Swahili Service

“FANYA BONDE LAKO LIJAE MAHANDAKI”

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: 2 WAFALME 3:1-27

 

Wafalme watatu waliacha Mungu nje ya mipango yao. Katika dhiki yao walimuomba Mungu apate kuwasaidia. Huwezi kupigana vita vya kiroho mpaka kutubu dhambi zako, pamoja na uasi, ubinafsi na dharao. Hivyo upako wa Roho Mtakatifu utapatikana. Fanya bonde la maisha yako lijae mahandaki (ditches).

Mfalme Napoleoni Bonaparte wa Ufaranza ulipanga kuvamia Urusi. Generali mmoja wake akasema, “Mwanadamu anapanga lakini Mungu anatekeleza” (“Man proposes, but God disposes.”) mfalme Napoleoni akajibu, “ninapanga na kutekeleza” (I propose and dispose). Hivyo Napoleoni hakumhusisha Mungu katika mipango yake, jambo hilo lilileta maafa kwake na jeshi lake.

Mungu alimwonyesha Napoleoni kivumbi kupitia jambo rahisi, Mungu alinyesha barafu (snowflakes). Katika mwaka wa 1812, Napoleoni Bonaparte aliingia Urusi akiwa na jeshi la askari 410,000. Katika mwaka huo huo, Napoleoni alitoka Urusi na askari 9,000.

Kwa kiburi chake Napoleoni alipoteza taji lake, jeshi lake, uhuru wake na ushindi wa Mungu ukaonekana. Baadae Napoleon alikamatwa na kufungwa maisha yake yote mle kisiwa cha St. Helena alipokufa mauti!!

Ujumbe wetu leo ni “fanya bonde lako lijae mahandaki” (ditches).

Hebu tuone:-

KUMSAHAU MUNGU NA MATOKEO YAKE.

  • Hali yao, Wafalme watatu wa Israeli ulizorota maana wote walimwacha Mungu nje ya mipango yao ya vita juu ya mfalme Mesha wa Moabu.

Ahabu na milki yake walimwacha Mungu.

Yoramu alikuwa mwana wa mfalme Ahabu.

  • Biblia inaeleza kwamba mfalme pamoja na nyumba yake waliuza maisha yao kwa uovu na shetani.
  • Ahabu alikuwa mwana wa Omri, mke wake alikuwa Jezebeli Binti yake mfalme Ethibaali mfalme wa Sidoni.
  • Yezebeli alianza ibada za miungu ya Phoenicia (Sidoni). Baali alijengewa hekalu kote Israeli.
  • Yoramu hakuwa na heshima kwa Yehova Mungu wa Israeli. Hata kwa kuona miujiza ya Eliya nyumba ya Ahabu haikushtuka.

Matokeo- Adui mkuu aliibuka.

  • Mesha mfalme wa Moabu aliinuka juu yake Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Yuda.
  • Mpango wake Yoramu.
  • Israeli yote wainuka kupigana vita.
  • Omba msaada kutoka mfalme Yehoshaphati mfalme wa Yuda.
  • Omba msaada kutoka Edomu na mfalme wake.

Yehoshaphati pia alimwacha Mungu!!

  • Yehoshaphati alikuwa ameokoka, akajiunga pamoja na Yoramu kwa sababu:-

Vita hivyo vilionekana vita vya haki.

  • Mwana wa Yehoshaphati alikuwa amemwoa dadaye Yoramu- Athalia.
  • Huyu Athalia baadae aliwaua watoto wa kiume wa Yehoshaphati, kukabaki kijana mmoja mdogo aliyefichwa katika nyumba ya Mungu na kuhani mkuu.

Biblia inaonya juu ya ushirika katika walioamini na wasioamini Mungu.

  • Ushirika uwe ni biashara, ndoa, urafiki, sherehe na mengi- 2nd Wakorintho 6:14-18.

Hatumwoni mfalme Yehoshaphati, mfalme aliyeokoka akimuuliza Mungu mapenzi yake kwa maombi au kwa ushauri kutoka kwa nabii wa Mungu!!

  • Wafalme wote watatu walikuwa mbali na Mungu wa mbinguni, Mungu wa Israeli.
  1. Shida, janga iliwapata wafalme na majeshi yao.
  2. Baada ya siku saba jangwani, jua kali, vumbi, kiu, hakuna maji.
  3. Ni ajabu jinsi hali yetu ya kiroho inaweza kujionyesha katika hali yetu ya maisha.
  4. Kifo kiliyatisha maisha yao kama wafalme, majeshi yao na wanyama wao wote.
  • Walihitaji msaada na miujiza ya Mungu.

ILIWAPASA KUMRUDIA MUNGU WA ISRAELI

  1. Ushauri- “TAFUTA MUNGU.”
  2. Je, mara ngapi tumeanza jambo bila Mungu, bila ushauri wake, bila maombi?
  3. Mfalme Yehoshaphati aliyafanya yale aliyohitajika kufanya hapo mwanzo.

“Tafuta Mungu Bwana wako kwanza”- v.11.

4. Imba wimbo- “Yesu kwetu ni rafiki.”

  • Mithali 16:3- “Mkabidhi BWANA kazi zako na mawazo yako yatadhibitika.”
  • Mithali 16:1-7.

UJASIRI WA NABII ELISHA

Wafalme wale watatu walimwendea nabii Elisha.

  • Kumbuka si Elisha alienda kwao, Wafalme walimtafuta Elisha.
  • Elisha hakubabaishwa na ukuu wa mwanadamu yeyote.
  • Elisha hakuogopa Wafalme na majeshi yao.
  • Elisha alizoea kusimama mbele ya Mungu na uwepo wake, hivyo mwanadamu ni nani kwa Elisha?
  • Ikiwa umezoea kusimama mbele za Mungu- hakuna wa kukutisha moyo.
  • Malaika Gabrieli alimwambia Zekaria- “mimi ni Gabrieli ninasimama mbele za Mungu”- Luka 1:19.
  1. Ufunuo wa Mungu kwa Israeli na Yuda.
  2. Hata naye nabii Elisha alihitaji kuutafuta uso wa Mungu.
  3. Elisha alimtafuta mcheza kinubi- sifa na ibada zinavuta uwepo wa Mungu.
  • Ukitaka kumwona Mungu, sifa, ibada na kisha utulivu- Zaburi 46:10.
  • Neno la Bwana lilimjia Elisha, “fanya bonde lijae mahandaki”- V.16-17.

SULUHISHO: TENGENEZENI MIOYO YENU.

Tunapigana vita vya kiroho.

Wafalme hao watatu na majeshi yao walikuwa na silaha zao, panga zao mikononi lakini mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu wao.

  • Hakuna njia yoyote, kushinda vita bila MAJI- Roho Mtakatifu.
  • Upako ni lazima kwa vita vya kiroho.

Kuna hatua tatu za vita vya kiroho.

  • Vita vya ndani.
  • Vita vya nje juu ya mwanadamu.
  • Vita dhidi ya nguvu za giza katika ulimwengu wa roho.

Silaha zetu zinazo nguvu- 2 Wakorintho 10:4.

  • Kupigana vita vya kiroho ni lazima kuweko roho zetu na nyumba zetu katika order.

Kufanya mahandaki ni picha ya hali ya mioyo yetu.

  • Jangwa ni picha ya mioyo yetu.
  • Ukavu, tasa, kifo, bila kulimwa, bila kutubu dhambi.
  • Mioyo iliyokauka lazima kulimwa upya upako upatikane.

Njia za Mungu ni za ajabu.

  • Hamtaona upepo au mvua lakini mahandaki yatajaa maji!!
  1. Lazima kuwa tayari kwa baraka za Mungu.
  2. Mpe Roho Mtakatifu nafasi:-
  • Kupitia maombi.
  • Kwa sifa na ibada.
  • Kufunga saumu.
  • Injili kwa wote.
  • Kwa kufanya mahandaki kila mahali.
  • Lazima kila bonde kufanya mahandaki.
  • Tabiri mema juu ya maisha yako, kinyume cha unabii wa shetani kwako.
  • Shetani aliposema:-
  • Nitaharibu huduma yake- mwambie huduma yangu itasimama!
  • Nitaharibu ndoa yako- jamii yangu itabarikiwa.
  • Nitaingilia afya na uchumi wako- afya na uchumi wangu zitastawi.
  • Leo kunao upako wa kumaliza ukame wote katika maisha yako- Ayubu 14:7-9.
  • Nusa harufu ya maji sasa!! Harufu ya miujiza, furaha, amani, urejesho.
  • Bila upepo, bila mvua, lakini mahandaki yalijaa maji.
  • Sasa anza kumsifu Mungu, deni utalipa, ndoa utarejeshewa, jamii itarudiana, ugonjwa umepona, biashara yako itastawi, watoto wako wataokoka.
  • Badili misimu (season) wako.
  • 2 wafalme 3:18-19- “Hili ni jambo rahisi mbele ya Mungu.”

MWISHO

  • Omba msimu mpya leo.
  • Wacha jangwa yako ijae maji kila mahali.
  • Wacha adui zako washindwe.
  • Pokea urejesho wa Bwana leo, katika jina la Yesu Kristo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *