MFULULIZO: TUMAINI HAI
SOMO: 1 PETRO 3:18-22.
Leo tunatazama kifungu kigumu zaidi katika Agano Jipya. Kumbuka Petro akiwaandikia kanisa lilikuwa katika dhiki kuu. Hawa Wakristo walitapakaa mbali wakihofia maisha yao chini ya utawala wa mfalme Nero yaani Kaisari wa Roma. Hawa Wakristo walikuwa wamepoteza yote, nyumba, biashara, jamii na nchi yao. Kweli hawa walikuwa katika mateso na dhiki nyingi mno. Petro amewaandikia ili awape tumanini hai. Petro anawaeleza kwamba Kristo aliwatesekea sana zaidi ili wapate kuokoka.
Petro anawaeleza mateso ya haina mbili.
- Kuteseka kwa sababu ya dhambi na makosa-Wagalatia 6:7-8.
- Kuteseka kwa sababu ya kufanya mema.
Katika kifungu cha (V. 18) Petro anatueleza yale Kristo alitutendea (3:18-22).
Petro anatueleza mambo matatu Yesu Kristo alitenda kwa ajili ya kila mmoja wetu:-
YESU KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YETU-1 Petro 3:18.
- Kwa sababu ya kifo cha Yesu Kristo msalabani, Petro anatueleza:-
Kifo cha Yesu msalabani kilikuwa cha ajabu-(Vs. 18) (mara moja).
- “Kristo aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi.”
- Kifo cha Yesu Kristo hakiwezi kurudiwa mara nyingine!! Kifo chake ni mara moja tu kwa historia.
- Katika Agano la Kale dhabihu ilitolewa kila siku, kwa sababu dhabihu hizo hazikuwa kamillifu na za kutosha.
- Yesu Kristo alitoa dhabihu kamilifu, takatifu, ya kipekee-Waebrania 7:27.
Kifo cha Yesu Kristo kilikuwa sadaka.
- Petro anasema “Kristo aliteswa mara moja” kwa ajili ya dhambi.
- Kristo hakufa kwa ajili ya dhambi zake lakini dhambi zetu.
- Kristo hakujua dhambi, hakufanya dhambi hata moja.
Kifo cha Yesu Kristo kilikuwa kwa ajili yetu.
- “Mwenye haki kwa ajili ya wasio haki.”
- Yesu Kristo alichukua mahali petu, alichukua dhambi, laana, aibu na dhiki zetu.
- Kristo alibeba dhambi zetu katika mwili wake kwa ajili yako!!
Kifo cha Yesu msalabani kilikuwa patanisho.
“Ili atulete kwa Mungu.”
- “Atulete” Maanake ni “atukabidhi kwa Mungu,” Atujulishe kwa Mungu.
- Yesu Kristo anatujulisha kwa Mungu Baba. Tunajulikana na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo kwa damu yake iliyomwagika kwa ajili yetu.
- Sasa tumepatanishwa na Mungu, sasa hakuna tena uasama katikati yetu na Mungu wetu.
- Sasa hatuna vita na Mungu, tumefanyika kuwa wana wa Mungu kwa damu yake Yesu Kristo.
- Sasa tumekubalika mbele zake Mungu wa mbinguni.
- Sasa sisi si wageni mbele za Mungu na mbele za malaika wake.
YESU KRISTO ALITANGAZA USHINDI WAKE MSALABANI-1 Petro 3:19-20.
- Vifungu hivi viwili vimeleta tafsiri majadiliano zaidi ya (19).
- Wakatoliki (catholics) wanatumia kifungu hiki kufundisha mambo ya (Purgatory).
- Watu wa sabato (SDA) wanafundisha juu ya nafsi kulala (soul asleep).
- Mormons na wao wanabatiza kwa niaba ya wafu.
- Katika kanuni za tafsiri ya vifungu ngumu kuna kanuni mbili:-
- Kifungu ngumu kisitumiwe kufundisha doctrines au mafundisho ya msingi.
- Usifundishe kifungu ile ngumu nje ya mafundisho dhairi (out of context).
- Petro anasema Yesu Kristo alipokufa msalabani na kuzikwa kaburi, Roho yake ilienda kuhubiria “maroho yaliyo kuwa kifungoni,” Roho waliokaa kifungoni.
- Kulingana na Petro wakati kati ya kifo cha Yesu Kristo na kufufuka kwake, Kristo alifanya tangazo (Kerusso) katika kifungo au gereza la pepo.
- Maswali tatu yanaibuka kutoka kifungu cha 19:-
- Je, Yesu Kristo alienda wapi?
- Je, Yesu Kristo alienda kwa nani?
- Je, Yesu Kristo alitangaza nini kwao?
Je, Kristo alienda wapi?
- Kumbuka 1 Petro 3:19 imeandikwa katika maombi ya mitume-Apostles creed. Yesu Kristo alienda (aliteremka kuzimu).
- Lakini hakuna mahali popote katika Biblia Yesu kristo alizuru jehanamu.
- Katika Matendo 2:31, Yesu Kristo alitembea Hades (mahali pa roho za wafu). Hades si kuzimu.
- Hades mahali pa muda mfupi-kuzimu ni mahali pa kudumu (permanent).
- Kabla ya kufufuka kwa Yesu Kristo kulikuweko na mahali kuwili Hades na Paradiso, mahali roho za wafu zilienda.
- Lakini Yesu alipofufuka paradise yote iliamishwa mpaka mbinguni-Waefeso 4:8-9.
- Kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kuligeuza kila jambo ulimwenguni na mbinguni.
- Leo mtu aliyeokoka akifa anaenda mara moja mbinguni kukaa na Mwokozi Yesu Kristo-Wafilipi 1:20-24.
Je, Yesu alienda kwa nani?
- Aliwahubiri “roho waliokoka kifungoni.”
- Yesu Kristo alihubiria roho za wafu. Kwa kawaida “roho” ni za malaika, “nafsi” ni za wanadamu.
- Yesu Kristo alihubiri kupitia Nuhu. Kwa wale waliofungwa kwa sababu ya kuasi mbele ya ile gharika ya Nuhu.
- Hapa Nuhu anatumika kama mfano.
- Roho alizohubiria Kristo ni roho za malaika walioasi Mungu-Mwanzo 6:1-8.
- Linganisha wazo hili na 2nd Petro 2:4-5; Yuda 6-7.
- Yesu hakuwahubiria pepo “roho” ili wapate kuokoka maana wokovu si kwa malaika. Alihubiri, aliwatangazia (proclaim) ushindi wake juu yao.
Je, Yesu Kristo aliwatangazia nini?
- Yesu Kristo hakuwahubiri wokovu, kwa maana hakuna nafasi ya pili (second chance)-Waebrania 9:27; Luka 16:26.
- Yesu aliwatangazia ushindi wake juu yao kupitia msalaba.
- Yesu aliwatangazia kwamba “shetani ameshindwa, nguvu za shetani alizishinda Yesu Kristo.”
- Yesu Kristo kama jinsi hakimu alisema uamuzi wa korti ya mbinguni-kwamba shetani ameshindwa, kifo kimeshindwa, nguvu za shetani zimeshindwa, pepo zote zimeshindwa.
YESU KRISTO AMETUKOMBOA KUTOKANA NA HUKUMU-1 Petro 3:20-21.
- Kwa miaka hizo Nuhu aliwahubiria watu wa kizazi chake juu ya hukumu itakao kuja.
- Gharika ilipokuja jamii ya Nuhu pekee ndio iliingia katika ile safina.
- Nuhu alitumia miaka yake yote kujiweka tayari kuingia milele (eternity).
- Ubatizo hauwezi kuokoa mtu yeyote, lakini ubatizo ni ishara kwamba tumekufa pamoja na Kristo, tumezikwa pamoja naye, tumefufuka pamoja naye kwa upya wa uzima.
- Mtu anapookoka sharti kumfuata Yesu Kristo kwa maji ya ubatizo kama ishara ya neema ya Mungu. Ubatizo huu ni ubatizo ya waamini (Believers baptism).
MWISHO
- Kwa sababu Yesu Kristo alishinda mauti na kaburi, hatuna haja ya kuogopa kifo.
- Kwa sababu Yesu Kristo alilipa deni ya dhambi, kazi ya ukombozi na wokovu ilikwisha kabisa.
- Kwa sababu Yesu Kristo alimshinda shetani kabisa, shetani ni adui aliyeshindwa kabisa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
- UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI. - October 19, 2025
- THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR. - October 19, 2025
