MATENDO 2:22-28
UTANGULIZI
Mwokozi Yesu Kristo aliuona uchungu wa mauti. Mwili wake ulikufa kweli, kweli. Lakini Kristo hakuona uaribifu maana Kristo alikuwa bila dhambi, dhambi ndio huleta uaribifu na kuoza na wadudu waletao kuoza. Hivyo mwili wa Kristo ulikombolewa na ufufuo ,Kristo asishikwe na kaburi. Kaburi inashika watu, ili mauti yafanye kazi kamilifu. Mfalme Theodosius wa Ugiriki aliwafungulia huru wafungwa wote, Basi akasema, “Ninaomba Mungu naye afungue makaburi yote na kuwapa wafu wote uzima kutoka kwa mauti” Siku moja maombi ya Theodosius yatajibiwa, wafu watafufuliwa (Danieli 12:1-4)
Hebu tuone:-
I. HAIKUWEZEKANA NGUVU ZA MAUTI KUMSHIKA BWANA.
- Ukuu wa Yesu Kristo uko juu ya nguvu za mauti.
- Kristo alikuwa na uwezo wa kuweka maisha yake chini nayachukue tena (Yohana 10:18)
- Kristo alikuwa katika umoja na Baba na Roho mtakatifu katika ukamilifu wa utatu wa Mungu.
- Kristo alikuwa amemaliza kazi yote ya ukombozi wetu.
- Kristo alikuwa na ofisi ya Kuhani Mkuu katika enzi ya Melchizdeki (Waebrania 6:20)
- Alikuwa mfalme wa milele (Zaburi 45:6)
- Alikuwa mchungaji wa milele (waebrania 13:20)
- Kama Kristo angeshikwa na kaburi;
- Hakuna hakika ya ufufuo (I Wakorintho 15:17)
- Hakuna kuhesabiwa haki (Warumi 4:25)
- Hakuna mwombezi mbinguni (Waebrania 9:24)
II. HAIWEZEKANI NGUVU ZOZOTE KUSHIKA UFALME WAKE.
- Philosophia za Roma, Ugiriki na nguvu za ufamle wa giza hazitashika kazi ya kanisa la Kristo.
- Masomo ya wasomi wote na elimu yao haitashika injili ya msalaba (I Wakorintho 1:20)
- Ujinga wa vizazi hautashika injili ya Kristo (Mathayo 11:5, Mathayo 4:16)
- Mamlaka, utajiri, mapambo, uogo na desturi za dunia hii hazitashika ufamle wake (Matendo 4:26)
- Uovu wa dunia hii ni mapambo ya dunia, haitashika kabisa ufalme wa Kristo duniani (Yohana 16:33)
- Nguvu za uchawi, ibada za shetani kanisani hazitaweza kushika kazi ya injili (mathayo 16:18)
III. HAIWEZEKANI KUSHIKA MATEKA CHOCHOTE KILICHO CHA KRISTO
- Mwenye dhambi dhaifu ataweza kwenda huru leo (Zaburi 124:7)
- Mtakatifu wa Mungu hatashikwa mateka na dhiki, majaribu na mateso (Zaburi 34:19, 116:7)
- Miili ya watakatifu haitashikwa na kaburi siku zote (I Wakorintho 15:23, I Petro 1:3-5)
- Viumbe vyote havitakaa siku zote katika kuugua katika uchungu (warumi 8:21)
MWISHO
- Haikuwezekana mauti na kaburi kumshika Kristo.
- Haitawezekana dhambi, mauti na kaburi kukushika Mwana wa Mungu.
- Leo uemokoka ? Leo tembea naye daima.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
