Swahili Service

BWANA ANAKAA KATIKATI YA KANISA LAKE

MAKANISA SABA YA UFUNUO

UFUNUO 1:9-20

Huu ni ujumbe wa utangulizi katika mfululizo wa ujumbe juu ya Makanisa saba ya ufunuo.

  1. UTANGULIZI-KANISA KATIKA ULIMWENGU HUU.
  • Tunapoendelea katika ulimwengu huu kama kanisa, swali kuu ni “Je, kanisa litakuwa nini ulimwenguni?”
  • Ni jambo la maana sana kwa kila aliye kanisani kutambua yeye ni nani na kitambulisho chake, kwamba sisi ni wageni na wapitaji katika dunia ya chuki.
  • Janga hili limetufundisha kwamba, kanisa la kweli la Yesu Kristo liko katika dhoruba na mashaka mengi katika siku zijazo.
  • Hapa kwetu Kenya, kwa muda mwingi uliopita, serikali imekuwa na wazo la jinsi ya kusimamia kanisa na kuiongoza. Tangu wakati wa Rais wa kwanza mpaka leo, lengo limekuwa kusimamia na kuongoza kanisa.
  • Iwe ni wakati wa Njonjo, Wako, Muingai na wakati huu wa Mkuu wa sheria aliyoko sasa, lengo ni kuiongoza kanisa na shughuli zake zote.
  • Janga hii imetumika kutimiza lengo la siku nyingi.
  • Shida kubwa ni kwamba serikali itatumia wakuu wa madhehebu na dini kuweka sheria za kudhulumu kanisa.
  • Hivyo kanisa litajinyonga na kamba lake lenyewe kama jinsi leo.
  • Tume la dini juu ya janga hili limeweka sheria za kuua na kuvunja kanisa.
  • Baraza za Magavana Kenya, pia wametokea na sheria na amri 38 za kanisa kutii.
  • Baraza la dini nalo limekubali kuwa makachero wa serikali kutekeleza sheria juu ya kanisa la Kristo.
  • Hii ni baada ya Kenya Bureau of Standards kujaribu kuvunja Injili ya mtaani.
  • Janga hii tulionayo imetufundisha watoto wa Mungu kuwa na hakika ya wokovu na Imani timilifu ndani ya Kristo.
  • 1 Petro 2:11-“Wapenzi nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tama za mwili zipiganazo na Roho.”
  • Waebrania 11:16- “Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani ya mbinguni. Kwa hivyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao, maana amewatengenezea mji.”
  • Waebrania 13:13-14 “Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.”
  • Kwa muda mdogo, kanisa la Kenya limefurahia uhuru na ibada na dini, hivyo kanisa la Kenya haliko tayari kwa vita kuu ijayo juu ya kanisa kweli la Kristo.
  • Kanisa la karne ya kwanza lilizoea shida na mateso.
  • Kanisa la kwanza liliteswa, kuchukiwa na kudharauliwa wakati wa Kaisari wa ufalme wa Roma.
  • Kisiasa walichukuwa kwa maana walikataa kumwabudu kaisari kama mungu (Emperor worship).
  • Kidini walichukiwa kwa sababu walikataa kuabudu na kuitumikia miungu na sanamu za ufalme wa Roma.
  • Ki-uma walichukiwa kwa sababu hawa Wakristo walitoka kwa watu wa chini sana kiuchumi na kukataliwa na matajiri wa Roma.
  • Kiuchumi, Wakristo wa kwanza walichukiwa na makuhani wa kipagani na wenye biashara kwa maana Wakristo walipinga sana kutumia sanamu katika ibada zao.
  • Wakristo wa kwanza walizungukwa na dhambi za kila haina. Ufyaji mimba, uasherati, utumwa, utawala m’baya, hivyo Wakristo walikuwa adui wa ulimwengu mzima.
  • Kwa sababu ya uadui, Wakristo wengi waliteswa na kuuawa.
  • Stefano alipigwa mawe, Yakobo alikatwa kwa upanga, Filipo alisulubiwa msalabani, Mathayo aliuliwa Ethiopia, Yakobo mdogo akiwa umri wa miaka 94 alipigwa mawe na kupingwa na Wayahudi, kisha wakamkata kichwa na kichwa chake kuvunjwa-vunjwa kwa mawe.
  • Mathiasi alipigwa mawe na kisha kukatwa shingo lake.
  • Andrea alisulubiwa, Marko aliuliwa kwa mitaa ya Alexandria, mle Misri.
  • Petro na mke wake walisulubiwa vichwa chini siku moja.
  • Paulo alikatwa kichwa na Yuda alisulubiwa.
  • Batholomayo alisulubiwa, Tomaso (Thomas) aliuliwa India akihubiri Injili.
  • Luka naye alinyongwa juu ya mti wa mzeituni.
  • Simoni alisulubishwa kule uengereza.
  • Yohana pekee alikufa kwa uzee wake.
  • Wanawake kama Amphianus aliteswa mpaka kufa, Julitta aliuliwa kwa kuwekwa kwa mafuta yaliochemka!!
  • Basi hiyo ni kanisa la Karne ya kwanza, walivumilia mateso mengi.
  • Hivyo, kanisa la karne ya 21, litapita katika mateso kupitia kwa sheria kama zile za magavana wa Kenya wiki hii.
  • Je, tutaishije panapo mateso na kukatisha huduma kwa sababu ya umri wetu?
  • Katika makanisa saba ya ufunuo, kanisa lenye kuzaa matunda lilikuwa na Uungu, mafundisho safi, walimu wenye tabia nzuri, ibada safi, nidhamu katika maombi na utakatifu.
  • Yesu Kristo yupo katikakati ya kanisa lake. Je, Kristo anaona kitu gani katika kanisa letu?
  1. KAZI YA BWANA YESU KRISTO KATIKA KANISA LAKE
  • Tunapotazama sana kiitabu cha Ufunuo twaona:-
  1. Kazi ya Kristo katika kanisa lake (Ufunuo 1)
  2. Neno la Kristo kwa kanisa lake (Ufunuo 2-3)
  3. Unabii wa Kristo kwa kanisa lake (Ufunuo 4-22)
  • Yohana mtume alikuwa mtume wa mwisho kuishi.
  • Yohana mtume alishuhudia kanisa la Karne ya kwanza mpaka mwisho.
  • Yohana alistaajabu kwa makanisa mengi yalikuwa yameasi na kumwacha Mungu.
  • Generali Tito aliaribu Yerusalemu 70AD.
  • Generali Tito alikuwa na ndugu yake kwa jina Domitian.
  • Generali Tito alikuwa mshupavu wa vita, chini ya Baba yake Kaisari Vespasian. Lakini kabla ya Tito kuingia katika mamlaka kama kaisari alipata ugonjwa na akafa.
  • Domitian akachukuwa mamlaka kama kaisari.
  • Domitian alikuwa kaisari m’baya sana. Yeye pamoja na kaisali Augusto walikuwa kaisari wa kwanza kuamrisha watu wa Roma kuwaita wao “Bwana na Mungu.” Wakristo wengi waliuliwa maana walikataa kumwita kaisari ‘Bwana na Mungu” kwa sababu Yesu Kristo alikuwa Bwana wao.
  • Mtume Yohana alikataa kumwabudu kaisari hivyo akaamishwa kwa kisiwa cha Patmo.
  • Kazi ya Mtume Yohana akiwa miaka 90 katika kiziwa cha Patmo ilikuwa kukata na kuvunja mawe kama kufungwa.
  • Ufunuo 1:9-“Mimi, Yohana ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.
  • Hapa Patmo ndipo Yohana aliona ufunuo wa Yesu Kristo na akaandika kitabu cha Ufunuo!!
  • Katika Ufunuo 1:9-20- Yohana alipokea ufunuo wa kwanza.
  • Yohana ameruhusiwa kuona Bwana Yesu Kristo. Ameona nyota saba na malaika saba.
  • Yohana ameelezwa hawa malaika saba ndio wachungaji wa yale makanisa saba. Yohana pia ameona vinara saba ambayo ni yale makanisa saba katika Asia.
  • Katika maono hayo, Yohana alimwona Yesu Kristo katikati ya vile vinara saba akitembea.
  • Maana yake ni kuonyesha kazi ya Kristo katika kanisa lake.
  • Yesu Kristo anafahamu kanisa lake, mateso na dhiki ya kanisa, hata leo Kristo anaona jinsi kanisa lake linapofanyiwa na mawaziri wa Afya na Ofisi ya Rais na usalama wa ndani hapa Kenya.
  • Kanisa la kweli hapa Kenya, Yesu Kristo yumo katikati yenu, anaona jinsi masharti ya ibada ni mengi, Mungu anaona!!
  • Yohana aliyaona mengi sana, ameona ndugu zake, mitume wakiuawa, ameona Yerusalemu ikiharibiwa na watu 100,000 wakiuliwa.
  • Yohana ameona hekalu likivunjwa.

 

  • Yohana sasa anaonyesha hali jinsi ilivyo katika makanisa ya Bwana.
  1. Efeso-Wanapoteza upendo wao wa kwanza.
  2. Pergamo –Uasherati na dhambi katikati ya kanisa.
  3. Thiatira-Dhambi na upagani.
  4. Sardi- Kanisa lilikufa kabisa.
  5. Smirna-Kanisa katika dhiki na umaskini.
  6. Laodokia-Kanisa vuguvugu.
  7. Filadelfia-Kanisa la milango wazi.
  • Je, Yesu Kristo anasema nini juu ya kanisa lenu na letu?
  • Je, Yesu Kristo anasema nini juu ya kazi zetu, mafundisho, utakatifu, Injili, na juhudi zetu?
  • Yohana kweli alikuwa katika dhiki kuu, katika mahali pabaya, Yohana alijua mambo yataendelea kuwa mabaya zaidi.
  • Lakini Yohana alikuwa katika Roho (Ufunuo 1:10) “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu kama sauti ya Baragumu.”
  • Ilikuwa ni siku ya Jumapili mle Patmo. Siku ya kwanza ya juma ni siku ya Jumapili, na kanisa kwanza liliabudu siku ya kwanza.
  • Siku ya kwanza ni siku ya Agano jipya.
  • Siku ya saba ndio siku ya Agano la kale na Musa na Torati.
  • SURA YA YESU KRISTO (Ufunuo 1:12-17)
  • Yohana alimwona Yesu Kristo katika utukufu wake.
  • Yesu Kristo alikuwa katikati ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu.
  • Yesu Kristo yupo katikati ya kanisa lake.
  • Mavazi yake ni marefu na meupe-Ukuu wake, utawala na ufalme wake. Ukuhani wa Kristo kwa kanisa lake ni dhahiri (Waebrania 4:15)
  • Kichwa na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji.
  • Macho yake kama mwali wa moto na miguu yake kama shaba, sauti yake kama sauti ya maji mengi.
  • Utakatifu wa Kristo unahitaji kuonekana katika kanisa lake.
  • Yesu Kristo ni Mze wa Siku ?(Ancient of days)-(Danieli 7:9, 13, 22).
  • Yesu Kristo ni wa milele, mtukufu, kweli na mtakatifu.
  • Macho yake ni kama mwali wa jua-hakuna kitu asicho jua juu ya kanisa lake(Mathayo 10:26, Waebrania 4:13)
  • Sauti yake ni kama sauti ya maji mengi-kama jinsi Owen falls, Thompson falls hau Niagara falls.
  • Katika mikono yake Kristo, ameshika nyota ambayo ni wachungaji wa kanisa lake.
  • Bwana ameweka heshima kubwa kwa wachungaji wa kweli.
  • Bwana atailinda kanisa lake kwa upanga wake.
  • Wale wamepanga kusumbua kanisa la Kristo, Bwana atasumbuana na wao.
  • Uso wa Bwana ni kama mng’aro wa jua.

 

  • Yohana alianguka chini yake Bwana mwokozi.
  • Danieli alianguka chini yake Bwana.
  • Isaya alianguka chini yake Bwana.
  • Ezekieli alianguka chini yake Bwana
  • Manoa na mke wake walianguka mbele zake Bwana.
  • Sauli alianguka chini yake Bwana.
  • Na wewe umefanya nini mbele yake zake?
  • Waebrania 12:28-29 “Basi kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa na m’we na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho. Maana Mungu wetu ni moto ulao.”

MWISHO

  • Tunahitaji Yesu Kristo katikati ya kanisa lake.

Je, umeokoka? Leo ni siku yako kumpokea Kristo na kuanguka mbele zake na kutubu dbambi

  • Leo, liitie jina lake na utaokoka
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *