MFULULIZO: JINSI YA KUFANYA VITA VYA KIROHO
SOMO: EZEKIELI 28:12-19; WAEFESO 6:12; ISAYA 14:12-17
Katika mfululizo huu juu ya vita vya kiroho, tutazingatia sana amri kuu tuliyopewa na Yesu Kristo- “Mpende Bwana Mungu wako, mpende jirani yako kama jinsi ujipendavyo mwenyewe.” Amri kuu ndio msingi wa vita vya kiroho. Lazima kuelewa na uhusiano wako na Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kuokoka ni jambo la uhusiano na Mungu.
Vita unavyopigana kila siku ni vita vya kiroho. Vita vya kiroho si vita na mwanadamu lakini ni vita dhidi ya mamlaka- Waefeso 6:12. Unapopigana na mwanadamu mwenzako, vita hizo zinamsaidia shetani ambaye ndiye kiini cha vita vya kiroho.
Kanisa ulimwenguni wote katika historia imepoteza wakati kupigana vita vya mgawanyiko juu ya ‘doctrine.’ Vita vya namna hii haviwezi kusaidia Injili, bali Injili ya msamaha ndio tumeitiwa.
Hebu tujifunze:-
UWEPO WA MAOVU
- Uovu umejaa duniani kote, uovu ni jambo la kiroho.
- Shetani ni mtu, hivyo ana nafasi kama wewe na mimi.
- Shetani anazo hisia, uamuzi na akili kama jinsi mtu- Ezekieli 28:12-19.
SHETANI NI NANI?
- Kama wakristo tunahitaji kuchukua wakati kupigana na shetani na kazi zake- Ezekieli 28:12-19.
- Shetani si nguvu tu bali ni mtu kama jinsi wewe na mimi. Pia shetani ni roho ya uovu, ni kiumbe.
- Shetani anaabudiwa duniani kote. Katika nchi za magharibi siku ya shetani ni kila tarehe 31 Octoba- (Haloween).
- Shetani ametambulishwa kwetu mara ya kwanza katika Biblia- Mwanzo 3:1.
- Shetani aliishi mbinguni hapo Mwanzo, alikuwa pamoja na Adamu katika Bustani ya Edeni. Ezekieli 28:11-19- shetani alikuwa kiumbe ajabu zaidi, mpakwa mafuta wa Bwana. Kwa kiburi shetani alijiinua kuwa juu ya mlima wa Mungu. Shetani kwa kuasi Mungu, alitimuliwa mbinguni pamoja na theluthi moja 1/3 ya malaika za mbinguni- Yohana 8:44; 1 Tim. 3:6; 2 Petro 2:4; Ufunuo 12:7-9.
- Kama jinsi kila mwanadamu, shetani alipewa uchaguzi wa kuchagua maovu na mazuri.
- Urembo aliopewa na Mungu ulimwelekeza shetani kuwa na kiburi, hii ndiyo dhambi ya kwanza.
- Shetani alichagua kutoishi katika kweli, hivyo akaingia katika hukumu.
- Shetani ni kiumbe chenye akili ya juu zaidi katika ulimwengu wa roho. Shetani ni jambazi juu ya maisha.
- Shetani anayo akili, ujuzi, hisia na uamuzi wa binafsi.
- Shetani ni mwizi, alikuja kuiba, kuua na kuharibu- Mathayo 13:39; Luka 10:18, 11:18; Yohana 10:10; 2 Wakorintho 11:2-3, 13:13-15; 2 Tim. 2:26; Ufunuo 12:17.
- Shetani ametajwa mara 36 katika Biblia, kama “shetani” mara 33 na kama “Ibilisi” na devil.
- Jina “shetani” Maanake ni “Mshtaki.”
- Jina Devil, Ibilisi ni jina la Giriki “Diabolos”- mshtaki.
- Shetani pia anaitwa “Lucifer” Luciferi Maanake ni “mwana wa asubuhi” kumaanisha anadanganya kupitia urembo wake.
- Shetani ni mwenye kujaribu- Mathayo 4:3.
- Shetani pia anaitwa muovu- 1 Yohana 2:13; Ufunuo 12:9.
- Shetani ni baba wa udanganyifu.
- Shetani ni muuaji- Yohana 8:44, mfalme wa dunia hii- Yohana 12:31.
- Shetani ni mfalme wa hali ya anga, mungu wa kizazi hiki, mshtaki wa ndugu.
- Shetani anaitwa “Azazel”, Beelzebub- mungu wa “Nzi”- (the lord of flies) swarms of demons.
- “BELIAL” the base one, Maanake shetani ni mnyama (animal or bestial nature).
- Shetani ni mungu wa dunia hii- 2 Wakorintho 4:4; Walawi 16:8, 10, 26; Mathayo 4:3, 12:24; Waefeso 2:2.
- Shetani ni “roho” KAWI inayofanya kazi duniani- Waefeso 2:2.
- Shetani ni “Mpinga Kristo”- (Anti- Christ)- 2 Wakorintho 11:4; Ufunuo 12:10-17.
- Kila asiyeokoka yuko chini ya nguvu na uongozi wa shetani- 1 Yohana 5:19.
WATOTO WA SHETANI NI DHAHIRI- 1 Yohana 3:10
- Watoto wa shetani wanafanya kama shetani mwenyewe- Yohana 8:42-44.
- Watoto wa Mungu ni dhahiri, wanafanya kama Mungu, kama Yesu Kristo.
- Ni watu wa msamaha na upendo kwa ndugu zao.
- Sisi tuko kama Mungu na kama Yesu Kristo tunaposamehe.
MWISHO
- Kushinda vita ni kufahamu adui wako na jinsi alivyo.
- Kushinda vita ni kufahamu mbinu za vita.
- Kushinda vita ni kufahamu silaha zako za vita.
- Sisi tuko vitani na shetani na pepo zake na agenti wake.
- Katika Kristo, sisi ni zaidi ya washindi.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- WHO IS SPEAKING TO YOU? - September 3, 2025
- CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO. - August 31, 2025
- THE GOD WHO BREAKS YOKES. - August 31, 2025