Swahili Service

JINSI YA KUPINDUA LAANA

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: 2 WAFALME 5:17; 7:9; 8:4-5; WAGALATIA 3:13.

 

Kuna haina mbili za laana. Kwanza ni laana inayopata mtu kwa kumwasi Mungu kwa dhambi zake mtu huyo, pili kuna laana inayompata mtu kwa sababu ya makosa juu ya mamlaka ya wazazi, wakuu wa kiroho, serikali nk. Pia laana inaweza kuja kwa sababu ya dhambi za binafsi.

Nchi na watu binafsi wanapo kopa fedha wanajiweka katika laana ya umaskini. Tendo la ndoa nje ya ndoa inaleta STD, miraa na mug’uka ni laana juu ya nchi kwa sababu ya ulevi.

Kuvunja ndoa, kutupa watoto nje ya jamii ni laana juu ya nchi.

Ulevi na ajali zinazoletwa na madereva walevi ni laana juu ya watu wa nchi yao. Gehazi mtumishi wa Elisha alipata laana kutoka kwa Elisha kwa sbabu ya ulafi wake. Baada ya miaka saba laana juu ya Gehazi pamoja na jamii yake ilipata kupinduliwa!!

Hivi leo twaongea juu ya laana. Je, laana ni nini? Je, laana inaweza kukupata? Biblia inasema nini juu ya laana? Hebu tuone:-

JE, LAANA NI NINI?

  1. Laana ni kumtakia mtu mabaya na kutamka mabaya juu ya mtu.
  2. Watu wengi wanahisi kwamba kunao laana juu ya maisha yao na juu ya jamii zao.
  3. Katika nchi nyingi za Africa, kuna voodo, uchawi, wachawi wanalipwa kuweka laana juu ya watu.
  • Wengine wanatumia mapepo na majini kuwavamia watu.
  • Lakini unapokuwa na Yesu Kristo laana zinakukwepa-Luka 10:19; 1 Yohana 4:4.
  • Yesu Kristo anatupa uwezo juu ya pepo na laana-Mathayo 10:1.
  • Katika Biblia tunaona laana juu ya watu.
  • Laana kutoka kwa Mungu ni jambo la kutisha sana, ni ghadhabu na hukumu ya Mungu-Wagalatia 3:10; Kumbukukmbu 27:26.
  • Magonjwa na mauti ni ishara ya laana-Isa. 24:6.

JE, LAANA INAWEZA KUPINDULIWA?

Gehazi alipata laana-2 Wafalme 5:27.

  • Gehazi alipopokea bidhaa kutoka kwa Naamani kinyume na sababu ya ulafi, Elisha alitamka laana juu ya Gehazi.
  • Ukoma wa Naamani ulimpata Gehazi “Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako hata milele, naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.”
  • Jambo la kushangaza-1 Wafalme 8:4-6. Tunamwona Gehazi katika nyuma ya mfalme Joramu mwana wa Ahabu bila ukoma!!
  • Hapa Gehazi anaitwa “mtumishi wa Elisha.” Gehazi anaeleza mfalme Joramu jinsi nabii Elisha alimfufua mwana wa yule mjane wa Shunemu.
  • Haikuwezekana Gehazi kuweko kwa mfalme Joramu kama angali na ukoma-Walawi 13:45-46.
  • Laana ya Elisha juu ya Gehazi ilikuwa “Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako hata milele-2 Wafalme 5:27.
  • Hii ilikuwa laana ya milelel kwa sababu ya uamuzi mbaya wa Gehazi.
  • Hebu tazama jinsi Mungu anamtumia Gehazi. Hapo akimweleza mfalme Mshunemu na jinsi mwanaye alifufuliwa kutoka kwa wafu na nabii Elisha, pale pale yule mwanamke na mwanaye kwa mfalme!!
  • Elisha alikuwa ameshauri yule mwanamke kuhama kwa muda kwa kuwa kutakuwa na njaa kuu katika nchi.
  • Huyu mwanamke alipoenda zake watu walichukua shamba lake, sasa amefika kwa mfalme kuomba msaada.

Laana ya Gehazi ilipinduliwa-2 Wafalme 7:1-9.

  • Mfalme Beni-Hadadi (Shamu) aliuhusuru Samaria kwa muda mrefu, hivyo njaa nyingi ikawapata.
  • Kulikuwa na wenye ukoma wanne mle Samaria, hawa wenye ukoma walikuwa Gehazi na wanaye watu-2 Wafalme 7:9.
  • Kitabu cha Wayahudi (Talmud) kinasema kuwa hawa wenye ukoma walikuwa Gehazi na wanaye (Satah 47).
  • Baada ya miaka 7 Gehazi alitubu dhambi zake, neema ya Mungu ilimponya.
  • Talmud inasema hukumu ya Elisha juu ya Gehazi ilikuwa kali zaidi-Yer. Sunh 29.

MAPINDUZI YALIO MAKUU ZAIDI-YESU KRISTO.

Matokeo ya dhambi.

  • Mbele ya Adamu na Hawa kufanya dhambi waliishi katika ulimwengu safi, hakukuwa na dhambi, maovu na ugaidi. Hakukuwa na magonjwa na mauti.
  • Dhambi inapoingia duniani shida zote tunazoona ziliingia duniani.
  • Kuvunjika kwa ndoa, ulevi, chuki, tamaa, kiburi, utumwa, ndoa, vita na ugonjwa.
  • Maovu yote yalikuja kwa sababu ya dhambi.
  • Lakini kupitia kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo laana zetu zilivunjika kwa damu yake-2 Wakorintho 5:21.
  • Yesu Kristo ametukomboa kutoka kwa dhambi-Wagalatia 3:13; Wakolosai 2:14.

Laana zetu zimepinduliwa-Kumbukumbu 23:5.

  • Tulio ndani ya Yesu Kristo tumekombolewa, tunaenda Yerusalemu mpya-Ufunuo 22:3.

MWISHO

  • Laana zetu zilipinduliwa kwa msalaba wa Yesu Kristo.
  • Leo ikiwa utahitaji ukombozi wowote mjie Yesu Kristo.
  • Yesu akikuweka huru, utakuwa huru kabisa-Yohana 8:36
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “JINSI YA KUPINDUA LAANA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *