Swahili Service

AHADI ZA MUNGU

MFULULIZO:  JINSI YA KUSTAHIMILI DHOROBA ZA MAISHA

SOMO:   WARUMI 8:28

Sasa yapita karibu majuma tatu tangu koronavirus (Covid-19) kutangazwa hapa kenya na Afrika mashariki. Kweli kazi zetu zimefungwa hasa makanisa na shule zote. Curfew, amri ya kutotoka inche saa moja jioni mpaka asubuhi imeweka. Wengi wamepoteza kazi na biashara zao. Mambo ni magumu wezetu wamepoteza maisha yao, wengine wameishi katika vizuizi za quarantine siku si haba. Na bado janga yake koronavirus ingaliko duniani. Watu halaiki duniani wamefariki. Swali kubwa duniani na pia kwa binafsi ni, je, ni kitu gani chema kitakacho tokea katika korona?

Mbele ya koronavirus kuja duniani kuna watu bado walikuwa katika janga za hapo hawali, koronavirus imekuja kuongezea. Pengine unajiuliza je, kweli kuna mazuri hapa chini ya jua? Ujumbe wetu hivi leo ni ujembe wa kukupa tumaini na faraja kutoka kwa Mungu. Wewe unapojiuliza je, chochote chema kinaweza tokea katika mauti? Je, chochote chema kinaweza tokea kwa ugojwa huu wangu?

Je, chochote chema chaweza kutokea kwa unajisi na mateso ninayo pitia sasa?

Katika Biblia (Warumi 8:28) Biblia inasema hivi: “nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao, katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.”

Kifungu hiki ni AHADI kinafundisha mambo tano (5) juu ya Ahadi za Mungu

Hebu tujifunze:-

I.  AHADI ZA MUNGU NI HAKIKA NA KWELI—(NASI TWAJUA)

  • “Nasi twajua” ndungu na dada zangu popote ulipo,” nasi twajua.
  • Wewe unaoteseka, na ugojwa, kutumika vibaya, uchungu na maumivu ya roho na mwili “nasi twajua”
  • Wewe biashara yako imefunga na uchumi wako kuzorota “nasi twajua”
  • Wewe uliyefiwa, uliyetupwa inje, uliyekataliwa na kudhulumiwa “nasi twajua”
  • Wewe uliyembali na nyumbani na korona imefunga mipaka na safari za ndenge na unaishi ugenini ‘nasi twajua”
  • Ahadi za Mungu ni hakika kabisa (Waebrania 13:5)
  • Katika (Hesabu 23:19) “Mungu si mtu, aseme uongo wala si mwanadamu, ajute, iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
  • Mungu si mtu, Mungu si mwanadamu – mtu na mwanadamu hubandilisha nia na akili yake.
  • Mwanadamu anangeuka na kubandilika, ahadi zake si hakika.
  • Magazeti, radio na runinga (television) zilibuniwa kwa sababu mwanadamu anabandilika.
  • Leo mwanadamu anasema hivi, kesho vile, ndio bibilia inasema “na amelaniwa mtu amtegemeaye mwanadamu” (Yeremia 17:5).
  • Kuna mambo mengi mimi sina hakika nayo.
  • Sina hakika jinsi ya ni wapi nitakufa.
  • Dunia hii tunayoishi ni mahali pa shida na kukosa hakika ya mambo mengi sana.
  • Bila Mungu hamna tumaini, sasa hivi corona imetukosesha hakika, hatujui corona hii itakwisha lini, hatujui shule, makanisa na biashara zitafunguliwa lini.
  • Lakini kwa kila mtu anayemtumainia Mungu, kukosa hakika ni sawa kwa sababu Mungu yupo katika uongozi, hio ndio ujasiri wetu. (God is in control)
  • Katika (II Wakorintho 1:20) “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni amina, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”
  • Neno “amina” lilianza katika sinagogi la wayahudi wakati wa uamisho wa Babeli , mtu anapo omba au kusoma kifungu cha maandiko. Watu wote walisema “amini.”Baadaye kanisa ilipoanza wakristo wakafuata na pia islami na wao wakafuata. Baadaye “amini” ilita fsiriwa kutoka Kiebrania, Kigiriki, Kilatini, Kiingereza na lugha zote duniani (“amini, amueni, amina”)
  • Amini, maana yake ni kuamini (Trust or Faithfulness).
  • Baadaye maana ya ‘amini’ ikawa ni hakika, kweli, amani; tegemeo na ujasiri.
  • Ahadi za Mungu ni hakika, kamilifu, pamoja, zinajenga na zina marsharti.
  • Tumaini ni kitu unachopata kwa mda kupitia ujuzi.
  • Kwa miaka ile nimemtegemea Mungu nimemwona akiwa mwaminifu kwangu binafsi.
  • Mungu anasema na kutenda yeye ni mwaminifu.

II.  AHADI ZA MUNGU NI KAMILIFU (KATIKA MAMBO YOTE)

  • Hapa Biblia inasema “katika mambo yote, Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema.”
  • Kila jambo umepitia na jambo lolote utakalopitia jumla yake ni “mema”
  • Mambo yote mazuri na mbaya yatakapo jumulishwa yatakuletea – MEMA – maana Mungu yupo juu ya yote. (God is sovereign in everything and He is in control – even in Covid-19) katika (Mithali 16:4) “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake, naamu, hata wabaya kwa siku ya   ubaya.”
  • Ayubu aliyapitia majaribu mengi sana, lakini mwishowe Mungu alikuwa katika uongozi (Ayubu 1:9-12)
  • Mungu aliruhusu shetani, waseba, wakaldayo, dhuruba na upepo mkali kuaribu mali yake na watoto wake wote.
  • Mungu aliruhusu afya ya Ayubu kuaribika lakini, mwisho tunaona Mungu alikuwa na mpango katika majaribu ya Ayubu (Ayubu 42:5)
  • Baada ya majaribu ya Ayubu, Ayubu alimjua na kumfahamu Mungu na uwezo wake kibinafsi.
  • Hakuna kitu chochote ambacho kiko mbali na uwepo wa Mungu, hata coronavirus.
  • Hata shetani alikuwa chini ya nguvu za Mungu
  • “Katika mambo yote” maanake ni kwamba hakuna jambo ambalo liko inche ya uwezo wake na ambalo litafanya kinyume na mema kwetu.

III. AHADI ZA MUNGU NI KAMILIFU (MUNGU UFANYA PAMOJA)

  • Tazama, Biblia haisemi kwamba kila jambo ni nzuri hau njema.
  • Lakini kila jambo Mungu anafanya pamoja na wale wampendao.
  • Kuna mambo mengi yanafanyika kwetu yasio mema – ni mabaya.
  • Lakini mabaya yanafanywa na kuchanganywa na mema kwa jumla yote yanaleta mema!
  • Mambo yaliyofanyika kwa Yusufu hayakuwa mema, lakini Mungu alifanya pamoja na Yusufu kuleta mema kwake na jamii yake (Mwanzo 50:20)
  • Unapochukua kila ubaya peke yake unaona mbaya, lakini tunapochukua yote, Mungu anayafanya MEMA.
  • Keki ni mchanganyiko ya vitu vingi, unga, sukari, mafuta, mayai, chumvi, powder, machungwa, malimao na kadhalika.
  • Kama ukila kila kitu pekee, hamna utamu, lakini wakati vitu vyote vimepikwa pamoja unaona keki ni jema zaidi.
  • Pengine haupendi yale yanafanyika ndani yako sasa kwa sababu unapokea moja moja – lakini yote pamoja yatakuwa mema.

IV.  AHADI ZA MUNGU NI ZA KUTUJENGA (KWA MEMA)

  • Mambo yote yanafanya pamoja kwa wema wetu
  • Baada ya mambo yote itakuwa Baraka uenda sasa waona mbaya tu, lakini siku moja utaona ni mema kwako.
  • Hadithi yaelezwa ya mtu ambaye meli yake ilizama baharini yeye mwenyewe akajaribu kuogelea mpaka kiziwa kimoja. Akajenga nyumba ndogo, baada ya siku ile nyumba iliwaka moto. Baharia akalia sana na kusema Mungu amemwacha, lakini moshi wa kuteketea kwa nyumba yake ukavutia meli zingine na ndege, hivyo akaokolewa hakufa – mema yakamjia.
  • Wakati mwingine mema ya mambo yote tutayaona tukiwa hapa duniani, la si hivyo tutayaona tufikapo mbinguni.

V.  AHADI ZA MUNGU ZINAMASHARTI YAKE (KWA WALE WAMPENDAO MUNGU, WALIOITWA KWA KUSUDI LAKE)

  • Ukweli wa tano juu ya ahadi za Mungu ni kwamba ahadi zake zinaomasharti.
  • Mambo yote yanafanya pamoja na kuleta mema yanapokuwa katika mpango wa Mungu.
  • Kama bado hujaokoka, basi hauna uhusiano na Yesu Kristo kwa hivyo mwisho wako si mwema na njia yako haina mema.
  • Unapomtoa Yesu Kristo dani ya maisha yako kila jambo inabandilika.
  • “Nasi twajua ya kuwa katika yote Mungu hufanya kazi pamoja wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.”
  • Hii ndio Ahadi ya Mungu kwetu sisi zote.
  • Pengine unanisikiza na kunitazama na wewe bado haujafahamu jinsi Mungu anaweza kuleta mema kutoka kwa mabaya.
  • Pengine unasema coronavirus imevunja biashara yako ya hoteli, shule, kanisa, transport hau kazi yako.
  • Je, ni mazuri gani inaweza kupatikana katika majivu hayo.
  • Ni maombi yangu Mungu atajifunua kwako leo.
  • Lakini leo, shika ahadi za Mungu kwa karibu sana.
  • Weka mkono wako katika mkono wake umtengee yeye peke yake.

MWISHO

  • Wakati huu wa coronavirus wengi wetu twauliza, je, Mungu anaelewa na shida zetu?
  • Yeremiah alisema katika (Maombolezo 3:31-33) “kwa maana Mungu hatamtupa mtu hata milele maana anapomhuzunisha atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha.”
  • Matokeo ya coronavirus kwetu inahitaji kuwa kutembea na Kristo kwa karibu zaidi kwa waliokoka.
  • Na kuokolewa wewe bado kuokoka – liite jina lake leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *