Swahili Service

JAMII ILIYOFANYA MAKOSA

MFULULIZO: RUTHU

SOMO: RUTHU 1:1-2.

 

Katika somo letu leo, naomba kukuonyesha jamii iliyoishi katikati ya watu lakini kwa sababu ya wakati mgumu, walifunga virago vyao na kwenda nchi ya Moabu.

Pengine wewe ungesema “kwani kuna shida gani kuhama?” Je, si watu wanahama kila wakati?” hii ni kweli lakini ukiona jambo katika Biblia, lipo hapo kwa sababu.

Mungu aliweka kitabu hiki cha Ruthu katika Biblia hili tupate somo kutokana na maisha yao. Hebu tuone:-

JE, MASKOSA YAO ILIKUWA NINI?

  • Jamii ya Elimeleki na Naomi ilikuwa na shida, lakini walitafuta suluhisho ya shida zao mahali pabaya.
  • Jamii hii ya Elimeleki na Naomi inatufanya kusoma Zaburi 121.
  • Zaburi 121 inatueleza jinsi watu wa siku zile walitafuta jibu katika mahali jibu haliwezi kupatikana.
  • Hawa watu wa Zaburi waliweka sanamu zao juu ya milima.
  • Walipopata shida, walitazama milimani na kuanza safari ya kwenda juu ya hio milima kuomba sanamu zao.
  • Mwandishi wa Zaburi 121 anawacheka hawa watu wanao safari kwenda mbali milimani ya sanamu zao, bila kupata jibu!!
  • Zaburi 121:1, Je, nitayainua macho yangu kutazama milimani? Je, msaada wangu utapatikana milimani?
  • Mfalme Daudi anasema, mimi nipatapo shida, sitayainua macho yangu kutazama milimani, msaada wangu haupatikani milimani, bali msaada wake Daudi ulikuwa katika Bwana!!
  • Zaburi 121:2, mfalme Daudi anasema kwamba “Msaada wangu unatoka kwa Bwana, aliyeumba mbingu na nchi.”
  • Kwa kweli mfalme Daudi anasema “mimi Daudi, sitageukia sanamu za dunia hii kwa msaada ninaohitaji.”
  • Daudi ansema msaada wake haupatikani milimani na sanamu, lakini msaada wake unapatikana kwa Bwana, aliyeumba mbingu na nchi.”
  • Mungu wake mfalme Daudi ni Bwana muumba wa mbingu na nchi.
  • Mfalme Daudi kwa hakika anasema, “mimi sikufanya Mungu ninaye mtumikia lakini ni Bwana Mungu aliyeniumba.”
  • Huyu Mungu wa Daudi ni Yehova aliyeziumba mbingu na nchi.
  • Katika fungu zinazoendelea, mfalme Daudi anaeleza kwa nini yeye anamwelekea Mungu hili apate msaada-Zaburi 121:3-8.
  • Daudi hakufanya makosa watu tunafanya hivi leo.
  • Daudi hakufanya makosa waliofanya kama jamii ya Elimeleki na Naomi.
  • Jamii hii ya Elimeleki na Naomi walienda mahali pasipo kweli kusuluhisha shida zao!!
  • Ruthu 1:1, “Ikawa zamani za waamuzi walipotawala na kuamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.”
  • Na wakati wa njaa, jamii hii waliondoka kutoka nchi ya Mungu, kukaa nchi ya wenye dhambi-Wamoabu.
  • Wamoabu walikuwa wazaliwa wa Lutu na Binti yake-walipotoka Sodoma na Gomora.
  • Badala ya Elimeleki na Naomi kumtegemea Mungu wa Israeli, walichagua kwenda kuishi katika dhambi na wenye dhambi-Moabu.
  • Hakuna jamii nyingine ilihama Bethlehemu isipokuwa Elimeleki na Naomi!!
  • Watu wanapoanza kurudi nyuma wanageukia mahali kupata jibu la shida zao.
  1. Watu wanaporudi nyuma wanageukia ulimwengu na mahusiano (companionships).
  2. Watu wanaporudi nyuma wanageukia utoshelefu na utauwa (contentments).
  3. Watu wanaporudi nyuma wanageukia raha.
  • Naomi na Elimeleki walitoka Bethlehemu Yuda (nyumba ya mikate na sifa) wakaenda Moabu mahali pa laana.
  • Katika kisa hiki Naomi ni picha ya kurudi nyuma (backsliding).
  • Katika mlango huu wa kwanza Ruthu ndiye nyota kuu (starring).

NYUMBA MPYA YA NAOMI-Ruthu 1:2.

“…..wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko.”

  • Leo tunaona watu wengi wa Mungu wanao kaa Moabu ya sasa.
  • Watu wa Mungu wanaporudi nyuma utawakuta mahali pasipo bora kwa mtu wa Mungu kukaa.
  1. Utawakuta wakitazama vipindi ambavyo vinatazamwa na watu wa dunia hii.
  2. Utawakuta katika mikahawa na nyumba za burudani wanapokaa wenye dhambi.
  3. Utawakuta wakitazama TikTok na kupenda content za dunia hii.
  4. Utawakuta katika video stores waking’ang’ania kuchukua video za dunia hii.
  5. Utawakuta katika mall wakati ibada inaendelea.
  • Naomi na nyumba yake walifikia maovu na wakakaa starehe.
  • Mahali pabaya, dhambi, laana, lakini shida zao zitakwisha?
  • “Ikiwa hatutashiba na mkate wa mbinguni, tunaishi kula makombo ya dunia hii.
  • Elimeleki na jamii yake hawakupenda mikate na sifa za Bethlehemu. Walienda Moabu kujishibisha, lakini walipokuwa kule:-
  1. Walikaa huko (settled).
  2. Walikaa katika giza ya Moabu na kuipenda.
  3. Hawakuwa na mpango wa kurudi Bethlehemu ya Yuda.
  • Walipendelea kuishi huko Moabu hawakumiss ibada za Mungu wa Israeli tena.
  • Hawakujali tena sadaka na zaka zao, walizitumia kwa mahitaji yao!!
  • Waliendelea kukaa huko Moabu.
  • Walipata starehe katikati ya watu wa Moabu, wakawa kama wao!!
  • Walipendelea kukaa huko Moabu,  watu wa Moabu walipenda na kuwa starehe na wao.
  • Dunia haiwezi kuwa starehe na mtu wa kuokoka!!
  • Ikiwa watu wa dunia hii, walevi, washerati, wezi, wanao starehe na wewe, basi kunao shida.
  • Watu wa dunia hii wanapenda Wakristo wa kweli kuwavumilia (tolerant).
  • Kama wakristo wa kweli, dunia haiwezi kuwa starehe na sisi.

WALIENDELEA KUISHI NA KUKAA MOABU KWA SABABU WAMOABU WALIKUWA NA KITU CHA KUWAPA.

  • Kumbuka Elimeleki na Naomi walitoka Bethlehemu Yuda kwa sababu ya njaa.
  • Walikuja Moabu kwa maana Moabu kulikuwa na kitu cha kuwapa-chakula. Israeli hapakuwa na chakula.
  • Kumbuka wale waliendelea kuishi na kukaa Bethlehemu hawakufa njaa!!
  • Shetani aliwadanganya Elimeleki na Naomi!!
  1. Shetani amefaulu kuwadanganya watu wa Mungu kwamba dunia ndiyo inanufaisha (satisfaction).
  • Lakini kulingana na Biblia, Mungu ndiye anawapa watu utajiri (Kumbukumbu 18:8).
  • Utajiri wa shetani upo, lakini ni majuto kali sana.
  • Sadaka za shetani ni ile nafsi yako na watoto wako.
  • Utajiri anaopeana Mungu ni utajiri wa furaha na amani-Zaburi 1:3.
  1. Shetani amewadanganya wengi kwamba ulinzi na usalama unapatikana kwake (prosperity).
  • Wakristo wengi wameenda Moabu kutafuta usalama na ulinzi wa biashara zao na nyumba zao.
  • Lakini kumbuka Mungu ndiye aletaye usalama na ulinzi-Ayubu 1:10.
  • Ushuhuda wa shetani ni kwamba Mungu ndiye analeta utajiri, ulinzi na usalama-Ayubu 1:10.
  1. Shetani amewadanganya wengi kwamba ni yeye anayeleta utoshelevu (provision).
  • Lakini Yesu Kristo alisema “tafuta kwanza ufalme wake…..”-Mathayo 6:33.
  • Utoshelevu unatoka kwa Mungu-Zaburi 37:3-5.
  • Mungu ndiye utajiri wako, ulinzi, usalama na utoshelevu wako.

MWISHO

  • Utajua kwamba umerudi nyuma wakati umeketi na kukaa salama na watu wa dunia hii (Wamoabu).
  • Unapoishi na kukaa na furaha na watu wa Moabu.
  • Wakati unaona kwamba watu wa Moabu ndio wako na ufunguo wa maendeleo yako.
  • Kataa kukaa Moabu-ishi Bethlehemu-Yuda kwa vyovyote vile. 
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *