Swahili Service

DHIKI KUU (TAABU YAKE YAKOBO).

MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO

SOMO: Mathayo 24:1-31; Yeremia 30:6-7

 

Leo tunaendelea kutazama Biblia zetu juu ya siku za mwisho na mambo ambayo lazima kutendeka duniani kutimiza mpango mkuu wa Mungu. Mpaka sasa tumejifunza juu ya kunyakuliwa na kiama ya wafu waliolala katika Kristo, pia tumeona juu ya mtu aitwaye mpinga Kristo, yaani anti-Christ. Leo tunaona juu ya dhiki kuu, au siku zinazoitwa “taabu yake Yakobo”-Yeremia 30:6-7.

Dhiki kuu imeonyeshwa kama mwanaume anayejifungua mtoto!! Mwanaume huyu anao utungu mwing kiasi Analia na kuanguka chini. Biblia inasema dhiki kuu ni siku ya taabu nyingi na zaidi. Hakujakuwa na siku kama hizo na hakutakuwa na siku kama hizo tena. Hebu tuone juu ya dhiki kuu au taabu yake Israeli. Kuna sababu mbili za dhiki kuu;

  1. Kuadhibu mataifa ya dunia hii-Warumi 1:18; 2 Wathesalonike 2:12-13; Ufunuo 19:15.
  • Kwa miaka elfu wanadamu wamekataa neno la Mungu na mwito wa kuokoka. Katika dhiki kuu Mungu atahukumu watu wa mataifa.
  1. Kusafisha watu wa Israeli-Ezekieli 20:37-38; Zakaria 13:8-9; Malaki 3:3
  • Watu wa Israeli wamekataa Masihi wao-Yohana 1:11-12. Walimuua Mwokozi wao msalabani. Mungu atatumia dhiki kuu kuwaweka tayari Israeli kumpokea Masihi wao Yesu Kristo arudipo duniani. Hebu tuone.

JINSI DHIKI KUU ITAANZA-Mathayo 24:1-14.

  • Mathyao 24-ni sehemu ya ujumbe wa Yesu Kristo juu ya mlima Zeituni (Olivet discourse).
  • Wanafunzi wa Yesu Kristo walistaajabu sana alipowaambia kwamba hekalu la Yerusalemu lazima litaharibiwa-Vs. 1-4.
  • Siku mbele ya dhiki kuu zitakuwa wakati wa:-

Udanganyifu wa kiroho-Vs. 5-11.

  • Wengi watainuka na kujiita Masihi na Kristo.
  • Manabii wengi watajitokeza duniani.
  • Kutakuwa pia na watu wawili hodari zaidi kudanganya dunia.
  • Mapinga Kristo-Anti-Christ.
  • Nabii wa uongo-False prophet.
  • Ufunuo 13-Hawa wawili watafanya dunia yote kuamini kwamba wao ni Mungu.
  • Wawili hawa wataabudiwa kama Mungu.
  • Mpinga Kristo ataleta amani nyingi duniani kwa kipindi cha miaka 31/2-Ufunuo 6:2; Danieli 8:25.
  • Kumbuka manabii wa uongo kama jinsi David Koresh, Jim Jones, Sun Myung Moon, basi nabii wa uongo atakuwa zaidi.

Taharuki katika mataifa-Vs. 6-13.

  • Dhiki kuu itaanza na wakati wa misuko suko.
  • 6-7-Vita na matetesi ya vita.
  • Vita vitaongezeka, uasama katika mataifa.
  • Amani atakaye leta mpinga Kristo haitadumu-Ufunuo 6:4, mpanda farasi mwekundu-ni ishara ya vita.
  • Dunia nzima itainuka juu ya Israeli, chuki, na mateso-Mathayo 24:9; Danieli 7:25.
  • Tayari haya mambo yanatendeka mbele ya macho yetu (Kenya-Somali).
  • Russia na Iran wataungana kuipinga Israeli-Ezekieli 39:9.
  • Wakati huu, ni wakati wa maangaiko mengi.
  • Kutakuwa na njaa-Ufunuo 6:5-6.
  • Farasi mweusi-mauti-Ufunuo 6:5-6.
  • Utakuwa wakati wa magonjwa mengi-Vs. 7.
  • Robo ya wanadamu wa dunia watakufa-Ufunuo 6:8.
  • Wakati huu ni wakati wa tauni na dhiki-Vs. 7.
  • Wakati huu ni wakati wa uasi-Vs. 10-12.
  • Watu watapenda dhambi zaidi-Vs. 12

Injili ya Kristo itahubiriwa kote duniani-Mathayo 24:14.

  • Wahubiri 144,000-jeshi la Injili-Ufunuo 7:1-8.
  • Mashahidi wawili (Enoko na Eliya) watahubiri zaidi-Ufunuo 11:1-12.

JINSI DHIKI KUU ITAENDELEA-Mathayo 24:15-29.

Zitakuwa siku za shida-Vs. 15.

  • Mpinga Kristo atavunja ule mkataba wa amani na Israeli-Danieli 9:27.
  • Mpinga Kristo atauliwa-Ufunuo 13:3, 14.
  • Hekalu lazima kujengwa tena mle Yerusalemu.

Zitakuwa siku mbaya zaidi-Vs. 16-29.

Vs. 16-20-siku za usaliti na mateso.

  • Waisraeli wengi watakufa-Zakaria 13:8.
  • Waisraeli wengine watamfuata mpinga Kristo-Mathayo 24:10-12; Ufunuo 2:9; 3:9.
  • Wachache (mabaki) wataokoka-Ufunuo 12:14; Zakaria 13:9.
  • Zitakuwa siku za uchungu mwingi zaidi-Vs. 21.
  • Hukumu za baragumu.
  • Baragumu ya kwanza-Ufunuo 8:7, 1/3 ya mazingira itaaribika-Carbon.
  • Baragumu ya pili-Ufunuo 8:8-9. 1/3 ya bahari itakuwa damu, 1/3 viumbe vya bahari vitakufa, 1/3 ya meli duniani zitaharibika.
  • Baragumu ya tatu-Ufunuo 8:10-11. 1/3 ya maji safi ya dunia itaharibika na kuwa sumu.
  • Baragumu ya nne-Ufunuo 8:12. 1/3 ya nuru ya jua itazimika na nuru ya mwezi na nyota itapunguzwa, hii italeta madhara mengi juu ya viumbe vyote.
  • Baragumu ya tano-Ufunuo 9:1-12.
  • Dunia yote inavamiwa na pepo wachafu (demons) kutoka jehanamu.
  • Dimoni hawa watadhuru dunia kwa miezi mitano.
  • Dimoni hawa hawataua watu lakini kazi yao ni kutesa watu.
  • Watu watataka kufa, lakini hawatakufa.
  • Baragumu ya sita-Ufunuo 9:13-21.
  • Mapepo wabaya (dimoni) 200,000,000 watakuja toka jehanamu na kuwaua watu 1/3
  • Pamoja na dhiki hii, watu hawatatubu-Ufunuo 9:20-21.
  • Baragumu ya saba-Ufunuo 11:15-19.
  • Baragumu ya saba itatangaza kuja kwa Yesu Kristo duniani.
  • Bakuri (kitasa) saba za hukumu zaidi zitamwagwa duniani.
  1. Kitasa cha kwanza-Ufunuo 16:2, saratani (cancer) ilimwagwa juu ya dunia.
  2. Kitasa cha pili-Ufunuo 16:3.
  • Maji ya bahari zote ilikuwa damu wakafa viumbe vyote.
  1. Kitasa cha tatu-Ufunuo 16:4-7.
  • Visima vyote vya maji safi duniani vikawa damu.
  1. Kitasa cha nne-Ufunuo 16:8-9.
  • Ukali wa jua ukaongezwa-watu wakachomeka zaidi lakini hawakutubu dhambi.
  1. Kitasa cha tano-Ufunuo 16:10.
  • Giza itajaa dunia kote.
  • Watu wa ulimwengu watalia sana, lakini watakataa kutubu dhambi zao.
  1. Kitasa cha sita-Ufunuo 16:12-14.
  • Mto wa furati (Euphrates) utakauka maji yake, kutayarisha mapito ya majeshi ya dunia kwa vita vya mwisho.
  1. Kitasa cha saba-Ufunuo 16:17-21.
  • Tetemeko kuu zaidi-visiwa vitazama, milima itaanguka, miji mikuu itaharibiwa, mvua ya mawe (125lb=60kgs) itanyesha juu ya dunia.

Ukiwa umeokoka, hautapitia dhiki hii kuu, Halelleuya!!

Lakini Mungu ataona huruma zake, kufupisha siku za dhiki kuu-Habakuki 3:2.

JINSI DHIKI KUU ITAMALIZIKA-Mathayo 24:30-31.

  • Mwokozi Yesu Kristo atarejea duniani-Vs. 30.
  • Atakaporejea Kristo atamharibu kabisa mpinga Kristo-Ufunuo 19:11-14.
  1. Wenye dhambi waliosalia duniani watalia na kuomboleza.
  • Majeshi ya dunia yote watapinga sana kurudi kwa Yesu Kristo.
  • Watakuwa tayari kwa vita iitwayo ARMAGEDDON.
  • Damu itamwagika kiasi-Ufunuo 14:20.
  • Yesu Kristo atashinda vita hizi kwa neno la kinywa chake-Ufunuo 19:15-21.
  1. Watakatifu wa dhiki kuu watakusanyika.
  • Hawa ni wale waliokoka kwa mahubiri ya wale wahubiri 144,000 (wote Wayahudi) na pia wale mashahidi wawili.
  • Watakatifu hawa wataingia hai katika utawala wa Kristo wa miaka 1,000 pamoja na sisi, bibi arusi wa Kristo.

MWISHO

  • Tumeona kwa kifupi yatakayojiri duniani.
  • Dhiki kuu si mchezo.
  • Je, wewe uko tayari kwa kurudi kwa Yesu Kristo?
  • Je, wewe unao hakika ya wokovu wako?
  • Basi tuwatangazie wote wokovu huu mkuu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *