ISAYA 54:17
UTANGULIZI
Ulinzi ni moja yao ya Baraka za Mungu kwetu wana wa Mungu. Kila mtoto wa Mungu anahitaji kufurahia ulinzi na usalama wa nafsi, mwili, roho na mali (Zaburi 23:4-5). Kama Mwana wa Mungu unalindwa kutoka kwa maovu na hatari. Mungu anataka tujue kwamba usalama na ulinzi wetu haumo mikononi mwa mtu hau watu lakini dani ya Bwana mwenyewe. Mfalme wa Shamu alituma majeshi yake juu ya Israeli, mtumishi wake Elisha alifadhaika sana “Ole wetu ! Bwana wangu tifanyaje ? Elisha akamjibu, usiogope maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao (II Wafalme 6:14-18). Mungu aliyafumbua macho ya mtumishi wa Elisha, mtumishi akayaona majeshi, farasi na magari ya moto yakiwazunguka. Elisha alifahamu kwamba Mungu ni ulinzi na usalama wake. Ikiwa Mungu alimlinda Elisha, basi yeye atakulinda wewe. Ametupatia Roho mtakatifu kutembea nasi katika maisha na malaika wengi zaidi (Waebrania 1:14). Hivyo tembea katika maisha bila shaka na hofu bali kwa ujasiri wa moyo. Haijalishi unayoyapitia na nani anayekupangia maovu.hata unapojisikia wewe upeke yako, kumbuka (I Yohana 4:4) Ulinzi na usalama ni urithi wa watumishi wa Mungu. Hivyo ona mambo matatu katika kifungu hiki:
- silaha ni lazima kuundwa (II Wakorintho 2:11)
- Silaha ni lazima kufanyishwa kazi (deployed)-(Zaburi 34:19).– Shetani hakufamii kwa sababu ya dhambi lakini kwa sababu silaha zinaundwa na kufanyishwa kazi.
- Shetani (Adui) anachukua wakati mwingi kuunda, kufanyisha na kuanza vita juu ya watakatifu.
- Shetani anagojea wakati wa udhaifu wako.
Hebu tuone:-
I. KWANZA: KUFUNUA ADUI YETU
Adui zetu ni watatu:
- Mwili– Warumi 7:18-25, Wagalatia 5:16-25. tunamshida adui wa mwili kwa kutembea katika Roho mtakatifu. Lazima kumtii Roho Mtakatifu.
- Dunia: Yohana 15:18-19, I Yohana 3:13, I Yohana 3:13, I Yohana 5:19, Yohana 16:33.
- Tunashinda dunia kwa Imani yetu (I Yohana 5:4-5)
- Tunashida kwa maamuzi yetu (Zaburi 101:3)
- Shetani: (I Petro 5:8)
- Shetani na malaika zake wanataka uanguke (waefeso 6:11-18)
- Hivyo shetani atafamia afya, pesa, Imani na jamii yako.
- Tunamshida Shetani ; Kumnyenyekea Mungu , Kumpiga Shetani (Yakobo 4:7)
- Tunamshida shetani kwa damu, neno la ushuhuda na kutopenda nafsi zetu (Ufu. 12:11)
- Tutamshinda shetani kwa neno (Waefeso 6:17)
II. PILI: KUFUNUA BINU ZA SHETANI (2 Wakorintho 2:11)
- Shetani anatafuta kukunyanganya nguvu zako (I Samweli 13:9-22, 2 Wakorintho 10:4)
- Shetani anatafuta kukuzuia usifike lengo lako– Shetani anataka ukose shabaha yako (Yere-29:11)
- Shetani anatafuta kukufanya kiwete kiroho
- Shetani anatafuta kukuua kabisa (Yohana 10:10)
III. TATU: USHINDI WETU JUU YA SHETANI
- Watakatifu wako na nguvu na ushidi dhidi ya shetani kupitia kwa Roho Mtakatifu (Zakaria 4:6)
Hivyo:
- Wacha kuitetea dhambi dani yako. Wacha kulaumu watu, Mungu na mazingira yako.
- Mtiini Roho Mtakatifu (Yakobo 1:22)
IV. NNE: SILAHA HAZITAFAULU KWA SABABU:
- Mungu amenena hayo,
- Yesu Kristo alishinda vita vyako vyote na ameshinda kila silaha.
- Neno la Mungu ni juu zaidi ya kila silaha.
- Kwa sababu kila silaha ya shetani imepangiwa kutofaulu.
- Kwa sababu Mungu yuko upande wako
Kwa sababu silaha hazitafaulu, hivyo:
- Usiogope (Zaburi 46:1-5)
- Uwe na ujasiri katika Neno,
- Simama katika Bwana.
MWISHO
- Yesu Kristo alikuja tuwe huru kabisa kutoka kwa dhambi, shetani, daimoni, hofu na mauti.
- Hata ingawa tumezungukwa na adui, Kristo ametupa ushindi.
- Vita vyetu pengine ni katika, ndoa, afya na usiano wetu na watu wengine, lalkini ukweli ni, Hakuna silaha itakaye faulu.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
- UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI. - October 19, 2025
- THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR. - October 19, 2025
