400, neno kutoka mbinguni halikusikika. Zakaria akawa wa kwanza kusikia toka  mbinguni.

Hebu tuone:-

I.  WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI (V.5)

  1. Mtoto Yohana aliahidiwa kwa wazazi wake wakati wa utawala wa Herode, mfalme wa Uyahudi (BC 37-4 AD)
  2. Babaye Yohana alikuwa Zacharia
  • Maana ya jina Zakaria ni “Mungu amekumbuka” hau “aliyekumbukwa na Yehova”
  • Zakaria alitoka milimani ya Yuda
  • Zakaria alikuwa kuhani wa zamu za Abiya.
  • Zamu zote zikuwa 24 – makuhani wote walikuwa 20,000, hekalu moja tu – hivyo kupata nafasi ilikuwa ngumu sana, waliingia kwa kura. (I Mambo 24:1-10)
  1. Mamaye Yohana alikuwa Elisabeti, maana ya jina Elisabeti “yeye ambaye nadhiri yake ni kwa Mungu”
  • Babaye Elisabeti alikuwa kuhani
  • Elisabeti alikuwa bikira alipoolewa na Zakaria (Walawi 21:14)

II.   WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKUWA WENYE HAKI (V.6)

  1. Wote wawili walikuwa wenye haki, walijitoa wao kwa wao katika ndoa, walimwishia Mungu kama mume na mke.
  2. Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wote walimtumikia Bwana kwa uaminifu.
  3. Wote wawili walimpendeza Mungu kwa maneno, na matendo.
  4. Wote wawili waliishi bila lawama mbele za Mungu na watu

 

III.  WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKUWA NA SHIDA ZA        WANADAMU (V.7)

  • Kuwa mwaminifu na bila lawama na kuokoka si kukosa kuwa na shida maishani. (I Wakorintho 10:13)
  1. Hawakuwa na mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa.
  2. Wote wawili walikuwa wazee sana na shida za uzee zilikuwako. (Zaburi 69:20)

 

IV.   WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKUWA WATU WA IBADA (V.8-9)

  • Zakaria alikuwa kuhani mwaminifu, hata bila mtoto (Yakobo 1:12, Yakobo 5 :11)

 

V.   WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKUWA WATU WA MAOMBI (V.10) (Zaburi 91:15, I Mambo ya Nyakati 16:11)

 

VI.  WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKUWA NA KIBALI CHA MUNGU (V.11-17)

  • Zakaria alipokea kibali cha Mungu kwa njia tano.
  1. Mahitaji yao yalijibiwa na Mungu binafsi alipokuwa katika maombi na ibada.
  2. Maombi yake yalijibiwa – Elisabeti atazaa mwana, jina lake Yohana – “Neema ya Yehova”
  3. Mwana wao atakuwa mkuu.
  • Wazazi wake watafurahi – hakuna aibu, lakini fuhara.
  • Yohana ataleta furaha kwa watu wote
  • Yohana atakuwa mkuu mbele za Mungu
  • Yohana atakuwa mwenye nidhamu kuu, hatalewa pombe au kileo (I Tim 1:12)
  • Yohana atakuwa nabii wa Bwana atawarudisha wengi kwa Mungu.
  • Yohana atakwenda mbele za Bwana kutengeza njia za Bwana katika roho ya Eliya (Malaki 4:5)

VII.  WAZAZI WA YOHANA BATIZAJI WALIKOSA KUMWAMINI MUNGU (V.18-19)

  • Zakaria alikosa kusandiki neno la Bwana, hivyo akawa bubu na pia kiziwi.
  • Malaika Gabrieli ni malaika mkuu – Malaika Gabrieli ni mtu wa Mungu, anasimama mbele za Mungu. Gabrieli huleta habari njema kwa mwanadamu. (Danieli 8:16, 9:21, V.13, V.26)
  • Zakaria aliomba Ishara na akapewa Ishara – bubu, kiziwi.
  • Je, tunayaamini tunao omba?

VIII.  KUKOBA IMANI KUNAFUNGA ULIMI WA USHUHUDA (V.20)

  • Zakaria alikawia sana kwa kumwona Gabrieli na uwepo wa Mungu
  • Uwepo wa Mungu unachukua wakati, siku moja na Bwana ni njema kuliko miaka bila uwepo wa Bwana.

 

MWISHO

  • Je, umemgoja Bwana kiasi gani?
  • Leo, ndiyo siku ya kujiliwa kwako, dumu katika maombi, ibada, utakatifu na Imani.
  • Toa ushuhuda wako mbele za watu kwa jinsi Bwana ametenda makuu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *