LUKA 2:36-38
Ana ni moja wao aliyechangia pakubwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Leo tutazame maisha ya Nabii Ana. Ana kwa siku moja aliyatimiza mapenzi ya Mungu pamoja na kutimiza hatima ya maisha yake. Ana alipata mikosi katika maisha Yake, lakini kwa Imani Ana aliyashinda yote. Ana ni kielelezo chema cha jinsi ya kuishi kwa Imani. Ana hau Hanna maana yake jina ni Neema hau mweye kuneemesha. Babaye Ana alikuwa Fanueli wa kabila la Asheri. Fanueli ni jina ambalo Yakobo alipaita mahali alipo shindana mweleka na Mungu (Mwanzo 32:24). Maana yake Fanueli ni “uso wa Mungu”. Asheri maana yake ni “furaha”. Asheri alikuwa mwana wa nane wa Yakobo kwa wana 12 (Mwanzo 30:13)
Yakobo alipowabarikia wanawe kabla ya kufa kwake, alimsema Asheri “Asheri chakula chake kitakuwa kinono naye atatoa tunu za kifalme” (Mwanzo 49:20) naye Musa alimsema Asheri “Asheri abarikiwe kwa watoto, na akubaliwe katika nduguze, na achovye mguu wake katika mafuta.” (Kumbu kumbu 33:24). Asheri walikuwa kabila la kubarikiwa na mali na kuzaa watoto wa kifalme. Yoshua naye aliwapatia Asheri inchi nzuri sana kuwa urithi na miiki yao, karibu na bahari ya kati. Wanawake wa Asheri walikuwa warembo zaidi hivyo wakaolewa na wafalme! (Yoshua 19:24-31). Lakini kwa Baraka hizi zote Asheri aliishi katika majaribu mengi sana – waliendelea kuishi pamoja na wakanaani (Waamuzi 1:31-40) muamuzi Debora aliwanena Asheri (Waamuzi 5:17). Asheri alikuwa na imani Dhaifu, mambo ya kiroho hayakumpendeza Asheri. Hakupenda vita vya kiroho. Baadaye Asheri walichukuliwa mateka katika uamisho, hata ingawa hivyo pale Yerusalemu palikuwa na Ana—nabii mke, binti yake Fanueli mtu wa Asheri!! Neema yake Mungu inaenda upande upande kwa mataifa yote. Hebu tutazame:-
I. ANA ALIYABANDILISHA MAOVU KUWA MEMA (TURNING NAGATIVES INTO POSITIVES) KWA IMANI.
- Kuwapo kwa Ana Hekaluni mle Yerusalemu kwa onyesha maajabu ya uaminifu wa Mungu.
- Ana alikuwa mabaki ya kabila lake, mwenye Imani wakati kabila lake Asheri walimwacha Mungu wao.
- Ana kama Simeoni aliishi kwa kutarajia na kungojea wokovu wa Bwana.
- Imani ya Ana inaonekana katika machache yaliyoandikwa na Luka.
- Ana alikuwa mjane wa miaka 84. aliolewa akiwa miaka 14, na akaishi na mme wake miaka 7 hivyo Ana alikuwa na miaka 105. aliachwa na mme wake akiwa na umri wa miaka 21.
- Ana angeolewa tena lakini aliamua kumuishia Mungu na kumtumikia katika maombi na kufunga saumu.
- Biblia inasema ANA “haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
- Wakati wa biblia mme alikuwa ni bima ya mwanamke hivyo kufiwa na mume kuliacha mjane katika mikono ya wezi (social parasites or parasites of society)
- Pamoja na sheria ya Musa, waisraeli waliwanyanyasa wajane sana, kama Kenya ya leo (Ayubu 22:8-11, 24:2,21)
- Ana alijiolesha kwa Mungu (I Wakorintho 7:29-35).
II. ANA ALIJIFICHA HEKALUNI (ZABURI 68:5, 146:9
- Ana alijua Mungu na kao lake takatifu. Ana alipofiwa na mme wake mlinzi wake, Ana alimkimbilia mme wa kweli yaani Yehova. Ana alikaa katika nyumba ya Bwana wake, haondoki.
- Usiku na mchana, siku baada ya siku, kwa miaka 84. Ana aliomba na kufunga kwa ajili ya watu wake Asheri.
III. ANA ALITANGAZA UWEPO WA BWANA HEKALUNI.
- Ana alimshukuru Mungu na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu.
- Ana aliwatolea wengine habari zake Mkombozi Kristo.
- Haijalishi mda ulipongojea ahadi za Mungu kwako, haijalishi jinsi hali yako ilivyo mbele ya macho ya watu wengine, mtafute Bwana, jifiche katika uwepo wake, watangazie wengine habari zake. Siku moja tu, Ana alimwona Mwokozi wake.
MWISHO
- Ana alikuwa mke Nabii, hakupoteza Imani yake juu ya miaka mingi, Ana hakupatwa na machungu ya moyo hata kwa kufiwa na mme wake. Ana alikuwa mwombezi 24/7. Ana alimtambua Kristo, akashukuru. Ana alitangaza habari hizi kwa wote walio mwamini Mungu.
- Katika hali yote endelea kutembea na Bwana mpaka mwisho.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025

Ana nabii mke aliamua kukaa hekaluni na kuomba bila kukoma juu ya Bwana. Kwa maana hiyo alikuwa anatayarisha mazingira bora kabisa ya ujio wa Kristo na maisha yake ndani ya kukataliwa.
Jina la Bwana libarikiwe. Asante kwa neno hili
Najifunza kuzingojea ahadi ya Mungu Kwa kuomba bila kukata tamaa kama Nabii Ana