MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO
SOMO: MATHAYO 24:1-14
Wakati huu wa virusi vya corona (Covid-19) watu wengi duniani wamewaza sana maneno ya Yesu Kristo aliyoyasema juu ya mlima wa Mizeitum katika Mathayo 24. Ujumbe huu wa Yesu Kristo ndio mrefu zaidi katika ujumbe zake duniani, Yesu Kristo yuaja tena! Hakuna taswishi juu ya kurudi kwake duniani. Katika Mathayo 24, Bwana wetu anatazama siku zijazo na kutueleza juu ya kuja kwake mara ya pili. Katika mfulilizo huu wa ujumbe kwa Kiswahili tutajifunza zaidi habari za kuja mara ya pili kwa Mwokozi wetu. Hata ingawa, Bwana hakutueleza siku hasa ya kuja kwake, yeye mwenye alitupa ishara za kurudi kwake.
Chochote alichosema Mwokozi wetu lazima kutimia. Hebu leo tuone maneno ya hakika ambayo lazima kutendeka kulingana na unabii wa Bwana wetu Yesu Kristo:-
I. JAMBO LA KWANZA –HAKIKA YA UFUPI WA WAKATI HAPA DUNIANI (MATHAYO 24:1-2)
- Unabii huu ulitimizwa miaka 40 baadaye.
- Katika mwaka wa 70 AD, majeshi ya Roma chini ya Generali Tito yalingia Yesuralemu na kuvunja kabisa mji wa Yesuralemu, pamoja na hekalu ya Yerusalemu.
- Kutoka wakati huo, kila mwezi wa julai hau Augosti wayahudi wangali wanaomboleza siku ya kufunga saumu ya tisha B’AV, kukumbuka siku hii.
- Generali Tito na majeshi yake walibeba kinara ya hekalu ya Yerusalemu mpaka Roma, wakajenga sanamu kubwa inaoonekana mpaka hivi leo tangu mwaka wa 82AD.
- Hekalu lilikuwa mahali pa ibada kwa wayahudi – lakini sasa hekalu la wakristo ni Yesu Kristo mwenyewe na mioyo yetu ni hekalu la Roho mtakatifu.
- Katika Mathayo 27:51 – pazia za hekalu ziliraruka juu chini – Mungu alitufungulia njia ya mataifa yote kumjia Mwokozi na kuokolewa.
- Katika agano la kale, Mungu aliongea kwa lugha ya kiebrania kwa wayahudi, lakini katika agano jipya Mungu aliongoea katika kigiriki (kiyunani) lugha ya biashara duniani kote wakati huo.
- Mungu hataishi tena mahali hapo pa hekalu Yerusalemu, sasa anaishi katika kila moyo, na anayeokoka kupitia mwanaye, yaani Yesu Kristo.
- Lakini pia katika unabii huu, somo la maana kwetu binafsi ni kwamba wakati tulionao hapa duniani ni wakati mfupi sana.
- Wanafunzi wa Yesu Kristo, walimwonyesha hekalu na umaridadi wake – lakini Kristo hakuvutiwa bali alipenda wafahamu jinsi, vitu vya dunia hii ni vya mda fupi zaidi.
- Yesu Kristo aliwaambia, “hamyaoni haya yote? Amini, nawaambieni halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabonoshwa.”
- Ndungu na dada zangu, hakuna jengo lolote hapa duniani litakalo simama daima.
- Ukweli juu ya mijengo ni sawa na ukweli wa miili yetu – maisha na wakati ni fupi sana (Yakobo 4:13-15)
- Wakati ni mfupi zaizi, Mtume Paulo ametushauri (I Wakorintho 7:29-31)
- Kristo ametushauri kukesha na kuomba, maana hatujui siku ya kurudi kwake duniani.
II. JAMBO LA PILI – HAKIKA TAFADHALI TAFUTA UKWELI WA KIROHO KUTOKA KWA BWANA YESU PEKEE. (MATHAYO 24:3-5)
- Wanafunzi wa Kristo walimjia kwa faragha.
- Wanafuzi walikuwa wamechanganyikiwa kama sisi leo.
- Lakini wanafunzi walimwendea Yesu Kristo.
- Katika wakati huu wa koronavirus, hebu tumjie Kristo kwa maswali yetu yote.
- Wanafunzi wa Yesu Kristo walikuwa na maswali tatu.
- Mambo haya yatakuwa lini?
- Ni nini dalili yakuja kwako?
- Ni nini dalili ya mwisho wa dunia?
- Bwana Yesu Kristo alisema, katika mambo ya kiroho, wengi watadanganywa, lakini Kristo hawezi kwa maana yeye ndiye kweli (Yohana 14:6)
III. JAMBO LA TATU – HAKIKA YA UKUU WA WOKOVU (MATHAYO 24:6-9)
- Tunapookoka tunapata Baraka nyingi zisizohesabika. Hizi ni Baraka za kuokoka.
- Kwanza kama wakristo tunapata Amani katika dhoruba za maisha.
- Katika (Mathayo 24:6-9) Yesu alisema kutakuwa na dhoruba kali kwa wale wameokoka na wale bado.
- Tunasikia habari za vita na matetezi ya vita.
- Angalieni msitishwe, maana hayo hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado.
- Tunapowaalika watu kuokoka, tunawaliika kwa uzima tele, uzima wa milele, maisha dani ya Kristo ndio maisha bora zaidi – lakini maisha dani ya Kristo si maisha bila dhoruba.
- Bado kuna taabu, hata kifo katika kuokoka tunateseka kwa sababu ya ufamle wa mbinguni. (Yohana 16:33)
- Pili, Baraka kuu ya kuokoka ni upendo wa milele na milele (Mathayo 24:10-12)
- Tumepewa upendo usioweza kwisha (Warumi 5:1-5)
- Tatu, Baraka kuu ya kuokoka ni nguvu za kusima imara daima. (Mathayo 24:130
- Wale wameokoka kweli, kweli watastahimili mpaka mwisho.
- Ishara kubwa ya kwamba mtu ameokoka ni kustahimili mpaka mwisho.
- Ikiwa hautastahimili mpaka mwisho ni kwa sababu ulikuwa bado uokoka!! (Wafilipi 1:6, II Timotheo 1:12)
- Nguvu za kustahimili zinatoka kwa Mungu mwenyewe (Waefeso 3:16, Wafilipi 4:13)
IV. JAMBO LA NNE – HAKIKA LAZIMA INJILI KUHUBIRIWA DUNIANI KOTE (MATHAYO 24:14)
- Yesu Kristo yuaja mara ya pili, lakini ni kitu gani amesubiri?
- “Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo ndipo mwisho utakapokuja”.
- Yesu Kristo yuasubiri dunia yote kusikia injili ya wokovu.
- Yesu Kristo yuasubiri yeyote atakaye okoka kuokoka.
- Kila mtu aliyeokoka ameitwa kuitangaza habari njema ya wokovu.
- Mambo mengine ya kurudi kwa Yesu Kristo ni siri, lakini yale ya maana tayari juu ya kuja kwake tumeelezwa.
MWISHO
- Ukweli na uhakika uliojuu zaidi ni kwamba Yesu Kristo yuaja tena.
- Kwa sasa Kristo yutayari kuokoa yeyote atakaye weka imani yake juu yake.
- Mtume Paulo amesema katika (Warumi 10:13)
- “Kwa kuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka.”
- Unaweza kukoka sasa, tunapomwendea Mungu katika maombi.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025