MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI
SOMO: 1 SAMWELI 22:1-2; ZABURI 142:1-7; ZABURI 57:1-11.
Daudi alikuwa mpakwa mafuta (Masihi) mfalme wa pili katika Israeli. Shida ni kwamba mfalme Sauli angali mfalme Israeli na anamwinda Daudi apate kumuua.
Sauli aliishi katika dhambi na uasi hivyo baraka za Mungu na uwepo wake zilitoweka maisha ya Sauli.
Daudi alizidi kuwa hofu kwa mfalme Sauli. Watu walio na wivu wanakosa sana amani, usalama na furaha. Wivu ni hatari kwa maisha ya wengine. Kwa wivu watu wanauana.
Lakini naye Daudi alikuwa na kitu ambacho Sauli hakuwa nacho-Kibali cha Mungu na uvumilivu wa kumgojea Mungu na wakati wake.
Daudi alipata nafasi ya kumuua mfalme Sauli lakini alikataa sana kumdhuru mpakwa mafuta wa Mungu. Siku moja Daudi alikata mavazi ya mfalme Sauli katika pango, lakini alipata hukumu katika dhamiri yake-1 Samweli 24:5-6.
Kweli Daudi alikuwa mtu roho yake inamwelekea Mungu.
Hata katika kumkimbia Sauli, Daudi hakumkasirikia Mungu wake. Lakini aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu hata katika shida nyingi. Hebu leo tuone watu waliojeruhiwa pamoja na Daudi katika pango la Adulamu.
- Hapa Daudi ni mfano mwema wa Yesu Kristo. Aliwapokea watu wa kila haina waliomjia, hakuwatupa mbali naye-Mathayo 11:28-30.
- Tulipomjia Mwokozi wetu Yesu Kristo tulikuwa watu wabaya sana. Tulikuwa watu wa dhiki, wadeni na wengine tulikuwa watu wenye uchungu mioyoni mwetu.
- Tumekusanyika kwake Yesu Kristo, naye amekuwa Mwokozi, jemedari wetu.
- Hebu sasa tuwatazame hawa watu waliomjia Daudi pale Adulamu-1 Wakorintho 1:26-31.
WATU KATIKA HALI YA DHIKI (DISTRESS) 22:2.
- Hawa ni watu walioishi katika mateso na kufinywa.
- Hawa ni watu waliotumiwa vibaya na mfalme Sauli.
- Maumivu yao yalikuwa dhairi walipomjia Daudi mle Adulamu.
- Hawa walikuwa watu ambao ungewachukua katika jeshi lako.
- Hawakuwa na pesa na mali walikuwa maskini.
- Sisi nasi tulivyomjia Mwokozi wetu Yesu Kristo tulikuwa katika dhiki, tumenyanyaswa na shetani na mapepo.
- Tabia zetu zilikuwa duni, tulikuwa tumetupwa na dunia-tulikuwa katika dhiki.
- Tulikuwa mbali na Mungu wetu, lakini sasa tumemjia Mwokozi-1 Yohana 3:2.
- Daudi naye pia alikuwa na dhiki zake, lakini alijua jinsi ya kujitia moyo-1 Samweli 30:6, 18.
- Huwezi kumiliki vilivyo vyako mpaka kwanza kujitia moyo katika Bwana.
- Leta dhiki zako kwa Yesu Kristo maana Yesu anaweza-Waebrania 2:18.
WATU WALIOKUWA NA DENI-22:2.
- Hawa watu walikuwa wametozwa ushuru zaidi ya jinsi wangaliweza kulipa.
- Wakati wa zamani kodi ilikuwa shida kubwa kwa watu.
- Chini ya ukoloni hapa Kenya, kodi ilikuwa lazima.
- Riba nazo zilikuwa za juu zaidi, watu walichukuliwa kuwa watumwa kwa jinsi ya deni zao, watoto na wake za mtu wangechukuliwa utumwa kwa sababu ya deni-2 Wafalme 4:1-2.
- Wakati wa mfalme Sauli,wengi walipata kuwa maskini sababu ushuru ulikuwa juu zaidi. Mkopo nao ulikuwa na riba ya juu zaidi hivyo watu wakawa wadeni kiasi kukimbilia mbali.
- Sisi nasi tulikuwa wadeni tulipomjia Yesu Kristo.
- Deni ya dhambi zetu, deni ya makosa.
- Yesu Kristo alilipa deni ya dhambi zetu msalabani.
- Adui yetu shetani anawatoza watu ushuru wa juu zaidi. Dhambi ni deni kubwa. Dhambi ni bwana mkali zaidi.
- Tulipomjia Kristo, amekuwa kiongozi mkuu wa wokovu wetu-Waebrania 2:10.
- Hivyo tulimjia Kristo tukiwa katika dhiki na madeni.
WATU WALIOKUWA NA UCHUNGU MIOYONI MWAO-22:2.
- Mfalme Sauli hakuwa pale kutumikia wake, bali kutumikiwa.
- Watu walikuwa na uchungu mioyoni mwao.
- Watu wanapata kuwa na uchungu kwa sababu matarajio yao haijafikiwa na kutimizwa.
- Watu wapata kuwa na uchungu moyoni kwa sababu malengo yao yamegonga mwamba.
- Watu walikuwa na matumaini na matarajio mengi juu ya mfalme wao-1 Samweli 8:1-22.
- Tulipomjia Yesu Kristo tulikuwa na uchungu mioyoni mwetu.
- Tulijaribu sana kupata raha na amani kupitia pesa, pombe, mapenzi, sifa lakini zote zilituangusha mioyo ikawa na uchungu.
- Sasa tumemjia Yesu Kristo-Waebrania 2:7-8; Ufunuo 19:11-16.
- Daudi alipokuwa katika pango la Adulamu aliandika Zaburi 57, 142, 61:1-2.
MWISHO
- Je, maisha yako kwa sasa ni kama jinsi pango?
- Je, pango lako ni baraka hau ni kilio?
- Kwa vyovyote vile, mjie Yesu Kristo leo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
