Swahili Service

ANA-ALIUTARAJIA UKOMBOZI WA ISRAELI.

SOMO: LUKA 2:36-38.

 

Kuokoka ni kuishi maisha ya kutarajia ukombozi wa Mungu. Mungu anawabariki wanaomtarajia Mungu katika kuomba kwa kufunga na kuomba. Katika ibada ya kingereza tunatazama maisha na kazi ya Simioni. Simioni na Ana ni watu wawili wasio ubiriwa sana wakati huu wa Krismasi.

Leo tunatazama maisha na huduma ya Ana mke nabii. Simioni na Ana walitarajia sana kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo. Mara kwa mara tunakumbuka mamajuzi na wachungaji kondoo, lakini Simeoni na Ana wanasahaulika sana. Basi wacha nikualike Yerusalemu katika hekalu na tukutane naye Ana aliyeutarajia ukombozi wa Israeli. Hebu tuone:-

UMRI WAKE ANA-Luka 2:36-37.

  • Kwanza tuone neno tunalopewa juu ya Ana mke nabii wa Mungu.
  1. Maana ya jina lake Ana ni “Neema” “Grace.”
  • Ana alikuwa Binti ya Phanueli na maana yake Phanueli ni “maono ya Mungu” “Vision of God.”
  1. Biblia inaeleza kwamba Ana alikuwa mke nabii, cheo cha juu zaidi katika huduma.
  • Ana anawekwa pamoja na waliochaguliwa kama jinsi Miriam dadake Musa na Deborah aliyekuwa mke muamuzi katika Israeli.
  • Ana ni mmoja wao, watu Mungu anapendezwa kufanya kazi nao. Mungu anaongea na watu kama Simeoni na Ana.
  • Tunaelezwa kwamba Ana alikuwa Binti wa Phanueli katika kabila la Asheri.
  • Asheri ni moja ya kabila za Israeli zilizopotea tangu uamisho wa Assyria mwaka wa 806 B.C.
  • Katika mwaka wa 1930 kuna mafundisho yaliosema kwamba makabila mengi ya Europa kama jinsi Uingereza (British) Scandinavia, German, Dutch, Canada na Amerika, New Zealand na Australia na South Africa ni yale makabila 10 ya Israeli.
  • Mafundisho hayo yanazidi kusema nyumba ya ufalme ya uiengereza imetoka na ufalme wa Daudi. Uenda ikawa.
  • La muhimu sana ni kwa hapa tunapata moja wa wazaliwa wa kabila la Asheri aliyebaki Yerusalemu mpaka kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  • Mungu ndiye ajuaye hawa makabila 10 ya Israeli wako wapi. Tunaelewa kwamba wakati wa dhiki kuu makabila yote ya Israeli watahusika katika kuhubiri Injili 12,000 kutoka makabila yote 12 (144,000).
  • Wanawake wa kabila ya Asheri walikuwa ndio warembo zaidi katika Israeli.
  • Mpaka leo Asheri wanawatoa warembo zaidi duniani.
  • Biblia inatueleza kwamba Ana alikuwa mzee wa miaka.
  • Ana aliolewa kwa miaka saba (7) na alikuwa mjane kwa miaka 84 (91). Tukiongeza miaka ya ujana wake (14) Ana alikuwa na miaka 105 wakati alipomwona Kristo Bwana.
  • Tunampata Ana hekaluni akiwa mikaka 105!! Ana angali anangojea ukombozi wa Israeli katika uzee wake.

UPWEKE WA ANA-Luka 2:37.

  • Kila neno na kila jina katika Biblia linao pumzi ya Mungu. Luka anasema “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana.”
  • Maisha ya Ana yalikuwa maisha ya huzuni mwingi.
  • Ana aliolewa na kukaa kwa ndoa miaka saba pekee (7). Mume wake aliaga dunia.
  • Ana aliachwa akiwa miaka “21.”
  • Pamoja na ujana, na urembo wake Ana aliamua kuishi bila mume mpaka siku ya kufa kwake!!
  • Ana alichagua njia ngumu ya kuishi pekee na katika utakatifu, huku anaomba na kufunga usiku na mchana.
  • Ana alidhubutu kuishi pekee, akiutafuta uso wa Mungu na kutarajia ukombozi wa Israeli.
  • Ana alijitoa kwa Mungu kabisa na kuishi katika upweke kwa miaka 84.
  • Kuishi maisha pweke, bila kuoa na kuolewa si jambo la kila mtu.
  • Si mapenzi ya Mungu kila mtu kuolewa au kuoa, lakini kuna wale wamechagua kuishi pekee katika utakatifu kwa ajili ya utumishi wa Bwana.
  • Mtu asiyeoa anaweza kumtumikia Mungu kwa njia nzuri kaliko aliyeoa-1st Wakorintho 7:32-35.
  • John Westley wa kanisa la Methodist, kwa kazi nzito ya Injili aliachwa na mke wake.
  • Pia mwanamke asiyeolewa anaweza kumtumikia Mungu vizuri zaidi kuliko yule ameolewa-Vs. 34.
  • Lakini kuoa au kuolewa si dhambi-Waebrania 13:4.
  • Ana alitumika miaka 84 katika hekalu bila shaka.

UTUMISHI WAKE ANA-Luka 2:37-38.

Ana alimtumikia Mungu kwa kuomba na kufunga.

  • Maombi ndio huduma ya juu zaidi katika kumtumikia Mungu. Huduma ya maombi ni maana zaidi kuliko kuhubiri, kufundisha na huduma zingine zote.
  • Simeoni na Ana walielewa Mungu alikuwa ametoa ahadi ya Mkombozi kuifariji Israeli na kuwaokoa watu na mataifa.
  • Simeoni na Ana walitarajia Mungu kutimiza ahadi zake.
  • Waliomba wakitazama unabii.
  • Ana alitumia miaka yake 84 kwa kuomba, aliomba pamoja na kufunga.
  • Kuna watu wengi katika Biblia walioomba na kufunga saumu, wengine walifunga siku moja-Waamuzi 20:26, usiku moja Danieli 6:18, wengine kama Musa alifunga siku 40-Kutoka 34:28; Eliya 40-1st Wafalme 19:8, Yesu Kristo-Mathayo 4:2-40.
  • Kila wakati kufunga kunakuja mbele ya maombi-kufunga ni kujiweka tayari kwa maombi.
  • Kufunga si njia ya kumlazimisha Mungu kutenda, lakini nbi ili mapenzi ya Mungu kutendeka.
  • Kufunga saumu ni njia ya Mungu mwanadamu ajitoe na kutazama Mungu.
  • Ana alifanya maombi kuwa kazi yake na Mungu alimzawadia Ana.
  • Ana alimtumikia Mungu kwa kumsifu na kumtolea dhabihu ya sifa-Vs. 38.
  • Ana aliendelea kumsifu Mungu na kutangaza kwa wote waliotarajia ukombozi wa Mungu mle Yerusalemu.

MWISHO

  • Maanake Krismasi ni kutarajia ukombozi wa Mungu kwa mataifa na faraja kwa Israeli.
  • Krismasi ni kuwaeleza watu habari za Yesu Kriso, yaani Injili.
  • Sisi nasi kama jinsi Simeoni na Ana tunaishi nyakati za hatari.
  • Je, Krismasi hii, utawatangazia wote na wa jamii yako Injili ya Yesu Kristo?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *